google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 5, 2020

Mambo Matatu Ya Kuyaboresha Ili Kuwa Mtu Wa Mafanikio.

No comments :
Kuna vitu ambavyo kila mtu anahitajika sana kuviboresha kila siku, ili kufikia ngazi fulani ya mafanikio. Kama hautaweza kuboresha vitu au mambo hayo, ni wazi utakwama na hautafanikiwa kwenye maisha yako.
Na kwa bahati nzuri mambo hayo si magumu kuyaboresha, ila wengi huwa wanashindwa kuyaboresha, labda niseme kwa sababu ya uzembe au kuamua tu. Leo naomba nikushirikishe mambo matatu tu, kama utayaboresha basi umefanikiwa.
1. Boresha bidhaa, kama una bidhaa ambayo unaiuza, hakikisha bidhaa hiyo unaiboresha na mpaka iwe ya viwango vya juu. Usikubali kukaa na bidhaa kwa muda mrefu pasipo kuiboresha, kwani ukiiboresha, itakusaidia sana.
Utakuwa unajiweka kwenye wakati mgumu sana kama huboreshi bidhaa yako. Kwa hiyo kama unauza vitu fulani hivi, viboreshe. Kama unatoa huduma ya aina fulabi hivi, pia huduma hiyo iboreshe bila hata ya kinyongo na itakupa mafanikio makubwa.

2. Boresha njia, usiishie tu kuboresha hiyo bidhaa jifunze na kuboresha njia za kuuza bidhaa hiyo. Ukiwa na mbinu mbalimbali za kuuza bidhaa hiyo, huo ni uhakika wa njia ya kukupeleka kwenye mafanikio makubwa.
Kila siku jiulize, utafanya kwa njia ipi na ambayo njia hiyo itakupa matokeo sahihi ya wewe kusonga mbele. Tafuta njia sahihi zitakazo kupa wateja wengi au mafanikio makubwa. Uelewe hivi ukiwa na njia sahihi utafanikiwa.
3. Jiboreshe wewe, kila siku jenga mwonekano mpya, jenga lugha mpya kwa wateja wako na hiyo ni njia sahihi ya kukufikisha kwenye mafanikio. Unapojiboresha wewe, unakuwa unaleta mvuto kwa biashara yako.
Acha kila wakati kuonekana ni mtu wa kukunja sura, jenga ukarimu kwa wateja wako na watakupenda na utakuwa unawavutia sana. Ukijiboresha wewe, inakusaidia kuleta mafanikio makubwa ya kibiashara kwako.
Hayo, ndio mambo matatu yanaweza yakakufanya ukafanikiwa sana, ikiwa utayazingatia na kuyachulia hatua za kiutendaji kwa kuyaboresha. Unasita nini, ni wakati wako wa kuchukua hatua na kuyaboresha mambo hayo.

Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua. 
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

Blog; dirayamafanikio.blogspot.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.