Jun 25, 2020
Mambo Muhimu Mnapaswa Kuelewa Wakati Mnapitia Nyakati Ngumu Kiuchumi Kwenye Mahusiano Ya Ndoa.
Kuna
wakati katika maisha ya mahusiano yako
ya ndoa unaweza usiyaelewe kabisa, hii ni kwa sababu kuna wakati mnaweza
mkajikuta katika maisha hayo ya ndoa mnakata tamaa kabisa ya kuendelea kuishi
pamoja, hii ni kwa sababu ya ugumu wa maisha ambao mnaupitia.
Tumekuwa
mashuhuda wazuri sana kwa kuona ndoa nyingi zikivunjika katika karne hii, hii ni kwa sababu ya ugumu wa kiuchumi ambao
umejitokeza katikati ya safari ya mahusiano hayo ya ndoa.
Zipo
sababu nyingi ambazo husababisha mahusiano mengi ya ndoa kufa ila kubwa zaidi ni suala la kuyumba kwa
kiuchumi baina ya wanandoa hao husasani ukosefu wa kifedha katika kutekeleza
mambo mbalimbali.
Wapo pia baadhi wa wanawake wamediriki hata
kunyanyua vinywa vyao kuwatamkia waume zao kuwaita wanaume suluari hii yote
ikiwa waumeo hao wameyumba kiuchumi hawawapi mahitaji yao ya kifedha kama
ilivyokuwa hapo awali.
Kwani
hapo awali, mwanzo wa mahusiano hayo walikuwa wanapewa kila kitu kutoka kwa
wanaume wao, ila kwa sasa wamekuwa hawapati tena kile walichokuwa wanapewa
mwanzo. Ikumbukwe kuwa wanawake hao wamesahau kwamba katika safari mahusiano ya ndoa kuna kupanda na kushuka.
Kuna
wakati mtakuwa katika hali nzuri kiuchumi na kuna wakati mtakuwa na hali mbaya
sana kiuchumi. Hivyo mkiona mnapitia wakati mzuri kiuchumi katika mahusiano
yenu mnapaswa kumshukuru mwenyezi Mungu.
Pia
mnapopitia nyakati ngumu kiuchumi katika mahusiano yenu ya ndoa ni kwamba
mnapata kumshukuru Mungu kwa hatua ambayo mnapitia pia, Hii ni kwa sababu wapo
baadhi ya watu katika mahusiano ya ndoa wanapopitia kipindi ambacho wameyumba
kiuchumi wao hukata tamaa kabisa.
Wengi
wao wamefika hatua ya kutoona thamani ya
kuendelea kuishi tena kwa pamoja kwa sababu eti mambo yamekuwa hayaendi sawa. Ukiona hata wewe umefikia
hatua hii kumbuka kwamba mnakaribisha shetani aweze kuyasambaratisha mahusiano
yenu.
Kitu
pekee ambacho mnapaswa kuelewa wakati mnapitia nyakati ngumu kwenye mahusiano
ya ndoa hususani suala la kuyumba kiuchumi mnapaswa kufanya mambo yafuatayo;
Mtangulizeni Mungu;
Kama
nilivyosema hapo awali kwamba katika mahusiano ya ndoa kuna kupanda na kushuka,
kuna wakati mtakuwa vizuri kiuchumi na kuna wakati pia mtakuwa katika nyakati
ngumu.
Hivyo
inapotokea hali kama hii mnapaswa
kuelewa Mungu ndiye muweza wa kila jambo, hivyo mnapaswa kumuomba awasaidie
kuyalinda mahusiano yenu ya ndoa, vile vile
mnapaswa kumuomba yeye ili aweze
kuwasaidia katika kunyanyuka na kukua kiuchumi.
Msiruhusu Mawazo hasi
yawatawale.
Inapotokea
mmeyumba kiuchumi hampaswi kuyafanya mawazo hasi yatawale akili zenu, hii ni
kwa sababu ninyi ni watoto wema wa Mwenyezi Mungu na mawazo hasi ni ya shetani.
Hivyo
mnapoyaruhusu mawazo hasi yatawale akili zetu ni kwamba ninyi mtaona njia bora
ya kutatua tatizo hilo ni kuachana na kufanya kila mtu afanye mambo yake,
kitendo hicho si kizuri kwa sababu mnakiuka kiapo chenu cha ndoa pia
mnamkaribisha shetani aweze kuwatala vyema.
Shirikianeni katika kazi.
Miongoni
mwa mambo yatakayowasidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kuwa na mahusiano
ya ndoa yaliyobora ni pamoja na kushirikiana vyema katika kufanya kazi.
Ni
muhimu kushirikiana vyema katika kufanya
kazi kwa sababu hata pale inapotokea kuna anguko la kiuchumi basi wote muweze
kujua ni wapi ambapo pamewafanya mpate anguko hilo la kiuchumi.
Jambo
hili ni muhimu sana, hii ni kwa sababu ndoa nyingi zinaamini mtu mmoja ndiye
ambaye atahusika kuinua uchumi wa familia, hili si kweli bali ukweli mnatakiwa
kushirikiana vizuri kwenye kila kazi mnayoifanya ili mjue faida na hasara
mnayoipata katika kazi fulani muifanyayo.
Jifunzeni kuweka akiba.
Ili
msiweze kupata anguko la kiuchumi kwa namna moja ama nyingine basi kila
wanandoa ni vyema wakajifunza kuweka akiba. Kuweka akiba ni muhimu sana kwa
sababu kuna wakati akiba hiyo hutumika hasa pale unapokuwa umepatwa na anguko
kiuchumi.
Hivyo
kivyovyote vile wanandoa mnapaswa kujifunza juu ya utaratibu wa kuwekea akiba
ila akiba hiyo iweze kuwasaidia baadae
hasa pale mnapopata angulo la kiuchumi.
Jifunze kutokana na makosa.
Kuanguka
kiuchumi isiwe sababu kwa wanandoa kukata tamaa bali liwe na somo kwao kuona ni
wapi ambapo wamekosea na kurekebisha makosa yao.
Pia
ikumbukwe kuwa unafuu wa kila jambo hususani suala la unguko la kiuchumi kwa
wanandoa hutokana na anguko hilo kama somo la kuweze kurekebisha makosa ili
baadae waweze kuwa vizuri zaidi.
Hivyo
ikiwa mmepata anguko katika mahusiano yenu ya ndoa mnapaswa kujifunza namna ya
kutokana na anguko hilo ila baadae msiweze kuanguka tena.
Mkiyazingatia
hayo yote ambayo nimeyaeleza kwa siku ya leo ni kwamba maisha yenu ya ndoa
yatakuwa ni mzuri sana, kila mmoja wetu atayafurahia mahusiano hayo. Asante.
Ndimi; Afisa Mipango Benson Chonya
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.