Oct 20, 2015
Kama Unataka Kutimiza Ndoto Zako, Acha Kufanya Makosa Haya.
Kila mmoja ana ndoto zake katika maisha, kila mmoja ana njia
yake ambayo anaiamini inaweza kumsaidia katika kutimiza ndoto zake za maisha.
Ndoto ni kama malengo ambayo kila mmoja anakuwa amejiwekea katika safari yake
ya maisha. Mafanikio ni pale unapokuwa umeweza kutimiza ndoto zako. Kuna
ambao walishindwa kutimiza ndoto zao labda kutokana na kutoelewa mambo machache
ambayo walioweza kutimiza mipango yao waliweza kuyaelewa.
Je unaweza kuiweka ndoto yako kuwa hai? Kuweka ndoto hako hai na
kuiishi ni kuepuka kufanya makosa ambayo wengi waliokata tamaa walishindwa. Je
ni makosa gani ambayo wengine hushindwa na kupelekea ndoto zao kuzimika?
1.Wasiwasi.
Wapo ambao ndoto zao zimezimika kwani wamekuwa na wasiwasi sana.
Unaweza ukawa unajiuliza "Je nitafanikisha kweli?". Wasiwasi hauna
nguvu yoyote katika kupelekea mambo yaende sawa bali huaribu mambo kwenda sawa.
Wasiwasi hukatisha tamaa, na kupelekea mtu kuona kuwa hawezi kutimiza malengo
yake. Una wasiwasi wa nini? Unapoona una wasiwasi chekelea na uuambie wasiwasi
wako kuwa "Nitazidi kuwa imara".
Woga ni kitu ambacho kinatenganisha watu waliofanikiwa na
waliofeli kufanikiwa. Kumbuka maana ya kufanikiwa simaanishi pesa na umaarufu
bali hali ya kuweza kutimiza malengo yako uliyopanga ni mafanikio pia.
Hivyo badala ya kuruhusu wasiwasi ukutawale, endelea kuweka
msimamo na kushikilia malengo yako.
MIPANGO MIZURI YA MALENGO NI MUHIMU KUJIWEKEA. |
2. Usikubali
vikwazo vikutawale.
Kwa kifupi ni kuwa lazima utakutana na vikwazo, vikwazo ni jambo
la kawaida katika maisha, vikwazo vipo kwa lengo la kutuimarisha. Na kama
kungekuwa hamna vikwazo tusingeimarika kwani kujisahau kungeongezeka. Vikwazo
vinatakiwa uvitazame kama vile ni ngazi, vinakusaidia kupanda hali fulani na
tunapaswa kujifunza na kuwa imara zaidi katika hali za vikwazo.
Ukifuatilia watu walioweza kuishi katika ndoto zao kila mmoja
atakuambia ni lini alipopata kikwazo kikuu ambacho hatasahau, wengine
walikataliwa kuwa hawawezi, wengine walikosa hata uwezo wa kutimiza ndoto zao,
lakini wote hao ambao wamefanikiwa japokuwa walikutana na vikwazo hivyo,
watakuambia kuwa HAWAKUKATA TAMAA.
Hawakuruhusu vikwazo viwatawale na kuwarudisha nyuma. Walizidi
kuimarika na kusonga mbele na kuzidi kushikilia nia yao.
3. Kubaliana na hali
uliyonayo.
Hali uliyonayo hivi sasa inabadilika. Maisha hubadilika na
hayabaki sawa milele. Hali zinapita, utazidi kukutana na watu mbalimbali,
utazidi kujifunza vitu mbalimbali na maisha hayataacha kukundisha. Wapo ambao
wamekata tamaa kutokana na hali waliyonao hivi sasa haiwezi kuwafikisha pale
wanapodhamiria lakini wanasahau kuwa mambo hubadilika. Jambo dogo linaweza
kubadilisha maisha yako yote na hukutegemea. Maisha ni maajabu.
