Jun 15, 2016
Unajua Kwa Nini Pesa Ni Ngumu Kupatikana?
Binadamu ili apate kufahamu kitu
fulani lazima picha iliyoko kichwani ilingane na kufanana na kitu unachotafuta.
Endapo picha zikipishana lazima itakuwa vigumu sana kupata hicho unachotafuta.
Mara nyingi, tatizo hili la kupishana kwa picha linatokea zaidi kwa vitu vingi
ambavyo siyo...
halisi, kama vile PESA. Katika suala la pesa, watu wengi
wanapicha ambayo haiendani na uhalisia wa pesa yenyewe. Kwa maana nyingine ni
kwamba pesa, siyo kitu halisi tofauti na inavyochukuliwa na watu wengi.
Kitu ambacho siyo halisi, mara nyingi huwa hakioneani kwa urahisi mpaka utumie macho ya ubongo ndipo unaweza kukiona. Kwa maana nyingine ni kwamba pesa ni kitu ambacho akionekani kwa macho, na ni kitu ambacho SIYO HALISI.

Watu wengi wanadhania kuwa pesa ni
kitu halisi, ndiyo maana wakiona zile noti na silver wanadhani wameona
pesa…hapo kila mmoja utakuta anafukuzia ufukuzia noti lakini bila mafanikio
yoyote.
Inatosha kusema kuwa katika utafutaji wetu wa pesa tuko katika makundi makuu mawili ya watu. Kundi la kwanza ambalo ndilo la wengi ni lile linaloichukulia pesa kuwa ni kitu halisi na mara nyingi hawa wanatumia HISIA zaidi katika kufanya maamuzi mbalimbali juu ya utafutaji wake.

