Jun 24, 2015
Nguzo Tatu Muhimu Za Mafanikio Ambazo Ni Lazima Uwe Nazo.
Umefika sasa wakati wa kila
mmoja wetu kutambua kuwa ana uwezo mkubwa wa kutumia vipaji vilivyo ndani mwake
kuweza kumletea mafanikio makubwa
maishani. Hii nikiwa na maana
kuwa inakulazimu kuweza kujua kuwa hiki kipindi tulichonacho sasa ni kipindi
cha maarifa ambayo kwa sehemu kubwa yanahusisha vipaji na ubunifu mkubwa zaidi
ili kuweza kufanikiwa.
Katika kipindi hiki mtu anayefanya
chochote kwa sababu yoyote hawezi kufika popote. Watakaoweza kumudu mashindano
ya dunia hii ya sasa, ambayo imefanywa kuwa ndogo zaidi, ni wale tu walio na
maaarifa maaalum na kwa sababu maalum na siyo tu maarifa. Ninasema hivi sio kwa
kukutisha na pia si maanishi uwe na elimu ya chuo kikuu ndiyo uwe na maarifa
haya, unaweza kuyapata hata kama hukwenda shule.
Kwa kulijua hilo kuwa tupo
kwenye dunia ya ushindani ambayo inatulazimisha kuwa na maarifa, vipaji na
ubunifu ni muhimu kwetu kujipanga ili kuhakikisha mambo hayo yote matatu tunayo
ili kuweza kujihakikishia kufanikiwa, kwani mambo hayo ni nguzo muhimu sana
kwetu sisi na kizazi kijacho ili kujenga taifa imara lililofanikiwa.
Pamoja na umuhimu wa
maarifa, ubunifu na vipaji katika suala zima la mafanikio yetu, lakini kwa
bahati mbaya wazazi wengi hapa nchini hawajui au hawajali sana kuhusu vipaji.
Hii hupelekea wazazi wengi kuweza kukandamiza vipaji vingi vya watoto wao bila
kujua kuwa wanaua vipaji hivi vya watoto.
Kuna wazazi ambao huwakataza
watoto wao wasiimbe kwa maelezo kwamba, kuimba ni ibilisi. Kuna wazazi wengine
huweza kuwavunja nguvu watoto wanacheza
mpira, kuchora na shughuli nyingine za kisanii kwa maelezo kwamba mambo hayo
huwapotezea muda wa masomo. Wasichokifahamu wazazi hao ni kwamba, huenda hivyo wanavyofanya watoto ndivyo vipaji vyao,
yaani ndiyo makusudi ya wao kuletwa hapa duniani.
Kwa watu wengi ikiwemo
wazazi kama ambavyo nawaongelea hapa wanapenda au wanataka watoto wao wawe ama
wafanye yale ambayo wao wazazi ndiyo wanayoyapenda bila kujali upendeleo na
uwezo wa watoto. Hali hiyo ndiyo ambayo inawafanya wasomi wengi wa nchi hii kwa
wasomi wa sifa na pato, badala ya kuwa wasomi wa ubunifu kwa faida ya jamii.
Kuna wasomi ambao hawakujua
tangu awali kwa nini wanasoma kile walichokisoma, kwa sababu hata uchaguzi wa
wasome kitu gani, ulifanywa na wazi wao, wakati mwingine, kwa kuwalazimisha.
Kuna vijana wengi wenye vipaji vikubwa ambao wameshindwa kuvitumia kabisa au kuvitumia
vizuri, kwa sababu vilikandamizwa utotoni.
Kama tulivyosema, umefika
muda sasa ambapo wazi wanapaswa kama siyo kulazimishwa na mazingira, kujua kwa
makusudi vipaji vya watoto wao ili waweze kuwasaidia kujenga kesho yenye
mkabala thabiti zaidi wa kimafanikio.
Mtoto anapoonesha kipaji fulani,
sisi wazazi tusikikandamize kwa sababu, hatukitaki. Anapoonyesha kipaji tumpe
moyo ili aweze kukiendeleza kwa faida
yake na ya kwa wengine. Kukandamiza vipaji vya watoto na kujaribu kuwaingizia
kile ambacho hakiko ndani mwao kwa hakika ni kuwaumiza bure tu.
Ifike
mahali na sisi tukubali kwamba, hata sisi huenda vipaji vyetu huenda vilikandamizwa au hatukuoneshwa
kwa namna nzuri ya kuvibaini na ndiyo maana pengine wengi wetu hatufurahii
shughuli tunazizifanya maishani mwetu. Kwa nini nasi tulee watoto ambao
watakuwa na utapiamulo wa ufahamu na matumizi ya vipaji.
Pia tutambue kuwa, tupo
kwenye kipindi cha zama za maarifa ni jukumu lako kutumia nguzo tatu hizo
muhimu kuweza kutufanikisha nikiwa na maana Maarifa, ubunifu na vipaji tulivyo navyo ili kufikia mafanikio
makubwa. Vitu hivi vikikaa pamoja na kufanyiwa kazi vinaleta matokeo makubwa na
ya kushangaza. Kwani hizo ndizo nguzo tatu muhimu za mafanikio kwako na kizazi
kijacho unazotakiwa kuzijua.
Tunakutakia kila la kheri,
endelea kujifunza kila siku bila kuchoka kwa kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO lakini hakikisha unawashirikisha wengine ili kuweza kujifunza zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI
NGWANGWALU,
0713
048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Nijambo lamsingi hasa ktk vizaz vijavyo%
ReplyDelete