Jun 7, 2016
Mambo Matatu (3) Yatakayofanya Kuboresha Kujiamini Kwako.
Kujiamini
ndiko kunakomfanya mtu aweze kufanikiwa zaidi. Watu wengi hawadumu katika mambo
wanayofanya hii yote inatokana na kufanya vitu kwa kutojiamini. Tupo baadhi
yetu tuna mawazo mazuri ila changamoto inakuja pale ambapo tunapotaka kuzitimiza.
Changamoto yenyewe inakuja kwa kuwa haujiamini unajiona ni bora umshirikishe
mtu mwingine, na kwa kuwa mtu huyo hana upeo wowote juu ya jambo hilo
atakwambia usifanye na kwa kuwa ni mtu wako Wa karibu unaacha kufanya jambo
hilo.
Mara kadhaa nimekuwa nikishika kalamu yangu kuandika ya kwamba moja ya changamoto kubwa ya watu waliofeli ni kwamba waliomba ushauri kwa watu ambao sio sahihi juu ya ushauri walioomba. Na kwa kitendo hicho kimefanya watu wengi kufa na Ndoto zao. Hivyo siku ya Leo ili kuokoa watu wengi wanaokufa na ndoto zao nimeona nilete makala hii uisomayo ili iweze kukupa nguvu na hamasa ya kuongeza kujiamini kwako.

Yafuatayo ndiyo
mambo muhimu ya kuzingatia ili kuongezea kujiamini kwako;
1) Tazama
ni mambo mangapi umeyatimiza.
Hii ndio
njia sahihi ya kuongeza kujiamini kwa jambo ambalo unalifanya. Kuna wakati
umekuwa umepanga mipango mingi lakini mingi ikekuwa haikamilika hii ni kutokana
haujiamini kwa mambo ambayo unayafanya. Kwa mfano mtu unaingia kwenye biashara
ila huna imani kama itakuwa au laaah!Ili
kujenga mahusiano kati yako na kujiamini ni vyema ukajua ni mambo mangapi ili
yapanga na leo yemetimia na mangapi hayajatimia. Ukiona mambo mengi ambayo
umeyapanga ukiona hayatimia ujue ya kwamba bado haujiamini kwa mambo yako. Ili
kujenga uiamara wa kujiamini hakikisha ya kwamba kila unalopanga linatimia kwa
wakati muafaka.
Tambua kilichomo ndani yako, kisha jiamini. |
2) Tambua kilichomo ndani yako.
Moja za gumzo ya kujua kilichomo ndani yako kinakufanya uweze kujiamini na kufanikiwa zaidi. Kuna baadhi ya watu hawajui vitu vilivyomo ndani yao. Unakuta mtu anafanya biashara lakini kumbe kilichomo ndani yake ni ualimu, hata hivyo kwa kuwa anafanya kitu ambacho hakipo nafsini mwake, mwisho wa siku unakuta biashara hiyo inakufa mapema hata kabla ya muda wake kufika.
Kama ndivyo hivyo basi ni wakati wako muafaka wa kuhakikisha ya kwamba unatenga muda wako siku ya leo ili uweze kujua ni nini kilichomo ndani yako. Huenda huko ndiko mafanikio yako yapo upande wako, kama kilichomo ndani yako ni kufanyabiashara! basi ifanye kwa uhakika wa kutosha ila kama unahisi wewe ni muigizaji kaa katika misingi.

Na moja ya umuhimu
wa kujua kilichomo ndani yako ni kwamba utakuwa mtaalamu kwenye kitu hicho.
Kufanya yote hayo kutakufanya uweze kujiamini kwani huko ndiko ugali wa watoto
wako ulipo.
3. Panga
malengo ya muda mfupi.
Ukitaka
kufanikiwa unachotakiwa kupanga ni kupanga mipango ya muda mfupi, hata yawe
malengo makubwa kiasi gani, kumbuka kufanya hivi kutafanya uweze kujua mbinu
mbalimbali za utekezaji wa malengo hayo. Moja ya kuweza kufanikiwa zaidi pindi
upangapo malengo ni lazima ujue muda maalum wa kutekeleza malengo hayo.
Mfano
kama unataka kununua gari nzuri andika lengo lako ni lini utanunua gari hiyo
hii itakutia hasira za kufanya kazi kwa bidii ili uweze kufanikisha lengo hilo.
Kufanya hivi Kutakujengea imani ya kujiamini ya kwamba unaweza kutimiza ndoto
yako kwa wakati mfupi.
Mwandishi;
Benson Chonya
Simu:
0757-909942Email bensonchonya23@gmail.com
Facebook; Benson Chonya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.