Oct 19, 2015
Mambo 6 Ambayo Watu Wasio Na Mafanikio Wanayafanya Kila Wakati.
Kitu
kikubwa kinachotofautisha watu wenye mafanikio na wale wasio na mafanikio ni
fikra, tabia na yale mambo ambayo wanayafanya kila siku. Watu wenye mafanikio
yapo mambo ambayo wanayafanya kila wakati na ambayo huwapelekea kufanikiwa
kwao. Na watu wasio na mafanikio yapo mambo pia ambayo wanayang’ang’ania
kuyafanya na yanapelekea kushindwa kwao.
Kwa
hiyo kama katika maisha yako hujafikia viwango fulani vya mafanikio
unayoyahitaji, tambua kabisa kuna mambo ambayo umekuwa ukiyang’ang’ania sana na
yamekufikisha hapo ulipo. Hivyo, kama unataka kufanikiwa na kutoka hapo ulipo
huna haja ya kujilaumu sana, ni kitendo cha kuamua na kuchukua hatua ya
kuachana na mambo yanakurudisha nyuma.
Kwa
haraka haraka naomba nikutajie mambo ambayo wasio na mafanikio wanayafanya kila wakati.
1. Kulalamika.
Watu
wasio na mafanikio mara nyingi ni watu wa kulalamika sana. Utakuta
wanalalamikia hiki mara kile na mwisho hujikuta wakishindwa kuchukua hatua na
kubaki kama walivyo. Hili jambo ambalo hulifanya karibu kila siku kwa
kulalamikia hata mambo madogo ambayo wanauwezo wa kuyabadili. Na kwa
kulalamikia huko sana, hujikuta wakishindwa kufanikiwa.
ACHA KUWAZA HASI KILA WAKATI
2. Kuwaza hasi.
|
Fikra
na mitazamo ya watu wasio na mafanikio mara nyingi zipo hasi sana. Karibia kila
kitu wanakiona kwa mtazamo hasi. Hata suala la mafanikio kwao wanakuwa wanaona
ni suala la wengine sio lao. Kwa mitazamo hiyo huwafanya wazidi kuona kila kitu
hakiwezekani ikiwa pamoja na mafanikio yao. Kwa kuendelea kujenga fikra hasi,
hivyo ndivyo ambavyo hujikuta maisha yao wakiyabomoa bila kujijua.
3.
Kupoteza muda.
Kati
ya kitu ambacho hakina thamani sana kwa watu wasio na mafanikio ni muda.
Matumizi yao ya muda ni mabovu utafikiri wao wana saa 48 kwa siku. Na kutokana
na sababu hii ya kupoteza muda hovyo, maisha yao hubaki kuwa ya hovyo. Kwa
sababu hakuna wanachokuwa wanakizalisha katika muda mwafaka. Muda mwingi
wanakuwa wanapoteza katika mambo ya kipuuzi na yasiyo na maana.
4. Kupuuza.
Siku
zote watu wasio na mafanikio maisha yao ni ya kupuuza mambo mengi ambayo kama
wangeyafatilia yangewaletea mafanikio makubwa. Ni watu ambao wanapuuza kwa
kudharau sana biashara ndogo ingawa hawana. Hiyo haitoshi wanapoteza pesa kwa
matumizi yasiyo ya msingi kwa kuona si kitu. Utakuta haya ndiyo maisha yao kwa
sehemu kubwa wanaishi kwa kupuuza mambo madogomadogo ambayo baadae
yanawarudisha nyuma kimafanikio.
5. Kujenga uadui.
Pia
hiki ni kitu ambacho watu wasio na mafanikio wanacho. Mara nyingi ni watu wa
kujenga uadui na watu waliofanikiwa. Maisha yao yanakuwa yamejaa roho mbaya
ambazo hazitaki kuona wengine wakifanikiwa. Kwa ubinafsi huo wanaoutengeneza
mara kwa mara, huwafanya washindwe kujifunza kutoka kwa watu walio na
mafanikio. Na matokeo yake hujikuta maisha yao yakizidi kuwa magumu.
6. Kuficha ukweli wa mambo.
Siyo
rahisi kwa watu wasio na mafanikio kuweka wazi ukweli wa maisha yao, hata inapotokea
pale wanapohitaji msaada wa kweli. Hawa ni watu ambao ni wasiri sana na
hujifanya wana mafanikio kumbe hawana. Na Hili ndilo kosa kubwa wanalolifanya
ambalo linawatesa na kuwafanya wakose msaada wa kile wanachokitaka katika
maisha yao ya kila siku.
Kwa
vyovyote vile, maisha uliyonayo sasa, yanatupa picha nzima ya kile
unachokifanya mara kwa mara. Ikiwa maisha yako ni ya mafanikio, endelea
kung’ang’ania mambo yaliyokupa hayo mafanikio. Lakini, ikiwa maisha yako ni ya
kushindwa inabidi ubadili mwelekeo haraka sana na kuacha kushikilia mambo
yanayokurudisha nyuma. Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo ambayo watu wasio na
mafanikio huyafanya sana katika maisha yao.
Tunakutakia
mafanikio mema, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Kumbuka TUPO PAMOJA.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.