Jun 3, 2016
Kama Utakwepa Kulipa Gharama Hizi, Huwezi Kufanikiwa.
Hakuna
kitu chochote ambacho unaweza ukakipata katika hii dunia pasipo kulipia gharama
zake. Kila kitu ni lazima ulipie gharama za aina fulani ili ukipate.
Asikudangaye mtu kwamba eti yapo mafanikio ya bure au ya kirahisi rahisi. Kila
mafanikio yana gharama zake ambazo unatakiwa kuzilipia kwanza ili kuyapata.
Kwa
wale wanaokwepa kulipia gharama za mafanikio, ni wazi huwa hawafanikiwi. Matokeo
yake hujikuta ni watu wa kulalamika na kulaumu kila hali. Ni gharama hizi ndizo
ambazo tunakwenda kuziongelea katika makala haya. Ikiwa akwepa kulipia gharama
hizi kwa namna moja au nyingine hakika, hutaweza kufanikiwa. Karibu sana na
twende pamoja kujifunza ili kujua gharama hizo.
1.
Kufanya kazi kwa bidii sana.
Kati
ya kitu ambacho hutakiwi kukwepa kama unataka kufanikiwa ni kufanya kazi kwa
bidii. Inatakiwa uweke nguvu zako zote kwa kile unachokifanya na si kufanya kwa
mkono mlegevu. Ikiwa utafanya kazi kwa bidii hakuna kitakachokuzuia tena
kufanikiwa.
Ili
kulielewa hili vizuri, jaribu kuwaangalia watu wenye mafanikio jinsi
wanavyofanya kazi. Tunaambiwa muda mwingine wanafanya kazi kwa muda hadi wa saa
kumi na mbili. Tambua kama unataka kufika viwango vya juu vya mafanikio kufanya
kazi kwa bidii ni gharama ambayo lazima uilipe.
Fany kazi kwa bidii zote, utafanikiwa. |
2.
Kutoa thamani.
Si
kufanya kazi kwa bidii tu, ndipo kutakapokufanya wewe ufanikiwe, hapana.
Unaweza ukafanya kazi kwa bidii sana lakini usifanikiwe ikiwa utafanya kazi
zako bila kutoa thamani inayotakiwa. Ni lazima ufanya kazi zako huku ukitia
thamani ya viwango vya juu, thamani unayotoa ndio inayokupa pesa.
Kwa
mfano unaweza ukawa muumbaji, lakini ikiwa nyimbo zako utakuwa unatoa bila kuwa
na thamani kubwa kwa wasikilizaji wako hazitasilikizwa na pia hutafanikiwa. Kwa
hiyo, ni lazima kwako ujitoe kufanya kila linalowezekana kuhakikisha unatoa thamani
kwenye nyimbo zako na hivyo ndivyo unakuwa umelipia gharama ya thamani.
3.
Kubali kukosolewa.
Mbali
na kufanya kazi kwa bidii na kutoa thamani, gharama nyingine ambayo unatakiwa
ulipie ili ufanikiwe ni kukubali kukosolewa. Wengi huwa hawako tayari kukubali
wanapokosolewa kwa wale wanayoyafanya. Huwa ni watu wakutaka kusifiwa sana.
Kwa
kuwa unataka mafanikio, ikitokea watu wakawa wanakukosoa acha kuumia sana. Tumia
kukosolewa huko kama kujirekebisha na kisha kuendelea kusonga mbele. Vinginevyo
ukishindwa kulipa gharama ya kukosolewa ni rahisi sana kuacha kile
unachokifanya kwa sabab ya hofu ya kukosolewa.
Kama
nilivyoanza kusema mwanzoni mwa makala haya, ili ufankiwe ni lazima ulipie
gharama, jiulize binafsi upo tayari kulipia gharama ili kufikia mafanikio yako.
lkiwa haupo tayari itakuwa ni vigumu sana kufanikiwa kwako.
Tafakari
juu ya hili na kisha chukua hatua za kubadili maisha yako kwa haraka sana.
DIRAYA MAFANIKIO inakutakia kila la kheri katika safari ya mafanikio. Na endelea
kujifunza bila kuchoka, ukifanya hili utababadili sana maisha yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.