Kubali hali ya sasa na maisha yako ya wakati huu, shukuru kwa
uhai ulio nao, marafiki wanaokuelewa, na tafuta kitu cha kushukuru nacho badala
ya kujiumiza kwa mawazo na lawama.
Kubali wakati huu wa sasa, shukuru kwa kila jambo, huku ukifanya
juhudi kuhakikisha unaendeleza malengo yako. Hata kwa madogo shukuru.
4. Kushikilia
yaliyopita.
Kosa lingine ambalo wengi hukosea na mwishowe kushindwa kutimiza
malengo yao ni kushikilia wakati uliopita. Bado wanaishi kwa kuwaza makosa
waliyoyafanya, mazuri waliyopoteza n.k. Wakati uliopita ulishapita, wakati
uliopo ndio wakati ambao unakupa nafasi wewe kujirekebisha na kuishi vyema.
Wakati ujao nao unategemea wakati huu wa sasa kutabirika. Kama wakati huu wa
sasa unautumia vyema na kuweka malengo utasonga mbele.
Kumbuka hakuna kiasi cha majuto ya wakati uliopita kinachoweza
kubadili yaliyopita na hakuna kiasi cha wasiwasi kuhusu wakati ujao ambacho
kinaweza kuubadili wakati ujao bali wakati huu wa sasa ndio pekee kwetu sisi. Jifunze
kwa yaliyopita na zidi kusonga mbele.
5. Kusahau
kujitunza.
Wengine husahau hata kutunza miili yao, kula kwa afya, mazoezi,
na kuhakikisha wana afya ya mwili, akili na roho.
Huwezi kufurahia matimizo ya ndoto zako kama una afya mbaya, kama
umezungukwa na tatizo. Usikubali kupoteza uhai, kuharibu afya yako, au kufanya
ambacho kinaashiria huwezi kujitunza na kujithamini. Unapaswa kujijali na
kutambua kuwa nawe unastahidi kujijali badala ya kujali ndoto/malengo yako tu.
Wapo ambao wanaamini bila kusaidiwa hawawezi kutimiza ndoto
zako.
Labda nitoe mfano mzuri, unaweza siku moja ukakutana na mtu na
kutokana na kujitambua kwako ukaweza kuweka urafiki mzuri na mtu yule. Kumbe
mtu yule anafahamiana na fulani ambaye naye kuna kitu ulichokuwa unahitaji sana
kusaidiwa na anakuunganisha na mwishowe unajikuta umepata mtu wa kukusaidia
kutimiza ndoto zako.
Sio kwamba hali ya kusaidiwa haitokei bali hutokea, kumbuka Mungu hana mikono kwamba itashuka mikono mawinguni na kukupa unachotaka bali ulimwengu ukitaka kukupa kitu fulani au huduma fulani hutumia wanadamu wenzio kukufunza na kukusaidia. Badala ya kutegemea msaada bali endelea kuishi vyema, heshimu kila mmoja awe wa chini yako au wa juu yako. Ishi na watu vyema na ishi katika haki. Haimaanishi ukifanya hivi itakusaidia moja kwa moja bali itasaidia njia yako ya kutimiza ndoto zako kwa kukuweka katika amani na watu.
Sio kwamba hali ya kusaidiwa haitokei bali hutokea, kumbuka Mungu hana mikono kwamba itashuka mikono mawinguni na kukupa unachotaka bali ulimwengu ukitaka kukupa kitu fulani au huduma fulani hutumia wanadamu wenzio kukufunza na kukusaidia. Badala ya kutegemea msaada bali endelea kuishi vyema, heshimu kila mmoja awe wa chini yako au wa juu yako. Ishi na watu vyema na ishi katika haki. Haimaanishi ukifanya hivi itakusaidia moja kwa moja bali itasaidia njia yako ya kutimiza ndoto zako kwa kukuweka katika amani na watu.
