Jun 27, 2016
Mambo Muhimu Ya Kukumbuka Kama Unataka Kuwa Mjasiriamali Mwenye Mafanikio.
Kila
kitu katika maisha ya binadamu kinaanza kama wazo. Haijalishi kitu hicho kimeleta
mafanikio au la, lakini mwanzo wake huwa unaanzia kwenye wazo analokuwa nalo
mtu.
Kumbuka
siku zote, mawazo yako ndiyo
yanayokufanya uwe na maamuzi ya aina fulani. Maamuzi hayo pia ndiyo yanakufanya
uwe na matendo ya aina fulani. Na matendo hayo ndiyo yanayotoa matokeo ya kile
ukifanyacho.
Kwa
hiyo, ikiwa unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio, kitu cha kwanza unachotakiwa
kuwa nacho ni mawazo sahihi. Unapokuwa na mawazo sahihi yatakusaidia kufanya
maamuzi na matendo sahihi.
Hivyo,
mafanikio utayaona kwa sababu maamuzi na matendo yako yatakuwa sawa kukusaidia
kufanikiwa. Kwa sababu hiyo, ni lazima kukumbuka mambo ya msingi kama unataka
kuwa mjasiramali mwenye mafanikio. Kwa vipi?
Yafuatayo
Ndiyo Mambo Muhimu Ya Kukumbuka Kama
Unataka Kuwa Mjasiriamali Mwenye Mafanikio.
1.
Jifunze kuwajibika.
Mjasiriamali
mwenye mafanikio ni yule ambaye anawajibika na kuweka mambo sawa kila wakati na
sio kusubiri hali fulani ndizo zimletee mafanikio. Mjasiriamali huyu anakuwa
tayari kukabiliana na kila changamoto na kutatua.
Hili
ni jambo muhimu sana la kukumbuka na kuweka kwenye akili ikiwa unataka kuwa
mjasirimali mwenye mafanikio. Wakati wote usisubiri matokeo ya aina fulani bali
pambana mpaka kieleweke.
Jifunze kuwajibika. |
2.
Jifunze kuwa mbunifu.
Ubunifu
ni njia pekee itakayokufanya uwe mjasiriamali wa mafanikio. Hakuna mafanikio
kwenye ujasiriamli kama wewe si mbunifu. Karibia kila kitu kinaweza kufa kwako
usipochukua hatua za kuwa mbunifu.
Jifunze
kufikiri tofauti na wajasiriamali wengine. Kwa mfano kila wakati unaweza ukawa
unajiuliza ufanye nini cha ziada ili uongeze idadi ya wateja kwenye biashara
yako? hapo ndipo unatakiwa kubuni mambo ya ziada ambayo wengine hawana.
3.
Jiamini.
Vipo
vikwazo vingi katika safari ya mafanikio. Lakini yote hayo yanapotokea ni
wakati wa kujifunza kujiamini wewe mwenyewe na kuamini ndoto zako kuwa unaweza
kuzifikia. Hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya hivyo zaidi yako. Ni lazima
ujue kujiamini kwako ndio msingi mkubwa wa mafanikio.
Wajasiriamali
wenye mafanikio wana hulka au tabia ya kujiamini sana. Hicho ndicho
kinachowasaidia waweze kufikia viwango vya juu vya mafanikio. Hata wewe kama
usipochukua jukumu la kuweza kujiamini hakuna utakachoweza kufanikisha sanasana
utazidi kushindwa.
4.
Usikate tamaa mapema.
Hakuna
kitu kibaya kama kukata tamaa mapema. Unapokuwa unakata tamaa unakuwa
unaitangazia dunia kwamba wewe huwezi tena. Na kimsingi hakuna faida hata moja
ambayo mtu anaweza kuipata eti kwa sababu ya kukata tamaa.
Wajasiriamali
wakubwa wenye mafanikio ni ving’ang’anizi wakubwa wa malengo na ndoto zao. Wanajua
bila kufanya hivyo hakuna kitakachofanikiwa. Siku zote mafanikio yanakutaka
usikate tamaa mapema la sivyo, utayasikia mafanikio kwa wengine.
5.
Jitoe mhanga.
Je,
wewe ni miongoni mwa watu wanaojitoa mhanga kuhakikisha ndoto zao zinatimia? Kama
jibu ni ndiyo basi wewe ni miongoni mwa wajasiriamali wenye mafanikio makubwa.
Sifa
kubwa ya wajasiriamali wenye mafanikio ni kujitoa. Mara nyingi huwa hawaangalii
hasara watakazozipata zaidi sana huangalia kile watakachokipata. Hili ni jambo
muhimu sana la kulielewa na kuliweka kwenye akili yako ikiwa wewe unataka kuwa
mjasiriamali wa mafanikio.
6.
Nenda hatua ya ziada.
Jifunze
kujiongeza na kuongeza vitu vya ziada ambavyo ni tofauti na wajasiriamali
wengine. Ikiwa huwezi kujitofautisha wewe na wajasiriamali wegine, basi moja
kwa moja upo kwenye hatari pengine ya kushindwa kwa baadae.
Hapa
unatakiwa kujitoa na kufanya kazi zako kwa uhakika na muda mrefu. Hiyo haitoshi
unatakiwa kujifunza kila wakati yale ambayo wenzio wanayafanya. Kwa kwenda
hatua za ziada ni silaha muhimu ya kukufanya ukawa mjasiriamali wa mafanikio.
Naamini
umejifunza kitu cha kukusidia kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio. Lakini usiishie
hapa endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kupata maarifa yatakayoboresha
maisha yako.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.