Oct 5, 2015
Mambo 7 Ya Kujifunza Kutoka Kwa Bilionea Bill Gates.
Kwa
hakika unapozungumzia wajasiriamali wenye mafanikio makubwa kwenye dunia hii ya
sasa huwezi kukosa kumtaja Bill Gates. Kwa mujibu wa jarida la Forbes lililoko nchini marekani, ambalo
huzungumzia sana mafanikio ya watu linadai kwamba kwa sasa Bill Gates utajiri
wake unafikia dola za kimarekani bilioni 77. Na jarida hilo linamtaja kwa sasa
Bill Gates kuwa ndiye TAJIRI wa kwanza duniani.
Swali
kubwa ambalo mimi na wewe tunaweza tukaanza kujiuliza ni kwamba, kitu gani
ambacho kimemfanya Bill Gates kufikia mafanikio makubwa? Je, ni bahati au akili
nyingi alizonazo? Ni rahisi sana kuamini kuwa ana bahati au akili sana, lakini
ukweli wa mambo ni kwamba hakuna jibu sahihi kati ya yote hayo mawili iwe
bahati au akili nyingi zaidi. Kama yote hayo siyo sasa ni kitu gani
kinachosababisha Bill Gates kufanikiwa zaidi?
Haya Ndiyo Mambo 7 Ya Kujifunza
Kutoka Kwa Bilionea Na Mfalme Wa Software Duniani Bill Gates:-
1. Kuwa tayari kujitoa mhanga.
Katika
moja ya maandishi yake Bill Gates anadai kuwa, biashara wakati mwingine ni kama
mchezo wa bahati nasibu hivyo huwezi kujua kama utashinda au kushindwa. Hivyo
anasisitiza ni lazima kujitoa mhanga ili ufanikiwe. Anaendelea kusema kuwa kuna
wakati maisha yana vizuizi, kukatishwa tamaa lakini yote hayo utayashinda ikiwa
utaamua kujitoa mhanga, mpaka kufanikisha mipango na malengo yako.
Kitu gani cha kujifunza hapa?
Mafanikio
sio lelemama yanahitaji kujitoa mhanga na kulipia gharama za kupata mafanikio
hayo. Kinyume na hapo itakwa ni ngumu sana kufikia mafanikio.
2. Kuwa king’ang’anizi.
Wakati
Bill Gates akianzisha kampuni yake ya Microsoft ambayo kwa sasa imemweka kwenye
chati ya utajiri zaidi, kampuni hiyo mwanzoni ili suasua sana. Lakini kitu
kikubwa kilimchomfanya Bill Gates afanikiwe mpaka sasa ni kile kitendo cha
kung’ang’ania ndoto zake mpaka zikafanikiwa. Alijituma zaidi na kufanya kazi
kwa bidii usiku na mchana mpaka akatimiza ndoto zake.
Nini Cha kujifunza hapa?
Hakuna
njia ya mkato kufikia mafanikio na inachukua muda kujenga mafanikio makubwa
hivyo ni lazima kuwa king’ang’anizi kama nia yako ni kufikia mafanikio makubwa.
3. Jifunze kutokana na makosa.
Bill
Gates anadai ipo siri kubwa sana kujifunza pale unapokosea kuliko ukafanikiwa
moja kwa moja. Kwa sababu gani anasema hivyo? Kitu anachodai hapa ni kwamba
kwenye kukosea akili huwa inafanya kazi zaidi. Tofauti
na kufanikiwa unakuwa unasifiwa tu na usipokuwa makini unashindwa kujifunza
mambo ya msingi.
Jambo la kujifunza.
Acha
kuchukia makosa yako unayoyafanya, kaa chini ujifunze ili kufikia kilele cha
mafanikio.
4. Kuwa na mitazamo chanya.
Kujijengea
mitazamo chanya ni kitu cha muhimu katika maisha yako. Hili pia ni jambo ambalo
Bill Gates amelisisitizia ili kujenga mafanikio ya kudumu. Ni lazima kujua kuwa
utafanikiwa hata kama unaona njia ya mafanikio ni finyu kwako. Unapokosa
mtazamo chanya inakuwa ni rahisi kuweza kushindwa hata kwa yale mambo madogo
madogo.
Jambo la kujifunza hapa.
Siri
kubwa ya mafanikio ipo kwenye kuyachukulia mambo yako chanya na siyo hasi. Kwa
kufanya hivyo utafikia mafanikio makubwa sana.
5. Acha kujilinganisha na mtu
mwingine.
Pia
Bill Gates anasema kila mtu amezaliwa akiwa tofauti na mwingine na hawezi
kufanana na mtu yoyote duniani. Kwa hiyo kama wewe ni mtu wa kujilinganisha na
wengine sana na unataka kufanana na hao watu basi utakuwa unapotea. Kitu
kikubwa unachotakiwa kufanya nikutafuta mafanikio yako mwenyewe na kuachana na
tabia ya kujilinganisha.
Jambo la kujifunza hapa.
Jiamini
mwenyewe na kubali yale yaliyomo ndani mwako utafikia mafanikio makubwa sana.
6. Kuwa mkarimu muda wote.
Kitu
kingine mbacho Bill Gates anatufundisha katika safari yetu ya kuelekea kwenye
mafanikio ni kujifunza kuwa wakarimu muda wote. Akiwa na maana maisha kama
maisha wakati mwingine hayatabiriki. Leo unaweza ukawa uko juu kesho ukawa
chini. Hivyo ni vyema ukaishi kwa kuchukuliana na wengine sawa, kuliko ambavyo
ungejifanya wewe ni wewe tu.
Jambo la kujifunza hapa.
Acha
kuonyesha kiburi au kujiona juu sana pale unapokuwa na mafanikio. Badala yake
chukua jukumu la kuwa mkarimu muda wote.
7. Furahia mafanikio yako na wengine.
Mjasiriamali
wa kweli mara nyingi anafurahia mafanikio yake na wengine. Mafanikio anayoyapata
yanabaki kuwa siyo yake pekee, bali hata jamii yake inafaidika kutokana kile
alichokifanikisha. Hayo sio maneno yangu bali ni maneno ya Bilionea huyu Bill
Gates. Kwa hiyo hapa tunaonyeshwa siri nyingine kubwa ya kufikia mafanikio makubwa.
Jambo la kujifunza hapa.
Ni
muhimu kuwapa wengine moyo na kuwashirikisha au kufurahia wote pamoja katika
mafanikio tunayoyapata. Kwa kufanikisha hili litatusaidia kuachana na ubinafsi.
Hayo
ni mambo machache ya kujifunza kutoka kwa billionea huyu. Chukua hatua ya
kutendea kazi huku ukielewa wazi ukiamua kufikia mafanikio unayoyataka unaweza.
Kitu kikubwa ni uamuzi wako.
Tunakutakia
mafanikio mema na kumbuka endelea kuitembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza kila
siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia
mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035
kwa ushauri na msaada wa haraka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.