Jun 9, 2020
Njia Nne Za Kukabiliana Na Kukosolewa Katika Maisha.
Katika
dunia hii yapo mambo ambayo unaweza kuyakwepa, ila linapokuja suala la
kukosolewa na watu wengine kwenye kile unachokifanya au unachotaka kufanya huwa
hakuepukiki na huwezi kukwepa, lazima ukosolewe.
Maisha
ndivyo yalivyo, kwa vyovyote vile ni lazima watu wakukosoe, katika kukosoa huko
kupo kutakokujenga na kupo ambako kutakufanya upoteze mwelekeo kabisa kwenye
kitu unachokifanya au unachotaka kufanya, hii inategemea na wewe.
Kama
nilivyosema hapo awali kwamba kukosolewa kupo, kila mtu anakabiliwa na
kukosolewa. Kukosolewa hakukwepeki katika maisha na ndio ukweli ulivyo. Kama hutaki
kukoselewa, basi usifanye kitu, na usiseme kitu chochote.
Haijalishi
umekosolewa mara ngapi, haijalishi umekosolewa kwa miaka mingapi, unatakiwa
ujifunze kutawala kukosolewa huko. Hivyo, katika makala haya ya leo nitaeleza
kwa kina njia nne za kukabiliana na kukoselewa.
1. Potezea kukosolewa kwa njia hasi.
Kila
mmoja wetu ana malengo yake ambayo amepanga kuyatimiza baada ya muda fulani,
hivyo linapokuja suala la kukoselewa husasani suala la watu wengine kukukatisha
tamaa wewe endelea kupambana kwa sababau hayo ni maoni yao hasi.
Kwa
mfano unaweza ukawasikia watu wakikukosoa kwamba huwezi kufanikiwa kwenye jambo
unalolifanya huenda ikawa ni katika
mahusiano, biashara, elimu na mambo mengine kama hayo, wewe puuza hiyo habari.
Kumbuka hayo ni maoni yao binafsi na hakuna
wakuyazuia, ila unachotakiwa ni kujifunza kupokea maoni hayo kwa njia hasi, kwa
sababu kama utapokea kwa njia ya kauamini
kuwa huwezi kufanikiwa katika jambo fulani ni kweli hautaweza.
2. Thamini unapokoselewa kwa njia ya
kujengwa.
Kama
nilivyosema hapo awali kwamba kuna faida mbili za kukoselewa ambazo ni
kukujenga au kukupotezea mwelekeo. Wakati mwingine siyo kila anayekukosea ana
lengo ya kukatisha tamaa bali lengo lake linakuwa ni kukufundisha mambo ya
muhimu.
Hivyo
wakati mwingine usipuuze watu wengine
wanavyokukosoa kwa sababu watu wengine wanakuja kwako kama daraja ambalo
litakusaidia wewe kwa namna moja ama nyingine kuweza kufanya vizuri zaidi.
Wao
kazi yao kwa ni kuona makosa yako na kukupa elimu ya kuweza kufanya vizuri
zaidi ili uweze kuboresha zaidi kile unachofanya. Kwa hiyo thamini sana
kukoselea kwa njia chanya kutakujenga na kukusaidia kufanikiwa.
Kumbuka
unapokosolewa iwe ni kwenye biashara, mahusiano, familia na mambo mengine,
unachopaswa kuelewa ni kwamba si kila anayekokosoa lengo lake huwa ni baya, hapana wakati
mwingine watu wanapokukosoa wanakusaidia kuweza kukujenga na kukuimarisha zaidi
hivyo usiwapuuze.
3. Chukulia kukosolewa ni sehemu ya
maisha.
Naam,
wala hujakosea kusoma upo sahihi kabisa, kama nilivyosema hapo
awali kwamba kukosolewa kupo na kutaendelea kuwepo na hivyo ndivyo
ilivyo kwa sababu maisha yana pande mbili yaani watu kupenda kile
wanachokifanya pia wapo baadhi ya watu hawatapenda kile unachokifanya,
Watu
wanaokupenda watakukosoa kwenye kile unachofanya ili uweze kufanya vizuri
zaidi, ila wale wasiokupenda watakukosoa
kwenye kile unachofanya ili usiweze kufanya vizuri. Maneno na mitazamo ya watu ipo, uliikuta na
utaicha, hivyo usigope na nani anasema nini juu yako.
Kitu
cha muhimu ambacho unapaswa kukizingatia
ni kuhakisha watu wote waache waendelea kukukosoa kwa sababu watu hao
hawaepukiki, ila kwa upande wako fanya upembuzi kwa kuona nani yupo sahihi
kisha uchue maoni ya mtu huyo kwenye kile unachokifanya ili kiweze kufanikiwa.
Kumbuka kukosolewa ni sehemu ya maisha.
4. Usifikiri kukosolewa kunakuhusu moja
kwa moja.
Kukosolewa
katika maisha kupo, ila siyo kila anayekukosoa ana lengo zuri la moja kwa moja na wewe, bali unachopaswa
kulewa ni kwamba unatakiwa kuchagua watu
wanasema nini kuhusu wewe.
Kama
yale wanayokukosoa ni ya kujenga basi hakikisha
unayabeba na kuyafanya yakufae
maishani kwenye kile unachokifanya au unachotaka kufanya ila kama si ya kukujenga unapaswa kuachana nayo na kuacha
maisha yaendelee.
Mpaka
kufikia hapo kwa leo sina la ziada, ni imani yangu kubwa kwamba kuna mambo
muhimu ya msingi ambayo umejifunza
yatakayokusaidia kwa namna moja ama nyingine ya kukabiliana na
kukosolewa kwenye mambo unayoyafanya au unayotaka kufanya.
Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.