Oct 1, 2015
Kwa Nini Watu Wengi Hutapeliwa Kirahisi?
Kwa
kawaida kila jamii ina tabia za jumla kama ilivyo kwa mtu mmoja mmoja. Kila jamii
ina tabia na haiba zake, ambazo zinaitofautisha na jamii nyingine. Inaweza kuwa
maringo na kiburi, kuchapa kazi kwa bidii, ukarimu na nyingine za aina hiyo.
Watanzania
kwa mfano, wanasifiwa kwa ukarimu, ambapo pia kuna wakati ukarimu huo
umetafsiriwa kama ni ujinga. Hatuna uhakika, kipi ni kipi kati ya hivyo viwili.
Lakini sifa ambayo jamii ya Tanzania ni ya wazi kabisa ni ile ya kutokujiuliza
maswali linapokuja suala la fedha mbele yao.
Pamoja
na kipato kigumu kwa Watanzania wengi, lakini wakitajiwa kuwekeza na kuvuna
kirahisi, kila mtanzania anaweza kupata fedha na bila hata kujua alikozipata na
alivyozipata. Ni vigumu siku zote Mtanzania kupata mtaji, hata mdogo tu, na
ndicho kilio cha kila Mtanzania kila siku.
Lakini,
inapotokea nafasi ya kuwekeza mahali ambapo kuvuna ni kwa haraka na wingi sana
Mtanzania hupata mtaji wa kuwekeza hapo. Kama anakopa, ananyang’anya au
kudhulumu, hakuna ajuaye, lakini, mara nyingi, fedha anayoitaka ataipata na
atawekeza. Mfano ni upatu.
Unapotangazwa
upatu wa kuvuna haraka na kwa wingi, akili ya Mtanzania inashindwa kufanya kazi
na kuanza kuweweseka kwa kutafuta fedha za kucheza upatu huo. Huwa hajiulizi
inakuwaje fedha ije kirahisi kwa kiasi hicho, ilimradi wahusika wana ofisi na
wanatoa risiti kwa malipo yanayofanywa, kwao hiyo huhalalisha kila kitu.
Kwa
bahati mbaya sana, hata wasomi humizwa kwenye ulaghai huu ambao hupitia kwenye
mwavuli wa upatu au mikopo nafuu. Kuna vikundi vingi vya kukopeshana na kucheza
upatu, ambavyo hutangaza kwamba, vina vibali vya serikali na vimeandikishwa,
ambavyo vimekuwa vikiwaumiza sana watumishi wa serikali na hata sekta binafsi .
Naamini
umeshawahi kusikia mmbo kama haya ya kiendelea katika jamii zetu mara kwa mara.
Kitu ambacho huwa najiuliza sana, hawa wenzetu wanakuwa wana nini hasa hadi
kukubali kuingia katika mkenge wa kudanganyika kirahisi na kupoteza akiba zao
hata ndogo walizojiwekea.
Hebu
jaribu kuchunguza, utagundua kumekuwa na taarifa nyingi za kiutapeli kwa namna
na mtindo uleule, kiasi kwamba, kila kitu kiko wazi kwa kila mtu ni namna gani
hawa matapeli wanafanya kazi zao. Lakini, bado unakuta watu wanatapeliwa kila
siku, asubuhi na jioni. Ni kama vile, watu hawana kumbukumbu na kile
kinachotokea au ni kama vile wanaposikia kupata fedha kirahisi, ufahamu wao unafyatuka.
Umefika
muda ambapo tuna haja ya kujiuliza, ni kwa nini wengi wetu au Watanzania
wanatapeliwa kirahisi kiasi hicho? Bila shaka,
Tanzania ni nchi pekee ambapo mtu anaweza kuiba kwa hila kwa njia ileile hata
mara kumi, mahali palepale.
Bila
shaka, tatizo siyo umaskini, na kama ni umaskini, basi umaskini huo ni wa
kufikiri zaidi kuliko wa fedha. Kama ni umaskini wa kufikiri na siyo wa fedha,
inabidi watu au jamii ianze kujiuliza, ni kwa namna gani itafikia mahali pa
ukomavu? Na ukomavu huo itaupata tu kwa kujifunza kila siku kupitia vitabu na
hata semina ili kuondokana na kutapeliwa huko.
Ni
wakati wa kuchukua hatua sasa za kubadili maisha yako na kuachana na fikra za
kuamini yapo mafanikio rahisi zaidi. Kila mafanikio unayoyataka ni lazima
uyalipie. Hicho kitu ndicho unachotakiwa kwa uwazi kabisa ili kujenga mafanikio
makubwa.
Nakutakia kila la kheri katika harakati za kuboresha maisha yako
na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia
mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035 kwa ushauri na msaada wa haraka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.