Jun 1, 2016
Hii Ndiyo Misemo Inayotufanya Tusitimize Ndoto Zetu.
Baada ya
kufanya uchunguzi wangu wa kina nikaja kugundua ya kwamba kuna baadhi ya misemo
ambayo imekuwa ukiturudisha nyuma sana kwenye safari zetu za kuyasaka
mafanikio, hii ni kutokana na mara kadhaa ukijaribu kufanya baadhi ya vitu vya
msingi yanakujia maneno au misemo hiyo eidha uliwahi kuambiwa na jamii ya watu
wanaokuzunguka au wewe mwenyewe.
Maneno hayo ndiyo
yamenifanya nikumbuke mpaka hadithi ya sungura baada ya kukosa ndizi kwa muda
mrefu akajipa maneno ya kwamba "sizitaki mbichi hizi" nafikiri nitakuwa
nimekukumbusha mbali kidogo juu ya hadithi hii.
Ndivyo
hata sisi tumekuwa tukitumia maneno hayo, ndiyo ambayo yamekuwa yakijirudia
kila siku katika maisha yetu, najua utakuwa unashangaa ila huo sio muda wa
kushangaa bali ni muda wa kibatilisha maneno hayo, inawezekana nimekuacha
kidogo ngoja nikukumbushe misemo hiyo au maneno hayo ambayo kimsingi yamekuwa
yakikukwamisha kupata Mafanikio.
Ifuatayo ndiyo misemo ambayo inakukwamisha kupata
Mafanikio.
1. Haraka haraka haina baraka.
Mara
kadhaa umekuwa ukijaribu kufanya vitu vya msingi vyenye kukuletea manufaa ila
kwa kuwa kuna baadhi ya watu wanao kuzunguka wamekuwa wakiona kile
ambacho unachokifanya mwisho wa siku kwa kuwa kina changamoto nyingi
watakuambia maneno hayo kwamba haraka haraka haina baraka kwa kuwa wewe ndiyo
mfanyaji wa jambo hilo unaamua kupunguza juhudi za kiutendaji wa jambo hilo.
Na
ukichunguza kwa umakini wanaokwambia maneno hayo wao tayari wapo mahali
fulani kimafanikio. Kumbuka kuwa kauli hiyo inazungumzia muda na muda
haumsubiri mtu hata siku moja na moja ya uchunguzi ambao umewahi kufanywa juu
ya muda waligundua ya kwamba kila mtu anayo saa lakini hana muda. Huo ndio
ukweli watu kwenye simu zao wana saa lakini hawana muda wa kuleta mabadiliko
binafsi na jamii kwa ujumla.
Misemo mibovu ni hatari kwa mafanikio yako. |
2. Pole pole ndio mwendo.
Hayo ni maneno
ambayo umekuwa ukiishi nayo na kuamini kuwa kila kitu kitafanikiwa kwa hatua
uliyo nayo. Ukweli ni kwamba kwa kila jambo ambalo unalifanya hakikisha unafanya
kwa uhakika na ufanisi wa kutosha ili kupata matokea .
Mara nyingi tumekuwa
na maisha yaleyale kila siku kwa sababu unamini ya kwamba polepole ndio
mwendo, huenda ikawa ni kweli. Ila tatizo linakuja kufanya vitu pole pole
ambavyo havileti matokea chanya ya kimaisha, unajua kwa nini? kwa sababu
unafanya mambo yako kwa staili ya aina moja.
Kwa mfano kama ni biashara umekuwa ukisubiria
wateja tu na huna muda wa kuwafuata wateja harafu unasubiri hiyo pole pole iwe
mwendo utasubiri sana.Hata watu ambao wamefanikiwa na wao walikuwa wanaamini sana Kuwa pole pole ndio mwendo huku wakiongeza juhudi za kutaka kufanikiwa kwa kasi zaidi, na moja ya njia ambayo walizitumia ni kufanya kazi kama watumwa na leo hii wanaishi kama wafalme. Hivyo ni muda wako muafaka na wewe kubadili njia za kutafuta mafanikio hayo tofauti na njia ulizozizoea.
Pia ni lazima ujue ya kwamba maneno yamekuwa yana nguvu sana. Kwa mfano kuna baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kusema nipo nahangaika, ni kweli kama ni miongoni mwa watu ambao utahangaika sana. Badili tabia kauli zako kuanzia leo, utafanikiwa.
Nukuu ya Leo; chochote bila chochote huwezi kupata chochote.
Mwandishi ni afisa mipango; Benson Chonya
Simu; 0757-909942
Facebook; Benson Chonya
Barua pepe; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.