Jun 4, 2020
Mambo Ya Kufanya Ili Kuwa Mshindi Katika Safari Yako Ya Ujasiriamali.
Zipo
hadithi nyingi sana za watu, ambazo zinaeleza ili kufanikiwa katika safari ya ujasiriamali unatakiwa kufanya hili
au lile. Na kwa bahati nzuri au mbaya
hadithi hizi ziko tofauti baina ya mtu na mtu.
Pasipo
kujali ni nini kinachozungumzwa sana katika safari ya kuelekea kwenye ujasiriamali,
hapa kupitia makala haya nataka nikushurikishe, mambo ya msingi ya kufanya ili
kuwa mshindi katika safari ya mafanikio.
Ni
mambo yapi ambayo unatakiwa uyafanye ili uweze kuwa mshindi katika safari yako
ya mafanikio? Sasa karibu ili uweze kujifunza mambo hayo;-
1. Tengeneza fursa.
Inaweza
kuwa ni kosa kubwa kwako kama kila wakati unasubiri fursa ikufate pale na
badala ya kuitengeneza. Kama unafanya hivyo yaani kusubiri fursa, nakuhakikishia
utakuwa unachelewa sana kufikia mafanikio yako.
Kama
kuna kitu unatakiwa kukifanya, hebu kifanye na acha kusubiri subiri hadi mambo
yawe sawa sana. Ukizidi kusubiri unaweza ukajikuta umechelewa kabisa. Kama ipo
fursa ya kazi ambayo hata hailipi sana, hebu anza kuifanya hiyo kazi, itakulipa
baadae.
2. Endelea kujifunza.
Wajasiriamali
wa kweli ni watu wa kujifunza kila siku, nawe pia kama unahitaji kuwa mshindi
katika safari ya ujasiriamali, unatakiwa tu kwa wewe kuamua kujifunza haswa na
tena kila siku bila hata ya kupoteza muda.
Kwa
chochote kile unachokifanya, kitafutie maarifa zaidi na hakikisha unakijua
vizuri ili kuweza kutimiza ndoto zako za kufika kwenye ujasiriamali wenye
mafanikio. Jifunze, jifunze, na acha kusimama kujifunza kila siku jifunze na
utafika mbali kimafanikio.
3. Rekebisha makosa yako mara kwa mara.
Lipo
eneo ambalo unatakiwa kufika kimafanikio, sasa ili kufika eneo hilo
kimafanikio, inabidi ukubali ukikosea kurekebisha makosa yako. Acha kujiachia
tu na kusahau kurekesbisha makosa yako, kwani ukishindwa hivyo utakwama.
Watu
wote ambao wanarekesbisha makosa yao, ni watu ambao wanaweza kufanikiwa na kufika
mbali sana kimafanikio. Unaweza ukawa ni miongoni mwa watu hao, kubali
kurekebisaha makosa yako ili uwe mshindi.
4. Jifunze kutokana na mazingira.
Ni
muhimu na na ni msingi kujifunza kutona na mazingira yanayo kuzunguka. Jaribu
kuchunguza eneo ulilopo lina fursa gani na watu wa eneo hilo wanahitaji nini,
kwa kujua hivyo itakuwa ni nia sahihi kwako ya kujifunza kutokana na mazingira.
Kama
ikitokea utashindwa kujifunza kutokana na mazingira basi elewa utakwama sana na
utashindwa kufanikiwa. Magfanikio ya kweli yanakuja na kujengwa kama utajua
namna ya wewe kujifunza kutoka na na mazingira yako na kuchukua hatua.
5. Kuwa na mwendelezo wa kufanya.
Ikiwa
unataka kuwa mshindi katika safari yako ya ujasiriamli, hakikisha una
mwendelezo wa kufanya. Usiwe mtu wa kuishia kati. Kama kuna kitu umeamua
kukifanya, fanya ufanyavyo ila mwendelezo huo unatakiwa kuwa nao.
Wengi
si wazuri sana katika kuwa na mwendelezo ni watu ambao akianza jambo hilo leo,
ni rahisi tu kumkuta mtu huyo jambo hilo kesha achana nalo na hana habari.
Ukijijengea nidhamu ya kuwa na mwendelezo, sio siri utafanikiwa.
Ukizingatia
na kuyafatilia mambo hayo na ukayachukulia hatua, yatakusaidia wewe kuweza kuwa
mshindi katika safari yako ya ujasiriamali.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua.
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.