Oct 7, 2015
Kila Mtu Ana Saa Mwilini Mwake.
Wanasayansi wamewapa
watu hawa majina ambayo yote
ni ya aina ya ndege. Kwanza ni
wale wanaochelewa kulala, ambao
wamewaita mabundi (owls) na wale wanaowahi kuamka, ambao
wamewaita kurumbiza (larks), ambayo ni aina ya ndege
pia.
Kuna watu
ambao, iwe wana kazi
au hawana , huwa wana kawaida ya kulala wakiwa
wamechelewa sana. Lakini, kuna
wale ambao hata kama kungekuwa na kitu gani, kuwahi kuamka ni
kama lazima kwao.
Ni kama
vile hawahitaji usingizi kwa muda
mrefu. Halafu, kundi kubwa ni lile la tulio wengi ambao tunalala kwa muda wa saa 7 hadi 8 kwa siku.
Ni watu
wanane kati ya kila kumi ambao wako kwenye kundi hili la
kulala kwa saa7 hadi 8
kwa siku. Kwa hiyo hawa wanaochelewa kulala au kuwahi kuamka , ni wawili tu kati ya
kila watu kumi. Hii ina maana kwamba, ni wachache katika jamii.
Wanasayansi wanasema, watu wanaochelewa
kulala, kama wale wanaowahi
kulala, wana tabia ambazo mtu anaweza kuzibaini, ambazo watu
wengine hawana. Kwa mfano, wale
watu wanaowahi kuamka, huwa
ni wenye kuchangamka sana wakati wa adhuhuri.
Ni watu
ambao kama ni kazi huzifanya vizuri sana
kwenye asubuhi ya saa nne hadi
saa tano. Ni watu ambao kwa kawaida wanakuwa
wazungumzaji sana, ni watu ambao
wanakuwa na tabia za kirafiki
au wanaweza kutengeneza urafiki kirahisi
na watu wengine.
Kwenye saa 3 hadi 4 usiku, wanakuwa kwenye hali nzuri kihisia na wanaingilika kirahisi katika muda kama huo.
Kwenye saa 3 hadi 4 usiku, wanakuwa kwenye hali nzuri kihisia na wanaingilika kirahisi katika muda kama huo.
Wale wanaochelewa kulala, huwa wanachangamka sana wakati wa adhuhuri. Kwa muda wa asubuhi, mara nyingi
jioni, hasa kwenye saa 12. Mtu
yeyote mwenye tabia ya kuchelewa kulala, huwa ni mchangamfu jioni zaidi
kuliko muda mwingine.
Kwa
nini kuna watu wanaochelewa kulala na wale wanaoamka asubuhi sana? Mtu anaweza
kuzungumzia uvivu au “ ushapu” na
kingine chochote ,lakini ukweli huenda
hauko hivyo. Kwenye mwili wa
binadamu, kuna aina ya saa ambayo
huratibu mwenendo wa binadamu katika
kila saa zake 24 za kutwa. Saa hiyo hufahamika kitaalamu kama circadian rhythms.
Saa
iliyoko kwenye mwili wa binadamu
huwa inaratibu mwenendo wa kulala
na kuamka kwa binadamu. Hufanya hivyo kwa kuratibu joto
la mwili na pia homoni kama zile za melatonin na cortisol.
Kwa
kawaida, homoni ya melatonin
huongezeka muda mfupi kabla ya mtu kwenda kitandani kulala, na hupungua muda
mfupi baada ya mtu kuamka. Homoni ya cartisol, ambayo hushughulika na sononi,
huwa juu muda mfupi kabla mtu hajapata fahamu akitokea usingizini.
Kwa
hiyo, mtu anakuwa mchelewa kulala au
muwahi kuamka, kutegemea tu kama homoni au mabadiliko haya yanafanyika
mapema zaidi au kwa kuchelewa sana ukilinganisha na jinsi
inavyotakiwa.
Saa
ya mwili wa binadamu ina tabia ya kufanya kazi
polepole au haraka kutegemea
umri. Ndiyo maana kwa wastani, wale wanaoamka mapema, wengi huwa ni wazee. Pia kwa sababu hiyo,
ndiyo maana wale wenye umri wa
sekondari na chuo, yaani wasiozidi
miaka 22, mara nyingi ndiyo
wanaochelewa kulala au ni “ mabundi” kama ambavyo wataalamu wanawaita na
hata wanafunzi wenyewe.
Kwa
kiasi fulani, tofauti hii ya umri katika kulala au kuamka, ni ya kibaolojia (homoni) na kijamii.
Mabadiliko ya kihomoni yanayojitokeza kwa kadri
mtu anavyokua, huondoa haja ya mtu huyo kulala saa nyingi, kama
zile anazohitaji mtu wa umri wa chini.
Lakini
imebainika kwamba, mwanga nao una athari
yake kwenye saa hii ya kuratibu ulalaji na uamkaji kwa binadamu.
Kwa
mfano, mtu anavyozidi kuwa mzee, ndivyo
ambavyo kudakwa kwa mwanga machoni mwake kunavyopungua. Hii huathiri
ufanyaji kazi wa saa hii.
Kijamii, nayo huhusu
shughuli au majukumu, kuliko kitu
kingine. Kwa mfano, watu wa umri wa kati na hata wanafunzi, huweza kukabiliana na utaratibu wa saa za
miili yao kwa kutengeneza ratiba zao za kulala
na kuamka.
Pamoja na ukweli
kwamba, utaratibu huwaumiza,
hudumu kulazimisha saa za miili yao kukulubaliana na utaratibu
wao mpya.
