Jun 8, 2020
Epuka Tabia Ya Aina Hii Katika Safari Yako Ya Mafanikio.
Watu
wengi wanashindwa kufanya vizuri katika maeneo wanayoyafanyiaka kazi kwa sababu
ya kukosa kwao uwezo wa kujiamini kwenye yale wanayoyafanya. Wao wamekubwa na
tatizo kubwa la kujilinganisha uwezo wao
kwenye yale wanayoyafanya na watu
wengine wanaofanya mambo kama yale wanayofanya wao.
Kwa
kitendo hiki kimesababisha watu hao kujiona kama vile hawajui sana
wakijilinganisha na watu wengine. Pia
kitendo cha kujilinganisha na wengine kimesabasha watu wengine wajione hawana
thamani na uwezo wa kufanya vizuri zaidi.
Kwa
muktadha huo, unachopaswa kuelewa ni kwamba wakati mwenyezi Mungu alipomuumba
mwanadamu alimpa kila mtu uwezo wake binafsi uwezo ambao huwa haufanani na mtu
mwingine, kama ndivyo hivyo kwanini uendelee kujilinganisha na wengine.
Tambua
kitendo ambacho unakifanya cha kujilinganisha wewe na watu wengine ni kinyume na sheria za mafanikio pia
kitakufanya ujione kama vile hujui na wakati mwingine kitakuondelea kabisa
uwezo wako wa kujiamini kwenye kila eneo unalofanyia kazi au unalotaka kufanyia
kazi.
Hivyo
ukiwa unataka kufanikiwa katika eneo fulani ambalo unalifanyia kazi basi,
unatakiwa uache mara moja tabia yako ya kujilinganisha na wengine kwa sababu
unajiua wewe mwenyewe pasipo kujua. Unatakiwa kuelewa uwezo wako wa kufanya
jambo fulani ni mkubwa sana zaidi ya unavyofikiria.
Na
ndiyo maana upo usemi mmoja unasema “Samaki hawezi kupanda juu ya mti, ngedere
hawezi kukimbia kama farasi, baadhi ya ndege pori hawewezi kuogelea. Hii ikiwa na
maana kila mmoja ana uwezo wake wa kufanya vizuri zaidi kutokana na mazingira
ambayo ameyazoea, hivyo ukimwambia samaki apande juu ya mti utaishia tu kumlaumu
kwamba ni mjinga, lakini ukweli ulio wazi kwamba siyo mjinga bali siyo sehemu
yake sahihihi aliyeizoea.
Samaki
uwezo wake mkubwa upo kwenye maji hii kutokana na uwezo wake aliyeoumbwa nao wa
kufanyia kazi na kufurahia maisha yake katika maji. Hivyo hata wewe furahia uwezo ulio nao acha
kujilinganisha na wengine kwa sababu kila mmoja ana uwezo wake wa kufanya jambo
fulani kutokana na mazingira aliyeyazoea.
Kumbuka
unapojilinganisha uwezo wako na mtu mwingine unafanya makosa makubwa sana kwa
sababu kila mmoja wetu ameubwa na uwezo wake.
Imeandikwa na Afisa Mipango: Benson
Chonya.
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.