Jun 16, 2016
Hasara Za Kutokujua Unachokitaka Katika Maisha Yako.
Watu wengi ambao walifanikiwa walijua ni nini ambacho wanakitaka katika
katika Maisha, hata hivyo waliweza kupambana kadri wawezavyo, walitembea kwa
njia yenye miiba, mabonde, visiki, maeneo yenye misitu na wanyama wapoli na
wakali, lakini waliendelea na safari kwa kuwa walijua nini ambacho walikitaka.
Sasa inakuwaje wewe mwenzangu ambaye umekutana na maji machafu kwenye
safari yako ya mafanikio harafu unarudi sehemu ambayo haina maji kisha
unajifuta maji hayo machafu.
Bila
shaka nadhani utakuwa umenielewa vizuri maelezo niliyoeleza hapo juu, kama
hujanielewa nazungumzia changamoto ambazo watu wengi huwa wanakumbuna nazo.
Lakini katika changamoto hizo watu wengi ambao hatuna maisha mazuri huwa ni
watu wa kukata tamaa na kunung'unika bila kujua umuhimu juu ya maisha haya ya
kimafanikio.
Maisha
haya yana sura ya aina mbili, upande wa kwanza una watu ambao wana amani moyoni
na amani ya nje ya mwili ambayo huwapelekea watu hao kuwa na uhuru wa kifedha
pia, lakini katika aina nyingine ya sura ya maisha huwa na muonekano wa
watu wenye imani yenye muonekano wa nje tu, na watu hawa hawana muda ila hawana
uhuru wa kifedha.
Na katika kundi hilo ndilo lenye watu wengi zaidi. Unajua kwanini idadi
kubwa ya watu wenye maisha ya kawaida wanafikiri kawaida pia?
Jua kile unachokitaka, utafanikiwa. |
Tujifunze
kitu kupitia hadithi ifuatavyo:
Hapo zamani za kale kulikuwako na mtu mmoja ambaye maisha yake yalikuwa ni ya duni sana, kila kukicha kwake aliona ni afadhari ya jana, hali ya maskini huyo tunaweza kusema ya kwamba ilikuwa ni hali ya pangusa nikae. Alijitahidi kadri awezavyo kuweza kupambana na changamoto za kimaisha lakini hali ilizidi kuwa ni tete zaidi.
Siku moja alipata habari ya kwamba
katika eneo lake analoishi alikuwa amekuja mtalamu mmoja kutoka nchi za mbali
ambaye alijinadi kwa watu hao kwamba unatoa Pete ya bahati, Pete ya utajiri,
kurudisha mpenzi aliyepotea na mambo mazuri kama hayo kama wafanyavyo waganga
wengi wa jadi hapa nchini.
Hivyo maskini huyo alikwenda kumuona mtaalamu huyo, ili maskini aweze kupata utajiri ambao ilikuwa ni Kiu yake ya muda mrefu, kwani aliamini kauli ambazo alijianadi mtaalamu yule.
Baada ya kwenda kwa mtaalamu yule. Mtaalumu kutoka na hali ambayo alikuwa nayo maskini yule hivyo mtalamu hakuumiza kichwa kujua hitaji la maskini yule. Hivyo baada tu ya kumuona akaseme najua wewe unahitaji pete ya bahati na utajiri bila shaka? Maana naimbiwa na mizimu yangu ya kwamba umehangaika kwa muda mrefu sana bila kupata Mafanikio yeyote yale.
Maskini huku akiendelea kutafakari ya kwamba mtaalamu kajuajuje, mtalamu akaendelea kumueleza ya kwamba tatizo hilo litakwenda kuisha ndani ya siku kumi kutoka siku ile endapo atakwenda kutimiza masharti kwa ufasaha ambayo atampa.
Mtaalamu akamuuliza maskini yule "je unafikiri ya kwamba utaweza kuyatimiza masharti hayo? Maskini bila hata kujua ni masharti gani! Pia kwa kuwa yeye lengo lake lilikuwa ni kupata utajiri basi akajibu "ndio nipo tayari mkuu", mtalamu akamuuliza tena je una uhakika na unachokisema? Maskini akasita kidogo kisha akasema ndio.
Basi mtaalamu akamwambia ya kwamba najua ya kwamba wewe una familia,
hivyo nataka uweze kumtoa kafara mwanao wa kwanza. Maskini alishutuka sana
wakati mtalamu anasema maneno yale! Ila mtalamu akasema kwa kuwa mwanzoni
ulijibu ya kwamba upo tayari basi hakikisha ya kwamba unafanya hivyo.
Maskini alifikiri kwa umakini hakupata jibu kwa muda huo, ila kadri dakika zinavyozidi kwenda aliyatathimini maisha yake akaona haina jinsi ni bora afanye tu sharti japo alipenda sana mwanae huyo. Basi mtalamu pamoja na maskini yule waliamua kuyafanya mambo hayo ambayo waliyaamua na kuyaona ndio suluhisho la kuondokana na umasikini ule.
Mwisho wa siku mtoto kweli alifariki kwa kifo cha kukutanisha huku kila
mwanakijiji alibaki mdomo wazi kama mlango wa daladala ambayo inawasubiri
abiria.
Lakini baada ya siku hizo kumi kutimia baada ya kufanya kafara hiyo, maskini hakuona mabadiliko yeyote ambayo alihadiwa na mtalamu yule. Basi maskini akarudi kwa mara ya pili kwa mtaalumu. Maskini akamuliza mtaalamu mbona sioni mabadiliko yeyeto ya kuelekea safari ya utajiri. Mtaalaumu akawambia ya kwamba awe na subira kwani mambo mazuri siku zote hayahitaji haraka.
Kwa kuwa mganga yule alikuwa ni tapeli ambaye alitumia utapeli wake kuwalaghai watu aliamua kutoweka maeneo hayo na kutokomea mahali pasipo fahamika. Hivyo maskini yule mwisho wa siku akajikuta anakosa utajiri ambao aliuhitaji na kumuua mwanae ambaye alimpenda kwa dhati.
Tafsiri ya hadithi hii nini?
Kisa hicho kinatufundisha ya kwamba watu wengi ambao hali zetu ni duni, huwa ni watu ambao "HATUJUI TUNACHOKITAKA" hivyo kwa Kunatufanya kwa kuwa hali zetu ni za chini tunaona ya kwamba kila kitu tunachoambiwa ni sahihi kukifanya bila hata kupima madhara ya jambo hilo.
Katika sayari hii watu wengi wameibuka na kuwa waongo sana.
Wamekuwa wakifanya utapeli ambao una hasara kubwa ambazo zinawaghalimu watu maisha
yao yote. Hata hivyo vijana wengi ambao ndio tunaanza harakati za mafanikio, macho na maskio yetu tumevielekeza huko.
Kwa hiyo nikusii ya kwamba hakuna Mafanikio ambayo yanapatikana kwa staili hiyo, hata hivyo ni bora kujua mapema leo hii kwamba kesho yako itakuwaje. Moja ya changamoto ambaye inawakabili wengi ambao hatuna mafanikio hutumia mbinu hizo zisizo rasmi mwishowe hujikuta wanapoteza dira na mwelekeo wa kimaisha.
Mwisho nimalize kwa kusema athari za kutojua unachokitaka ni kwamba unakuwa na mipangio mingi kwa wakati mmoja na yote inakufa bila wewe kutimiza ndoto yako.
Mwandishi ni afisa mipango. Benson Chonya.
Barua
pepe; bensonchonya23@gmail.com
Simu: 0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.