Itambue pesa kama kitu kisicho halisi. |
Kundi la pili ni lile la watu
wachache ambao wanaitambua pesa kama “kitu ambacho SIYO HALISI ~ ni WAZO” na
mara nyingi wanatumia ukweli katika kupanga na kuchagua njia za kuitafuta pesa.
Mara nyingi kundi ambalo linadhania kuwa PESA NI KITU HALISI, imekuwa vigumu sana kwao kupata pesa endelevu na wakati mwingine wameweza kuzikosa kila wanapoweka mtego. Kama usipochukua muda wako kutafakari juu ya pesa, ni rahisi sana kushawishika na kuona kile unachokiona kwa macho kama kitu halisi.
Hatari ya kuiona pesa kama KITU HALISI ni pale unapoifunga akiri yako isiweze kuona na kujua kile kinachosababisha pesa kuingia mfukoni. Kwakuwa akiri yako itakuwa tayari imejifunga basi mwisho wake ni kwamba hautajali kuboresha au kuendeleza kile ambacho kinakuwezesha wewe kupata pesa hiyo unayoifurahia sasa.
Kwa upande mwingine ni kwamba, ukiweza kuitafakari pesa katika uhalisia wake basi utaipata bila wasi wasi wowote, kwani kila mara utashikiria sana kile ambacho huivuta pesa kuja kwako.
Nitamjuaje mtu ambaye anaichukulia pesa kama kitu halisi? Ni wazi kuwa umewahi kuwasikia watu wengi wakisema kuwa pesa ni sabuni ya roho, pesa ni kila kitu, pesa ni bahati, siri ya kupata pesa aijulikani n.k. Hisia za namna hii juu ya pesa ndizo zinawafanya watu wengi kupenda kutumia njia za mkato ilimradi tu wamezipata.
Utumiaji wa njia za mkato katika kutafuta pesa umesababisha madhara mengi sana kwenye jamii zetu hizi hasa za kitanzania ambazo hazijawa na mifumo imara ya kijamii. Tumekuwa tukishuhudia wizi wa pesa, watu wanadhurumiana, watu wamejenga chuki na ndugu na jamaa na mengine mengi.
Madhara mengine ni ya kiuchumi kama kaya na taifa kwa ujumla…Watu wengi wanaodhania pesa ni kitu halisi siyo rahisi kwao kuamini katika kuzalisha vitu na huduma (thamani).
Wengi wanakuwa hapa katikati au
mwishoni mwa ule mnyororo mzima wa uzalishaji. Mwisho wake bidhaa na huduma zinakuwa
chache sana kiasi cha watu wengi kushindwa kuzipata kutokana na bei yake kuwa
kubwa.
Nchi ambayo ina watu wengi wa namna
hii, mara nyingi inategemea sana bidhaa kutoka nje ambazo tumeshuhudia kuwa ni
feki (bei rahisi) jambo ambalo limefanya thamani ya shilingi ya Tanzania
kushuka kila siku.
Watu wengi wakizidi kuamini kuwa pesa ni kitu halisi, ni wazi kwamba siku zote wataendelea kuamini kuwa pesa walizonazo ni kidogo na mwisho kujikuta wakijenga wivu na chuki dhidi ya wale wanaowadhania kuwa wanazo pesa nyingi.
Falsafa yangu katika hili ni kwamba “Ukidhania pesa ni kitu halisi, basi ujue kuwa hata njia na mbinu utakazotumia kutafuta zitakuwa zinafanana na zile za kutafuta vitu halisi”.
Kwa kawaida, upatikanaji wa vitu vyote ambavyo ni halisi huwa ni wa moja kwa moja; unatumia mchakato mfupi kuvipata. Ukitaka kitu fulani, ni kiasi cha wewe kunyanyuka na kufuata kilipo. Pia, vitu vyote ambavyo ni halisi, michakato yake ya kuvipata huwa ni rahisi sana na hauhitaji kufikiri sana.
Mfano: Ukitaka nyanya moja kwa moja ama utaenda shambani kwako au utaenda gengeni hayo yakifanyika unapata nyanya kwa dakika chache. Ukihisi njaa moja kwa moja unatafuta kitu halisi ambacho ni chakula – ama utakwenda nyumbani au hotelini, michakato hiyo ikifanyika tayari tatizo lako la njaa litakuwa limekwisha.
Kwahiyo, inaonekana faulo yetu ya kwanza katika kutafuta pesa ni pale tunapotumia mbinu ambazo ni maalum kwaajiri ya kutafutia vitu halisi.
Vitu ambavyo siyo halisi kama ilivyo pesa, navyo vina utaratibu wake na mbinu zake katika kuvitafuta. Pia ni vizuri kukumbuka kuwa, pesa yoyote unayoiona siyo halisi bali ni kitu kilichopewa thamani na binadamu, japokuwa pesa ni muhimu sana katika maisha lakini akili, afya na ufahamu wako ni muhimu kuliko PESA. Maana pesa ulipwa baada ya kuzalisha thamani (kutoa vitu na huduma).
Kwa maana nyingine ni kwamba, thamani yoyote ile uzalishwa au kuendelezwa na wewe binadamu. Wewe ndie unayetoa huduma au kuzalisha, wewe ndie unayechagua kazi gani ufanye ili upate pesa, hivyo wewe ni zaidi ya pesa na wewe ndie unayeamua upate pesa nyingi au kidogo. Lakini yote hayo yatategemea sana wewe kuacha kuiona pesa kama kitu halisi.
Kwahiyo, inahitajika wewe mwenyewe ufikirie kwa kina hadi ujiridhishe pasipo shaka lolote kuwa PESA SIYO KITU HALISI. Endapo utakuwa umekubali wewe binafsi tokea ndani mwako, basi tuungane katika kufahamu na kujifunza mbinu na njia mpya zinazotumika katika kutafuta na kupata vitu ambavyo siyo halisi kama PESA. Kwa kujielimisha kila siku, tutakuwa tumejenga uwezo wetu wa kutafuta na kupata pesa nyingi bila kuzikosa.

Imeandikwa na Cypridion Mushongi wa Blogu ya MAARIFA SHOP, unaweza
kujifunza zaidi kwa kutembelea blogu yake pia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.