Oct 9, 2015
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Kiongozi Bora Wa Maisha Yako.
Sifa
kubwa ya viongozi wengi walio duniani ni kutengeneza maisha ya mafanikio iwe
kwa jamii waliyomo ama maisha yao binafsi. Kiongozi yoyote yule ambaye hana
sifa za kuleta mafanikio huyo mara nyingi huwa hafai katika jamii husika. Kutokana na hilo
viongozi wengi iwe kwa bahati mbaya au kujifunza hujikuta wana sifa za aina
fulani ambazo zinawapatia mafanikio.
Lakini
unapokuja kuziangalia sifa hizo, si kwa viongozi tu ndiyo zinafanya kazi, hata kwako
pia unaweza kuzitumia kukupa mafanikio. Mpaka hapo hiyo yote inaonyesha suala
la kuujua uongozi ni la muhimu karibu kwa kila mtu ili kujijengea mafanikio
makubwa. Kitu cha kuuliza, ni kwa jinsi gani utakavyoweza kuwa kiongozi bora wa
maisha yako na kufikia mafanikio makubwa?
1. Jitoe kikamilifu kwa kile
unachokifanya.
Sifa
kubwa ya kiongozi ni kujitoa kikamilifu kwa kile anachokifanya. Haya ndiyo
maisha waliyonayo viongozi karibu wote duniani. Ni watu wa kujitoa sana
kufanikisha maisha ya wengine na yao pia. Sifa hii, ndiyo unayotakiwa kuwa nayo
ili kufanikiwa. Unatakiwa kujitoa kikamilifu na kwa nguvu zote mpaka malengo
yako yatimie.
2. Jitazame kama mshindi.
Hakuna
kiongozi ambaye huwa anaangalia mambo kwa kushindwa. Siku zote viongozi huwa ni
watu wa mtazamo chanya. Hiki pia ndicho kitu unatakiwa kukielewa vizuri, ili
kikujengee uwezo wa kuwa kiongozi bora wa maisha yako. Siku zote jitazame
mshindi kwa kila jambo unalolifanya. Hii ni mbinu nzuri sana ya kukufikisha
kwenye mafanikio makubwa.
3. Kuwa na ndoto kubwa.
Hakuna
kiongozi mkubwa wa maisha yako zaidi yako. Wewe ndiye kila kitu. Kwa kulitambua
hilo, ni muhimu kwako kujiwekea ndoto kubwa za kukufanikisha. Ndoto hizo kubwa
unazojiwekea ndizo zinazokufanya unakuwa kiongozi bora zaidi wa maisha yako.
Kumbuka, viongozi wote ni watu wa ndoto kubwa.
4. Jijengee uvumilivu wa kutosha.
Safari
ya maisha bila uvumilivu ni ngumu sana. Najua kwa kuwa unataka kuwa kiongozi wa
maisha yako ni lazima kwako kuwa mvumilivu kwa mambo mengi yanayojitokeza.
Kwenye maisha yapo mambo mengi ikiwa pamoja na kukatishwa tamaa na kurudishwa
nyuma. Haya yote utayashinda ikiwa utakuwa mvumilivu hadi mwisho.
5. Jijengee tabia ya kujihamasisha.
Inapotokea
mambo yako yanakuwa magumu, jiwekee utaratibu wa kujihamasisha. Unaweza ukajihamasisha
kupitia vitabu au semina mbalimbali. Lakini hiyo isiishie kwako tu, pia
wahamasishe na wengine na kuwasaidia kutimiza malengo yao. Kujihamasisha ni
njia pekee itakayokufanya usonge mbele hata pale unapohisi kukata tamaa.
6. Kuwa mtu wa kusikiliza.
Ili
uweze kujijengea tabia vizuri ya kuwa kiongozi sahihi wa maisha yako, kuwa
msikivu. Acha kuwa mwongeaji sana na kusahau kabisa kuwasilikiliza wengine.
Viongozi wote wenye mafanikio makubwa ni watu kusikiliza. Watu wa vitendo na
siyo waongeaji sana. Hivyo unachotakiwa kufanya ujue umuhimu wa kusikiliza
wengine, hiyo itakusaidia sana.
7. Kuwa na mitazamo chanya.
Mafanikio
makubwa ya viongozi wote, mara nyingi yanategemea mitazamo yao. Wengi wao ni
watu wa mitazamo chanya sana na mitazamo hiyo huwasaidia kufanikisha mipango na
malengo waliyojiwekea. Kwa hiyo unapoamua kuwa kiongozi wa maisha yako, tambua
suala la kujijengea mitazamo chanya halikwepeki. Hiyo ndiyo nguzo bora na
muhimu itakayokufanya kuwa kiongozi bora wa maisha yako siku zote.
8. Jifunze ubunifu.
Kwa
chochote kile unachokifanya, tambua ubunifu ni lazima unahitajika. Siri kubwa
ya kufikia mafanikio ni kuwa mbunifu kwa kile unachokifanya. Acha kufanya kwa
njia ileile itakukwamisha sana. Ukichunguza kwa makini utatambua viongozi bora walio
wengi ni wabunifu. Hivyo, jijengee ubunifu ili kuwa kiongozi bora wa maisha
yako na kufikia mafanikio makubwa.
9. Kuwa mtu wa misimamo.
Hautaweza
kumudu kuwa kiongozi wa maisha yako kama huna msimamo. Viongozi siku zote ni
watu wa misimamo. Siyo rahisi kuyumbishwa hovyo. Ni kitu ambacho unatakiwa
kujifunza na kujiwekea misimamo imara ambayo unaiamini. Misimamo hiyo unatakiwa
kuiweka katika maeneo mengi ikiwa ni pamoja na mafanikio unayotakiwa
kuyasimamia.
10. Jifunze mambo ya uongozi.
Siyo
lazima uwe mwanasiasa ili ujifunze suala zima la uongozi. Unaweza ukachukua
jukumu la kujifunza uongozi ili kukusaidia wewe binafsi katika maisha yako.
Ikumbukwe pia wengi wenye maisha makubwa ya mafanikio, ndani yao wana tabia za
uongozi. Kwa kujifunza mambo ya uongozi itakusaidia sana kutumia mambo hayo
kwenye maisha yako binafsi na kuwa kiongozi bora wa maisha yako.
Bila
shaka umetambua kwamba uongozi ni kitu cha msingi sana kwako na Kila mtu
anauwezo wa kuwa kiongozi kwenye maisha yake na kufikia mafanikio makubwa,
vinginevyo utaishia kuishi maisha ya hovyo yasiyo na mafanikio ikiwa utakuwa
unaishi bila kujiongoza.
Nakutakia
kila la kheri katika safari yako ya mafanikio na endelea kutembelea DIRA YAMAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia
mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035
kwa ushauri na msaada wa haraka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.