Jun 21, 2016
Malezi Mabaya Ya Familia Ni Adui Wa Mafanikio.
Miongoni mwa sababu
kubwa iliyonifanya leo kuchukua kalamu kuweza kumwaga wino wangu juu ya
karatasi ni kwamba uvumilivu umenishinda ndani ya moyo wangu. Mambo yamenifika
shingoni ni lazima niyaseme leo kabla umri wangu hajaelekea jioni (uzeeni).
Hata nikiangalia saa nayo bado mishale inazunguka pia hata siku nazo hazijawahi
kumsaliti lady jay dee kwamba siku
zinaganda.
Siku chache
zilizopita tuliadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kama ambavyo huadhimishwa
kila mwaka kitu hiki ni kizuri ambacho kinafaa kiendelezwe katika jamii
tunazoishi kwenu kufanya hivi ni kudumisha amani na upendo kwa watoto wetu.
Tuachane na hayo kwani hayo yamekwishapita na
wala haina haja tena kuzungumzia masuala ya maadhimisho hayo. Ila leo
nimeona ni vyema tuzungumzie kwa uchache juu ya MADILI BORA YA FAMILIA.
Jamii ya leo imekosa elimu tosha juu ya malezi bora kwa familia.
Hebu jaribu
kuzunguka mtaa wa kwanza utagundua kati ya watoto 9 kati ya 10 wanazungumza
lugha za matusi zaidi kama wanaimba nyimbo za injili au bongo fleva.
Ukitoka mtaa wa kwanza pita mtaa wa pili huko nako utastajabu ya Musa maana
huko watu wazima na akili zao wanacheza nyimbo za vigodoro, baikoko pamoja na
watoto wao.
Watu wazima hao
ukichungunza kwa umakini utagundua nguo ambazo wamezivaa ni fupi mithili ya
mabawa ya nzi, watu hao nguo ndefu na za heshima kwao huwa ni zenye upupu. Mmmh
tunakwenda wapi?
Tena toka mtaa pili
ingia mtaa wa tatu huko nako utashangaa kuokota dhahabu mchangani, watoto
wadogo wamekuwa ndio wanaigizwa kununua bia, madawa ya kulevya na mengineyo
mengi. Ukitoka mtaa huo jaribu kuingia mtaa mwisho huko nako kweli utaamini
dunia inaelekea ukiongoni maana kuna mambo ya ajabu sio kawaida ya nchi, kama
Tanzania huko utakutana na watoto ambao ni omba omba wengi ambao waliletwa
duniani na wazazi wenye akili timamu kabisa, wazazi hawa huwa napenda kuwaita
"sura ya mzee akili ya mtoto" maana hawafai hata kidogo.
Tunasema mara kadhaa kuwa kijana ni taifa la
kesho. Maneno hayo yatadhibitisha ukweli huo kwa malezi mtindo huo? Ya kuwalea
watoto malezi yasikuwa na heshima wala utukufu Mbele za Mungu. Kiukweli
najaribu kujiuliza kwa umakini bila hata kupata majibu sahihi tunaelekea wapi
kwa maisha ya aina hiyo?
Kimsingi ni kwamba
ugumu wa maisha haya tunayasababisha sisi wenyewe walezi wa familia zetu kwa
namna moja ama nyingine. Mara kadhaa tumekuwa tukiwatamkia maneno mabaya sana
watoto zetu hata hivyo kupelekea madili mabovu kwa jamaii hii. Mfano wa maneno
hayo wapo wale wanaowambia kuwa watoto wao ni wezi au vibaka.
Kila kukicha watoto wa mitaani wanaongezeka kwa idadi kubwa, ukichunguza kwa umakini juu ya hilo utagundua ya kwamba chanzo la ongezeko hilo ni mateso na mihangano mingi ya kifamilia ambayo kila baada ya sekunde inafanya ongozeko la watoto hao.
Kila kukicha watoto wa mitaani wanaongezeka kwa idadi kubwa, ukichunguza kwa umakini juu ya hilo utagundua ya kwamba chanzo la ongezeko hilo ni mateso na mihangano mingi ya kifamilia ambayo kila baada ya sekunde inafanya ongozeko la watoto hao.
Wapo pia baadhi ya
wazazi huwakatisha tamaa watoto wao kwa namna moja ama nyingi pindi wakiwa
wadogo na kusababisha maisha magumu kwa watoto na kuwapotezea dira ya maisha.
Watoto yatima wanaachwa katika mazingira magumu sana ambayo kila mwanajamii
hufumba macho pindi anapo watoto wa aina hiyo na kuona mtu huyo hausiki.
Tunaelekea wapi?
Ikiwa tunasema ya kuwa dalili ya mvua ni mawingu kwa methali hiyo tunaweza tukafananisha na kusema ya kwamba dalili ya umaskini wa nchi ni mateso, chuki na migogoro ya kifamilia inaandaa kizazi chenye maisha duni ambacho kinaamini katika misingi ya kuombaomba, wizi, utumiaji wa madawa ya kulevya na tabia nyingine ambazo hazipendezi machoni pa Mungu na kwa watu wenye heshima zao. Nauliza tena tunaandaa kizazi cha aina gani?
Ikiwa tunasema ya kuwa dalili ya mvua ni mawingu kwa methali hiyo tunaweza tukafananisha na kusema ya kwamba dalili ya umaskini wa nchi ni mateso, chuki na migogoro ya kifamilia inaandaa kizazi chenye maisha duni ambacho kinaamini katika misingi ya kuombaomba, wizi, utumiaji wa madawa ya kulevya na tabia nyingine ambazo hazipendezi machoni pa Mungu na kwa watu wenye heshima zao. Nauliza tena tunaandaa kizazi cha aina gani?
Hebu kabla sijaenda kuweka nukta tuangalie
malezi ya watoto katika baadhi ya familia nyingi. Katika kufanya utafiti
nimegundua ya kwamba malezi ndiye ambaye yanaandaa kwa kiasi kikubwa mafanikio
ya mtu kwa namna moja ama nyingine. Wazazi wengi hawana muda wa kukaa na
kuzungumza na watoto wao, ili kujua watoto wao wanahitaji nini katika maisha
yao, wazazi wengi wamekuwa wanafahamu ya kuwa mtoto ni lazima aende shule,
apete mahitaji mengine kama kula, malazi pamoja na chakula huku wamesahau watoto
wanahitaji zaidi ya hayo.
Hebu tujiulize ya
kwamba ni mara ngapi umekaa na watoto wako kuongea nao kuhusu mambo mbalimbali
yatakayomjenga kwa hapo baadae? Tujiulize tena hili tatizo na ongezeko la
watoto yatima chanzo chake ni nini? Halafu kwa nini kila huwa hatujali
juu ya jambo hili.
Wito wangu ni kwamba tuache kuchukulia vitu
katika taswira ya kawaida, najua suluhu juu ya jambo hili lipo payana kabisa,
tuache kupita na gari kwa mwendo wa kasi ili tuone mambo haya yanavyowadhuru
watoto wengi katika nchi yetu. Kuna usemi unasema mtoto wa mwenzio ni wako.
Ukweli juu ya kauli
hii upo wapi? Kauli hiyo ipo kwa baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima na
mazingira magumi ila katika taasisi na watu wengi kauli hiyo imekuwa haikuhusu.
Tafadhari najua ujumbe umefika mahali pake hivyo ni wakati muafaka wa kuchukua
hatua mahususi kuondokana na suala hili.
Ndimi, Afisa
mipango Benson chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.