google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 26, 2020

HADITHI; Acha Kufukuza Furaha, Kwa Sababu Ya Vitu Hivi…

1 comment :
Hapo enzi za kale, kulikuwa na mzee aliyekuwa akiishi kijijini. Mzee huyu naweza kusema, alikuwa ni mmoja wa watu wa bahati mbaya sana ulimwenguni, kwa nini nasema hivi, ni kwa sababu, karibu kijiji kizima kilikuwa  kimemchoka.
Mzee huyu alikuwa amechokwa kwa sababu gani, kwani kila wakati yeye alikuwa anatetemeka, kila wakati alikuwa akilalamika tu na kila wakati alikuwa katika hali mbaya, sura yake ikiwa imekunjamana kwa kukunja uso.
Kwa jinsi mzee huyu alivyokuwa akizidi kuishi kwa muda mrefu, maneno yake yalizidi kuwa sumu kwa wengi na yasiyopendeza. Kwa hali hii watu walimwepuka, kwa sababu ya kauli zake mbovu na mbaya za kukera.

Mzee huyu aliunda hisia za kutokuwa na furaha kwa wengine. Kutokana na hisia hizo, pia alijikuta naye akichukiwa na wana kijiji,  kwa sababu ya hisia zake hizo na tabia yake hiyo ambayo alikuwa amejitengenezea.
Lakini siku moja, alipokuwa na umri wa miaka themanini, jambo la kushangaza lilitokea. Mara moja kila mtu alianza kusikia uvumi huo, eti kwamba "mtu mzee anafurahi leo, halalamiki juu ya kitu chochote, anatabasamu, na hata uso wake unatabasamu."
Kijiji kizima kilikusanyika pamoja. Mzee huyo aliulizwa na wana kijiji, nini kimetokea na kwa nini leo anaonekana ana furaha? Jibu, alilotoa mzee huyo lilishangaza kidogo wengi, kwani aliwaambia hivi.
"Hakuna kitu maalum kilichotokea, ila kwa miaka themanini  najuta nimekuwa nikiifukuzia  furaha, na sikuwa nikiipata. Na hapo niliamua kuishi bila furaha, kumbe nilikuwa najitesa na sikujua kumbe furaha ipo ndani mwangu tu”
….”Ndio maana nimefurahi sasa baada ya kujua, vitu vya nje haviwezi kukupa furaha, bali furaha ya kweli inaanza na wewe mwenyewe na mtazamo wako ulionao, lakini kutafuta furaha ya nje huko ni kujichosha wewe.”
Fundisho la hadithi hii fupi ni nini? Kwenye maisha yako, acha kufukuza furaha kwa vitu vya nje, furahia maisha yako.

Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com



1 comment :

  1. Nimependezwa sana na mafundisho Yoko mwl.sasa naomba umuunge kwenye group lako la WhatsApp.namba yangu ni 0766650084

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.