Oct 26, 2015
Jinsi Unavyoweza Kufanya Jambo Ambalo Hujisikii Kulifanya.
Maisha
yanakuwa na maana na mazuri kwetu kama tunafanya yale mambo ambayo tunayapenda
na kuyatamani. Inapotokea unakuwa unafanya jambo ambalo hulipendi au hujisikii mara
nyingi mambo yanakuwa magumu sana. Ni kitu ambacho huwa kinatokea, unakuta tu,
hujisikii kufanya jambo fulani ambalo pengine ni muhimu kwako.
Je,
inapokutokea unataka kufanya kitu halafu ukawa hujisikii hapo unakuwa
unafanyaje? Je, unakuwa unaacha na kuendelea na mambo mengine au kuna hatua
unakuwa unachukua? Yapo mambo mengi unayoweza ukawa unajifikiria, lakini ukweli
wa mambo ni kwamba, zipo njia unazoweza kuzitumia kufanya jambo ambalo
hujisikii kulifanya.
Zifuatazo
Ni Njia Ambazo Unaweza Kuzitumia Kufanya Jambo Ambalo Hujisikii Kulifanya.
1. Anza kwa kidogo.
Kama
ni jambo ambalo hujisikii kulifanya anza nalo kwa kidogo. Kama wewe ni
mwandishi unataka kuandika kitu na unahisi hujisikii, anza na sentensi moja
kwanza, hiyo itakupa nguvu ya kuendelea zaidi. Na katika maeneo mengine ya
maisha yako unaweza ukatumia mbinu hiyohiyo, kwa kuanza na hatua ndogo katika
kila jambo.
ACHA KUKATA TAMAA, ANZA KUFANYA MARA MOJA. |
2. Usiruhusu akili yako kuogopa sana.
Kuna
wakati ni rahisi kujisikia huwezi kufanya jambo fulani kwa sababu ya woga ambao
unakuwa umeujenga kwenye akili yako. Mara nyingi akili inapokuwa na woga wa
aina fulani inakuwa siyo rahisi kufanya jambo lolote hata iweje. Ili kufanikiwa
katika hili, kwa vyovyote vile usiruhusu akili yako ikawa na woga wa
kupitiliza, kwa mfano woga wa kuweza pengine hutaweza kufanikiwa.
3. Jipe muda wa kujifunza.
Inawezekana
unashindwa jambo hilo kwa sababu hujalijua vizuri zaidi. Kama ni hivyo jipe
muda wa kujifunza na kulielewa jambo hilo kwa undani. Hii itakusaidia kuanza
kulifanya huku ukiwa na hamasa kubwa ambayo itakusaidia wewe binafsi kuweza
kulifanya jambo lako na kuweza kusonga mbele kimafanikio.
4. Acha kuahirisha.
Pamoja
na kuwa upo ugumu fulani wa kutokujisikia kulifanya jambo hilo, dawa pekee ya
kuweza kulifanya ni jifunze kutoweza kuliahirisha jambo hilo. Lianze hivyohivyo
hata kama ni kwa kidogo, hata kama huku ukiwa unahisi kama mwili hautaki, lakini kikubwa usiahirishe. Kwa kadri
utakavyozidi kufanya bila kuahirisha utajikuta unazidi kuongeza hamasa ya
kulifanya zaidi na zaidi.
Kwa
kifupi, hizo ndizo njia ambo unaweza ukazitumia kufanya lile jambo ambalo kwako
hujisikii kulifanya.
Tunakutakia
siku njema na mafanikio makubwa yawe kwako siku zote. Na kumbuka endelea
kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.