Wengine husubiria mpaka wawe na pesa kutimiza malengo yao,
wakati wakiwa hawana uwezo wa kutimiza malengo yao wanaacha ndoto zao. Kiukweli
unaweza pia kila siku ukafanya jambo moja ambalo linahusiana na ndoto zako,
hata kama ni dogo lakini siku yako imepita vyema kwa kuiishi katika ndoto yako.
7. Kujisikia vibaya watu
wakikusema vibaya.
Fahamu kuwa watakuhukumu (watahukumu kwa mabaya au kwa mema),
kwani wanadamu wengine hupenda kuhukumu watu na kuwazungumzia watu, lakini
ukipoteza raha yako kuwaza watakuhukumu vipi utakuwa mtumwa. Sio vibaya
kusikiliza watu wanavyokuhukumu, lakini ni vibaya pale mtu anapokuhukumu vibaya
na wewe kumchukia, mpende na jifunze uimara kupitia yeye, kwani changamoto hiyo
ipo kwa ajili ya kukuweka imara na kuzidi kuongeza upendo kwa wanaokusema
vibaya.
Shukuru kwa kila jambo na jiamini.
8. Kushikilia mambo
hasi.
Ni vigumu kuwaza mambo chanya au hasi kwa pamoja, bali unaweza
kuwaza au kushikilia moja. Kumbuka mawazo na fikra zako huumba. Pale unapoona
unawaza mambo katika upande chanya basi badili mtazamo wako na jaribu kuwaza
katika upande wa hasi.
Wengi wanawaza kuwa "ni vigumu kufanya hivi",
"Ukifanya hivi utashindwa", "Wewe huwezi",
"Unajidanganya" n.k. Mawazo haya hayajengi bali huzidi kukupa hofu.
Unapowaza mambo chanya hupelekea mambo chanya kutokea na unapowaza mambo hasi
hupelekea hasi kutokea. Kila njia moja ina umuhimu na kila njia inakupeleka
katika upande tofauti.
Badala kuwaza mabaya na kushikilia imani duni weka msimamo wako
katika njia sahihi. Usikubali kuwaza mabaya wakati wote. Usikubali hofu,
wasiwasi, hukumu, maneno, mawazo mabaya yakutawale.
Unapoweka akili katika mawazo hasi unaipa nafasi ya kukuonyesha
njia.
9. Kujilinganisha na
wengine.
Kujilinganisha hupelekea "wivu" na "tamaa".
Usikubali kujilinganisha na watu wengine, usikubali kuweka tamaa ya kutamani
maisha au hali ya mwingine. Sheherekea mafanikio ya mwenzio lakini sio utamani
na kutaka kuwa kama yeye, bali jifunze kupitia kwake na wewe uwe kama wewe.
Kila mmoja ana safari yake ya maisha, ndio maana uhai ukajigawanya katika
personality mbalimbali.
Hata wewe ukijiangalia kuna anayetamani kuwa kama wewe, kuna
ambaye hajafika ulipofika wewe, kuwa wewe kama wewe huku ukifurahia mafanikio
ya wenzio na sio ushindani, wivu, tamaa n.k.
10. Kutaka Watu Wakukubali
Kwa Ndoto Zako.
Usifanye kitu ili watu wakuone mjanja au watu wakusifie bali
weka malengo yako kwa nia ya kujiendeleza wewe na kuendeleza wanaokuzunguka.
Ukitaka watu wakukubali ukitimiza ndoto zako utakuwa unaishi kama mfungwa.
Jikubali kwanza wewe na hakikisha unaishi katika ndoto yako wewe kama
wew
Fahamu unataka nini, weka nia kwa
unacholenga, na tumia ulichonacho na kila nafasi uliyonayo kufika unapopanga.
Makala hii imeandikwa na Apolinary Protas wa JITAMBUE
SASA . Unaweza kujifunza zaidi kuhusu maisha na mafanikio, kwa kutembelea
blog yake www.jitambuesasa.blogspot.com. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana naye
kwa email jitambuesasa@gmail.com
|
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.