Oct 27, 2015
Usiruhusu Mambo Haya Matatu Yakakuzuia Kufanikiwa.
Yapo
mambo mengi ambayo mara nyingi yanakuwa yanamzuia binadamu kufikia mfanikio
yake. Mambo hayo yapo ambayo tunakuwa tunayajua na tunaweza kuyatawala, lakini
mengine tunakuwa hatuyajui, hivyo inakuwa ngumu kuyatawala. Hivyo kwa vyovyote
vile kila mtu hukutana na vizuizi fulani katika safari yake ya kufikia mafanikio.
Kwa
kuwepo kwa vizuizi hivi, hapa ndipo utofauti wa maisha huanza kujitokeza. Wapo
ambao huwa ni rahisi kushindwa kutokana na vizuizi. Wapo pia ambao huwa ni
ving’ang’anizi mpaka kufikia mafanikio yao. Wale ambao hushindwa , kuna wakati
hushindwa kwa vizuizi ambavyo naweza kusema wangeweza kuvishinda kama wangekuwa
makini kidogo.
Hapa
ndipo kipo kiini cha makala haya kilipo. Jaribu kukumbuka kidogo hivi, ni mara
ngapi umekuwa umekuwa ukizuiliwa na mambo madogo madogo kufanikiwa? Bila shaka
ni mara nyingi. Kuna wakati ulishindwa kutimiza ndoto zako kwa sababu pengine
ya visingizio tena visivyo na maana. Utakuta ni sababu ndogo ndogo ambazo umekuwa
ukijitengenezea.
Lakini
leo ninachotaka kukwambiani hiki, kama unataka kufanikiwa usiruhusu kabisa
mambo haya madogo matatu yakakuzuia kufanikiwa:-
1. Kukosolewa.
Acha
kushindwa kufikia mafanikio yako kwa sababu ya kugopa kukosolewa. Makosa unayoyafanya
yachukulie yawe fundisho kwako la kuweza kukusogeza mbele kufikia mafanikio
unayoyahitaji. Acha kusikiliza maneno ya watu wanaozidi kukukwambia kuwa eti
huwezi kufanikiwa tena. Hilo sio kweli kwani hakuna mtu anayejua uwezo wako
halisi.
Wapo
wengi ambao hushindwa kutimiza malengo yao kwa sababu ya kuogopa kukosolewa.
Kama kuna jambo unataka kulifanya wewe lifanye. Kama kuna mtu anayekukosoa mwache
aendelee kukosoa lakini safari yako izidi kusonga mbele. Hakikisha usizuiliwe
na kosa hili dogo na kukufanya ukashindwa kufikia mafanikio yako.
ONDOA HOFU ILI KUFIKIA MAFANIKIO YAKO |
2. Wasiwasi/woga.
Wengi
ni watu wa wasiwasi ama woga sana na hata wao kuna wakati wanashindwa kuelewa
wasiwasi huo hutokea wapi hasa. Utakuta ni watu wa wasiwasi kwa mambo madodogo
madogo na ya kawaida kabisa. Kwa mfano akitaka kufanya jambo hili au lile
anakuwa na wasiwasi mwingi sana nafsini mwake. Hili ni jambo ambalo kiukweli
huwakwamisha wengi kufanikiwa.
Sasa
kwa kuwa na wasiwasi huo ambao unakuwa unaujenga kila siku, inasababisha
mipango na malengo yako mengi kushindwa kutumia. Wasiwasi ni kitu ambacho
kinawafanya watu wengi kushindwa sana kutimiza malengo yao. Hiyo yote ni kwa sababu
unapokuwa una woga unasababisha kushindwa kujaribu mambo mengi ya
kukufanikisha.
3. Maumivu.
Inawezekana
unashindwa kuendeea mbele zaidi ya hapo ulipo kwa sababu ya maumivu uliyonayo
moyoni mwako. Maumivu hayo inawezekana uliumizwa baada ya jambo ulilokuwa
ukilifanya kushindwa kukuletea mafanikio makubwa au kukupa hasara ya kutosha.
Na ikafika mahali ukashindwa kujuani nini cha kufanya.
Haya
ni maumivu ambayo kwa namna moja nyingine tunakutana nayo katika maisha. Ni maumivu
ambayo hutufanya tushindwe kusonga mbele kila tukikumbuka makosa hayo. Kama upo
au ulishapitia hali hii, najua unaelewa ni kitu gani ninacho kiongea hapa. Ili
kufanikiwa, usiruhusu maumivu haya yakakufanya ukashindwa kufikia mafanikio
yako hata siku moja.
Kumbuka,
kwa kuwa na wasiwasi sana juu ya maisha yako, kuogopa kukosolewa na kushikilia
sana na maumivu ni mambo madogo ambayo yanaweza kukuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa. Acha kuruhusu
hali hii ijitokeze kwako. Kuwa shujaa wa maisha yako.
Dira
ya mafanikio inakutakia siku njema na mafanikio makubwa yawe kwako siku zote.
Na kumbuka endelea kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu;
0713 048 035,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.