Wanafunzi wa sekondari
na vyuo vikuu kwa mfano, huwa “ mabundi” kwa sababu ya shinikizo la kazi. Siyo kwamba, saa
zao za mwili ndivyo zinavyofanya kazi,
hapana.
Till Roenneberg
wa Chuo Kikuu cha Munich, Ujerumani, aliwahi kufanya
utafiti wa kutosha, akiwahusisha
watu zaidi ya 25,000 wa umri kati ya miaka
8 na 90 na kupata matokeo muhimu
sana kuhusu usingizi na saa ya
mwili wa binadamu.
Kwa
mfano, aligundua kwamba, watoto huwa wanalala sana asubuhi, hadi wanafikia
umri wa miaka 20. Hapo katikati kunakuwa
na mabadiliko ya ghafla na ya mara kwa
mara, ambapo kuna wakati huwa
wanaamka mapema kwa muda fulani.
Mabadiliko
haya yanatazamwa na wataalamu kama Roenneberg, kuwa ni
mabadiliko ya kibaolojia ambayo yanatoa taarifa ya mabadiliko ya
kimwili. Watoto wa kike wamebainika kuwa katika umri wa kati ya miaka 13 hadi
19 wanachelewa zaidi kulala
ukilinganisha na wale wa kiume, ambao
kuchelewa kulala upande wao, huanza wakati
wakiwa na miaka 21. Tatizo hapa siyo kwa sababu watoto wa kike wana kazi nyingi usiku, hapana. Ni suala la saa ya mwilini.
Watoto wa kike
hupevuka haraka na hivyo, homoni husika
nazo hufanya mabadiliko mapema.
Kwa
ujumla, watoto wa umri wa miaka 13 hadi
20 ambao huchelewa kulala ,hawana tatizo, bali mara nyingi, saa za miili yao
ndivyo zinavyotaka.
Nchini
Marekani kwa mfano, kumekuwa na midahalo
yenye kuhusu kama muda wa kuanza masomo
usogezwa kidogo, ili kuwapa watoto muda
wa kulala zaidi au la.
Hii
inatokana na ukweli kwamba, hivi sasa watu wengi wameanza kukubali kwamba,
mwili wa binadamu una saa inayorataribu kulala
na kuamka, ambayo siyo vizuri
kuiingilia.
Kwa
kawaida, jamii nyingi hutazama kuchelewa
kuamka kama udhaifu na kuchelewa kulala kama sifa ya aina fulani. Kuna
wanaoamini kwamba, kuamka
mapema humfanya mtu kufanya
kazi kubwa zaidi kwa siku au humfanya mtu kuvuna
zaidi katika kipato. Inategemea
tu, lakini hakuna ushahidi
unaotilia nguvu jambo hilo.
Ushahidi
mpya wa hivi karibuni unaonesha kwamba,
kulala mapema au kuchelewa kuamka, ni
suala la chembe urithi (DNA), badala ya
utashi wa mtu. Kama mtu anafanya mazoezi
na kumudu kubadili mtindo wake wa
kulala, anaweza, lakini kama
amerithi kulala au kuamka mapema, hali
inaweza kuwa mbaya kwa upande wa mtu huyo.
Kumbuka
kwamba, watu wanaopenda
kulala usiku sana, iwe wana
shughuli au hawana, bali wanapenda tu,
huwa hawapatishwi tabu na hali hiyo ya kukosa usingizi, kama ambavyo wale
wanaolala saa mbaya wale
wanaolala saa mbaya kwa sababu
maalumu, huumizwa na hali hiyo. Hii ni
kwa sababu, jambo hilo liko ndani mwao.
Mtu ambaye yuko hivyo, kujaribu kumlazimisha, ni kupoteza muda na kumuumiza bure.
Carolyn
Schur, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya usingizi na mtunzi wa kitabu
chenye kuchambua sana kuhusu wanaolala usiku sana na wanaoamka mapema sana cha Birds
of a Different Feather, anasema, kuna watu ambao pia ni kama wagonjwa kuhusiana na usingizi.
Watu
hawa ambao wanaelezewa kitaalamu kwamba,
wana tatizo linalofahamika kama Delayed
Sleep Phase Syndrome au DSPS, huwa
hawawezi kulala chini ya saa 8
usiku na huchelewa kuamka asubuhi.
Hawa
huwezi kuwabadili na kuwafanya kulala
mapema kabla ya saa 8 usiku na
kuwalazimisha kuamka mapema. Kama
utadumu au wao
watadumu, kuna uwezekano wa kuingia
kwenye matatizo.
Kila mmoja
wetu ana saa zinazomtosha
katika kulala pia.
Wengine wakilala kwa saa tano. Wakati
wa usiku inawatosha, wengine saa 7 ndizo zinazowatosha na wengine saa 8 au zaidi.
Ni
kwa namna gani tunaweza kuheshimu na kupata saa zinazotutosha kwa usingizi ni jambo
muhimu sana.
Lakini
kujua kuwa tuna saa miilini mwetu ambazo hutupangia tuwe watu wa kulala kwa namna gani, ni jambo lingine
muhimu.
Kuna
wakati tunaweza kuwalalamikia wenzetu, yaani waume au wake
zetu kwamba, wanachelewa sana kuingia kitandani au kwamba wanawahi au kuchelea
sana kuamka. Kwa sehemu kubwa suala linaweza kuwa saa ya mwilini na siyo utashi
wa mtu.
Nakutakia kila la kheri katika harakati za kuboresha maisha yako
na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia
mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035
kwa ushauri na msaada wa haraka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.