Jun 2, 2015
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuongeza Thamani Zaidi Katika Maisha Yako.
Je, unathaminiwa
na watu katika
jamii? Kama unathaminiwa ni
mambo gani yanayokufanya uone kuwa
unathiminiwa?. Kama unathaminiwa ni mambo
gani yanayokufanya uhisi
hivyo? Moja katika mahitaji
muhimu ya binadamu
baada ya chakula, mavazi na
malazi ni kuheshimiwa
na kuthaminiwa na
jamii.
Binadamu ni
kiumbe pekee aliye na
daraja kuliko viumbe
wengine wote. Kinachompandisha hadhi
kuliko viumbe wengine
ni uwezo wake
wa kufikiri, ambao
umemwezesha kuyatawala mazingira
yake na kuyatumia
ili kuboresha maisha
yake.
Maendeleo yetu
na maisha yetu
kwa jumla yanawategemea watu.
Tunachohitaji kutoka kwao
ni kututhamini, kutujali
na kutupenda. Watu
watutathamini kutokana na
matendo yetu na
jinsi tunavyoonekana kwao.
Hii ni kwa
sababu imethibitishwa kuwa
watu wenye muonekano
wa hali ya juu mara nyingi
huwa ndiyo mwenye
mafanikio katika maisha.
Licha ya
muonekano wetu kufanya
kuthaminiwe na watu,
unadhifu pia huwa
na uhusiano na
fikra zetu. Ndiyo
maana viongozi wa
dini, mashehe, mapadri, makasisi
na wachungaji huvaa
mavazi maalum ambayo
huwafanya wapate hisia
fulani za mamlaka
katika nafsi zao.
Inasemwa kuwa hata askari
anapokuwa anavaa sare
za jeshi heshima yake huwa juu
zaidi.
SOMA;
Haya Ndiyo Mambo Mawili Usipokuwa Nayo Makini Yatakusumbua Na Kukutesa Sana Katika Maisha Yako.
Niliwahi kusikia
kisa cha Ofisa na dereva
wake waliokwenda kwenye
sherehe. Walipofika waliegesha
gari mbali na ukumbi.
Hivyo watu
hawakuwaona jinsi walivyokaa
kwenye gari. Kwenye
ukumbi kulikuwa na
msichana aliyeandaliwa kumvisha
mgeni shada la
maua.
Ofisa na
dereva walipofika mlangoni
yule msichana alikwenda
kumvisha shada la
maua dereva badala
ya Ofisa na
huku watu wakimshangilia dereva
alivishwa shada la
maua kutokana na jinsi
alivyoonekana. Alikuwa amependeza
na kuonekana na
hadhi kuliko bosi
wake.
Kwa hakika
siyo sahihi kumthamini
mtu kwa mavazi
na muonekano wake
pekee kwa sababu
kuna mambo mengine
muhimu kama vile
akili, ujuzi na
tabia.
Lakini pia
tukumbuke kuwa siku zote
watu hutupangia thamani
kutokana na jinsi
tunavyoonekana kwao hasa
wanapotuona mara ya
kwanza. Mwonekano ndicho
kitu cha kwanza
ambacho hudumu zaidi
katika fikra za
mtu anayetuona mara ya kwanza.
Aidha
hata hivyo muonekano huo
huweza kuwa na taswira hata katika
sifa zetu nyingine
ambazo mtu huweza
kuzigundua baada ya kutuona kwa mara
ya kwanza. Mara ngapi tumewahi
kuwasikia watu wakisema
“Mtu kama yule
hawezi kutenda jambo
la kijinga kama
hili” kipimo wanachokitumia hapa
huwa siyo kingine
isipokuwa anavyoonekana.
Je, umewahi
kuchunguza ni watu
wa aina gani
ambao huonekana wanaheshimika sana
kwenye mkusanyiko wa
watu kama vile
kwenye kituo cha
basi sokoni au
mkutanoni. Utagundua kuwa
wanaoheshimika zaidi ni
wake walio nadhifu.
Kwa kawaida
watu huamini kuwa
mtu aliye nadhifu
ni mtu wa
maana, aliye mwenye
akili, msomi, anaye
aminika na aliyefanikiwa
katika maisha. Mtu asiye
nadhifu anayeonekana mchafu
watu humchukulia kama
mtu asiye na
maana, siyo mwerevu,
siyo makini na
hajaendelea kimaisha.
Lakini mtu
mwingine anaweza kukata
tama kuwa hawezi
kuonekana nadhifu kwa
kuwa hana fedha
za kuweza kununulia
mavazi ya thamani.
Hata hivyo, ikumbukwe
kuwa ili mtu
aonekane nadhifu sio
lazima avae nguo
ghali. Unadhifu ni
kuvaa nguo safi
na kuutunza mwili
mzima katika hali
ya usafi.
Hakika ili
tuwe nadhifu tunahitaji
nguo nyingi zitakazotuwezesha kuwa
nadhifu kila siku.
Tukinunua nguo za
bei nafuu tunaweza
kupata nyingi na
kuonekana nadhifu siku
zote.
Hatuna budi
kukumbuka kuwa unadhifu
haushii tu katika
manufaa ya kuwavutia
watu wanaokutazama bali
hata kwako wewe
mwenyewe. Kadri unavyojishughulisha kujiweka
katika ya unadhafu
ndivyo kadri unavyojijengea hali
ya kujithamini wewe
mwenyewe.
Unapojithamini wewe
mwenyewe ndipo na
watu wengine wanapokuthamini. Kwa
hakika unapojifikiria kuwa
wewe ni duni
na mtu wa
hali ya chini
utaonekana vivyo hivyo
kwa watu na
utajipunguzia nafasi ya
kuthaminiwa.
Kulikuwa na
kijana mmoja ambaye
hakusoma shule lakini
hakupenda kabisa watu wajue
hakusoma. Hivyo alikuwa
akijiweka kalamu mbili
hadi tatu kwenye
mfuko wa shati
lake. Alipotembea katika
mkono mmoja alishika
gazeti na upande
mwingine alibeba mkoba
wa mkononi.
Siku moja
aliingia posta kumsalimu
rafiki yake anayefanya
kazi hapo. Alipoingia
tu alikutana na
mzee mmoja kutoka
mtaani kwao aliyemuomba
amjazie fomu.
Kijana aliona
huo ni mtihani
mkubwa ambao ungefichua
siri yake. Lakini
alifikiri haraka akaweza
kuvuka mtihani huo,
alimwambia mzee ana
haraka ana kisha
akachukuwa kalamu moja
katika mfuko wa
shati akampatia mzee
na kumuomba atafute mtu
amjazie fomu yake.
Kila ninapoikumbuka hadithi
hii huzidi kuamini
kuwa mtu anaweza
kujitengenezea yeye mwenyewe
hadhi anayoipenda na
kuwafanya watu wamthamini.
Hata hivyo, pamoja
na kuwa nadhifu
bado kuna mambo
mengine ambayo mtu
anapaswa kufanya ili
watu wakuthamini kikamilifu.
Watu wanakuthamini
kikamilifu iwapo utaishi
nao kwa maelewano
ushirikiano staha na adabu.
Huna budi kuwatendea
matendo mema uwe
mwaminifu na mvumilivu.
Uepuke maneno
ya karaha, jeuri
wala usiwe na
choyo, chuki na hasira pamoja
na yote ni
lazima wewe pia
uwathamini.
Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA
ABEID SAKARA (Dar es salaam)
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.