Jun 3, 2020
Misingi Mitatu Ya Kuzingatia Unapoamua Kuweka Malengo.
Ili
uweze kufikia malengo yako, ipo misingi ya kuzingatia na kuifanyia kazi kila
siku. Kama utashindwa kuifanyia kazi
misingi hiyo, nikwambie kwako itakuwa ni kazi ngumu sana kuweza
kufikia malengo yako uliyonayo.
Tunaona
watu wengi wanakuwa na malengo, lakini watu hawa wanakuwa wanashindwa kuyafikia
kwa sababu wanakuwa hawana misingi sahihi ya kuweza kuyafikia. Je, uko tayari
kuijua misingi ya kufata ili kufikia malengo yako?
Kama
ni ndio, karibu ujifunze misingi hiyo kupitia makala haya;-
1. Weka malengo yanayofikika.
Unapoamua
kuweka malengo yako na ukawa na nia thabiti ya kuyafikia, unatakiwa kuhakikisha
unajiwekea malengo ambayo unaweza kuyafikia. Usiweke malengo ilimradi tu, weka
malengo ya wewe kuweza kuyafikia.
Hapa
katika kufanikisha zoezi hili, usijaribu hata kidogo kuweka malengo makubwa
sana na ambayo kwenye utekelezaji yatakukatisha tamaa. Weka malengo ambayo yako
ndani ya uwezo wako na una uwezo ya kuyamudu kuyafikia.
2. Usijiwekee malengo mengi sana.
Kujiwekea
malengo kwa wakati mmoja huko ni sawa na kujiandaa kushindwa. Weka malengo
ambayo ni machache na utayafanya kwa uhakika, kuliko kuweka malengo ambayo ni
mengi na inakuwa shida kwako kuyafikia.
Kwa mfano
unaweza ukaweka malengo ya kusoma kitabu kimoja kila mwezi. Unaweza ukaweka
lengo la kuboresha afya yako kila siku kwa kukimbia kidogo. Unapoweka lengo
moja, hiyo inakupa hamasa na nguvu ya kuweza kutenda zaidi na zaidi.
3. Fanya marekebisho ya malengo yako
inapohitajika.
Usiweke
malengo tu na ukaamua kuyaacha kama yalivyo, jitahidi sana, kufanya marekebisho
ya malengo yako kila wakati hasa pale inapohitajika. Kuweka malengo kwa
kuyamiminia zege huko ni kujipoteza.
Ukizingatia
mambo hayo matatu, utakuwa upo kwenye misingi sahihi wa kuweza kuyatimiza
malengo yako au kuyafikia kabisa. Kitu kikubwa kwako ni kuamua kuchukua hatua
za kila siku. Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo.
Nikutakie
kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO
ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.