Jun 17, 2015
Ugumu Wa Maisha Isiwe Sababu Ya Kukufanya Wewe Ukashindwa Kufanikiwa.
Mara nyingi katika maisha
yetu tuliwahi kukutana au kukumbana na masaibu, vimbwanga, vioja na mambo
mengine mengi ya kukatisha tamaa ya kusonga mbele. Nina uhakika kama kuna
baadhi yetu tungepewa fursa ya kuandika mahali kuhusu masaibu yaliyotukuta,
basi tungejaza maelfu ya kurasa, kwa sababu ni dhahiri kuna mambo mengi
tuliyopitia.
Huenda pengine vingekuwa ni
vitabu vingi sana ambavyo vingeweza kuuzika sana. Baadhi wange vitumia kwa ajili
ya kujifunza mambo mengi na kuwasahihisha wengine ambao walikatishwa tamaa au
wamekatishwa tamaa au na mambo kama hayo.
Lakini kwa bahati mbaya au
nzuri kuna wengine hawajapata nafasi hiyo au na wengine imewadondokea na
wameipata kwa kutumia vyema nafasi hiyo. Kwa wale waliopata nafasi ya kuandika
vitabu ambavyo vimesomwa sana duniani na kuhamasisha watu wengine na hata kubadili maisha yao, wamekuwa na
mchango mkubwa sana na wanakumbukwa daima.
Mfano ni daktari na mtaalamu
wa nyurolojia wa Marekani, Ben Carson, ambaye alipitia maisha magumu sana kabla
ya kufikia mafanikio hayo. Kutokana na yale aliyokuwa amepitia hadi kufikia kuwa
mtu mwenye jina kubwa duniani, aliamua kuandika kitabu ili awahamasishe watu
wengine ambao wamepitia masaibu kama aliyoweza kupitia yeye.
Moja ya vitabu vyake
vinavyopendwa na vilivyopata kuuzwa sana hapa duniani kile cha “ Gifted Hands”
(Mikono iliyobarikiwa). Kitabu kilichoelezea maisha yake kwa ujumla mpaka
alipofika kwenye ngazi ya mafanikio aliyopo sasa. Mwanzoni Ben Carson alikuwa na maisha magumu shuleni.
Hali iliyosababisha kuwa wa mwisho darasani mara kadhaa.
Alikuwa akiitwa majina mbalimbali
kutokana na hali hiyo, hivyo ikasababisha kuwa mtu wa hasira sana karibu na
kila mtu. Akiwa amedhamiria kubadili maisha ya mtoto wake, mama yake alimnyima
kuangalia televisheni wala kutoka nje na kucheza na wenzake hadi pale
atakapokuwa amemaliza kazi zake za shule kila siku.
Muda huo aliweza kuutumia
kusoma vitabu viwili na kuandika taarifa juu ya kile lichokisoma. Baada ya muda
fulani wa kuishi maisha hayo tofauti alianza kuona mabadiliko hata shuleni
walimu na wanafunzi wenzake walianza kumshangaa.
Aliwahi kusema : “Ni wakati
ule ndipo nilipogundua kuwa sikuwa mpumbavu”. Huo ni ulikuwa mwanzo wa
kihistoria uliobadilsha maisha yake ambayo yalikuwa magumu kupita kiasi.
Huo ni mfano mmoja tu lakini
nafahamu kuwa wapo baadhi ya watu walioandika vitabu kama hivyo kwa ajili ya
kuhamasisha watu wengine kuwa imara katika mafanikio na kile wanachokifanya
katika maisha yao, ili baadae mbele kuwe kweupe.
Japokuwa siyo rahisi kwa
sababu wakati mwingine utafanya hivi, halafu utaambiwa siyo vile. Basi tu watu
wengine hulka yaoni kuona unapiga hatua moja mbele halafu unarudi hatua mbili
nyuma. Jambo la muhimu ni kutokukata tamaa na kuongeza juhududi zaidi na zaidi
kwa kile tunachokifanya. Kumbuka hakuna marefu yasiyo na ncha, hivyo huwezi
kubaki kwenye umaskini milele ikiwa utaamua, ni lazima UFANIKIWE hakuna wa kukuzuia.
Ansante kwa kutembelea
mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO, endelea kuwashirikisha wengine kujifunza
zaidi kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
- Makala hii imeandikwa na Suzan Mwillo wa Gazeti la Mwananchi.
- Mawasiliano suzanmwillo@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.