Oct 2, 2015
Mambo Matano Ya Kuzingatia, Kama Wewe Ni Mjasiriamali Unayetaka Mafanikio Makubwa.
Mafanikio
ni kitu cha lazima sana katika safari ya mjasiriamali. Uwe mjasiriamali mdogo,
wa kati au mkubwa kwa vyovyote vile
unahitaji mafanikio. Lakini ili kufanikiwa na kufikia mafanikio hayo, yapo mambo ya msingi ambayo unatakiwa kuyazingatia.
Mambo hayo ni kama haya yafuatayo:-
1. Kujiwekea malengo.
Ukiwa
kama mjasiriamali unayetakiwa kufikia mafanikio makubwa, suala la kujiwekea
malengo ni lazima kwako. Unapokuwa na malengo yanakuwa yanakupa mwelekeo sahihi
wa kupata kile unachokitaka. Hiki ni kitu ambacho unahitaji kukizingatia sana
kwani ni nguzo kubwa ya kufikia mafanikio makubwa.
2. Kujitoa Mhanga(Take Risks)
Hakuna
mafanikio makubwa utakayoyapata bila kujitoa mhanga. Wajasirimali wote wakubwa
ni watu wa kujitoa mhanga sana. Wanakuwa wako tayari kutoa kitu chochote
ilimradi wafikie malengo yao. Kitu cha kuzingatia hata kwako wewe unalazimika
kujitoa mhanga na kulipia gharama ili kufikia mafanikio makubwa.
3. Kutokuogopa Kushindwa.
Wengi
wetu tumefundiswa sana kuwa kushindwa ni vibaya. Hali ambayo hupelekea tunakuwa
tunaogopa kujaribu karibu kila kitu kwa sababu ya hofu ya kushindwa. Ikiwa wewe
ni mjariamali unatakiwa kuwa jasiri na kujua kwamba mafanikio yanataka roho ya
ujasiri na kutokuogopa kushindwa. Hiyo ndiyo siri itakayokifikisha kwenye
kilele cha mafanikio na sio uoga unaouendekeza.
4. Acha kuridhika mapema.
Ni
kosa kubwa sana kujikuta unaridhika mapema eti tu kwa sababu ya faida
unayoitengeneza sasa. Ni vizri kujua, safari ya mafanikio bado ni ndefu kwako,
hivyo hutakiwi kuridhika kwa namna yoyote ile. Kama kuna jambo umelifanikisha,
endelea kwenye jambo lingine hadi kujenga mafanikio makubwa kabisa.
5. Tafuta ‘Mentor’
Acha
kujidanganyai kuingia kwenye safari ya mafanikio huku ukiwa peke yako. Ikitokea
umekwama kwa sababu huna mtu wa kukuelekeza au kukushauri, huo ndiyo unakuwa
mwisho wako. Hivyo ni muhimu kuwa na kiongozi wako ‘mentor’ ambaye atakuongoza kwenye kufikia mafanikio yako.
Kwa
kuyajua mambo hayo yatakusaidia wewe mjasiriamali kuweza kuendelea mbele zaidi
na kufanikiwa katika safari yako yamafanikio.
Nikiutakie
siku njema iwe ya mafanikio makubwa kwako. Kumbuka endelea kutembelea DIRA YAMAFANIKIO kujifunza na pia washirikishe wengine waweze kujifunza kupitia
mtandao huu.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.