Jun 28, 2016
Tumia Njia Hizi Kujua Kipaji Chako.
Moja ya
changamoto kubwa inayowakabili watu wengi ni kutojua kwa undani kipi
kipaji chako ambacho Mungu amekupa na ambacho unaweza ukakitumia kwa namna moja
ama nyingine ili uweze kuleta mabadiliko chanya katika jamii na wewe binafsi.
Na kwa kuwa kuna
watu wengi ndio wapo kundi hilo, kuna usemi unasema ya kwamba wengi wape basi
ngoja nifanye hivyo kuweza kuwapa somo hilo la namna ya kujua kipaji
chako kwani hii itamsadia kila mmoja ambaye atakwenda kufuatana nami
mwanzo hadi mwisho katika mukutadha wa makala haya.
Tunapozungumzia
neno kipaji huenda kila mmoja akawa na maana yake ambayo anaifahamu, lakini kwa
namna moja ama nyingine ni lazima mtu aweze kuzaliwa nacho hivyo Mwenyezi Mungu
huhusika pia katika kumpa mtu kipaji.
Hivyo endapo mtu
atakifahamu kipaji chake inampasa sasa ajue namna ya kukiendeleza kipaji hicho
ili kisife. Pia ikumbukwe ya kwamba tunapozungumzia kipaji tunamzungumzia
binadamu na maisha yake kwa ujumla.
Katika
tafiti ambazo zimewahi fanywa na Dr.
Fred Luskin kutoka Stanford
university yeye aliweza kugundua ya kwamba asilimia 65 ya watu wengi
hawajui vipaji vyao na katika kundi kubwa la idadi hii ya watu ndio ambao wanafanya
vitu ambavyo sio vyao.
Na pia asilimia 35 iliyobaki hawa ndio ambao wameweza
kuvijua hivyo vipaji vyao ingawa haviwasadii katika maisha yao na wengine kwa
asilimia 100, hii ni kutoka mafanikio yatokanayo vipaji hivyo huwa ni ya muda
mrefu.
Hivyo kwa kuwa watu
wengi tunataka mafanikio ya muda mfupi uvumilivu hufika ukomo na kujikuta
tunaviacha vitu hivyo na kuingia kufanya vitu vingine.
Mfano mtu anakuwa na
kipaji cha kucheza mpira katika timu kubwa hapa nchini na nje ya nchi,na kwa
kuwa huenda amecheza kwa muda mrefu bila matarajio yake kutimia mtu huyo huacha
kile ambacho hukifanya na kuamua kufanya kitu kingine ambacho sio kipaji chake
mwishowe mtu huyo anajikuta anafanya hiki anakiacha mara kile nacho anakiacha.
Ukiona hicho
unachokiita kipaji chako hakitoi burudani, hakifundishi, hakishangazi basi
hicho sio kipaji.
Namna ya kugundua kipaji chako.
1. Kumuomba Mungu.
Hapa huwa
pananifanya nimkumbuke sana rafiki yangu Samweli Salali kwani aliwahi kuniambia
ya kwamba kipaji ni kusudio la Mungu kwa kila mja wake. Kwani katika mafundisho
yake katika vitabu vya dini vinasema kabla sijaumba nilikujua.
Hii inamaana kila
mwanadamu aliyeumbwa na Mungu ana kipaji chake, hivyo kinauwezo mkubwa wa
kubadili maisha yake na jamii kwa ujumla, ila kipaji hicho watu wengi hawahujui
mpaka dakika hii kuwa kipi kipaji chake ambacho Mungu kampa.
Hivyo kama wewe ni
miongoni mwa watu hao ni muda wako muafaka wa kutumia Muda huu kumuomba Mungu
akuonyeshe kipaji chako hasa na kipi kwa sasa?
Tumia kipaji chako kikusaidie kufanikiwa. |
2. Marafiki, ndugu na wazazi.
Hili ni kundi muhimu sana ambalo litakusaidia wewe kujua kipaji chako. Labda unaweza ukajiuliza ni kivipi? Tulia leo nipo kwa ajili yako. Watu ambao wanakuzunguka ndio wana picha kamaili juu ya maisha yako.
Hili ni kundi muhimu sana ambalo litakusaidia wewe kujua kipaji chako. Labda unaweza ukajiuliza ni kivipi? Tulia leo nipo kwa ajili yako. Watu ambao wanakuzunguka ndio wana picha kamaili juu ya maisha yako.
Kwa mfano mtu akiwa
mlevi hawezi kusema mimi ni mlevi ila watu ambao wanakuzunguka ndio ambao
watasema yule jamaa ni mlevi sana. Picha hiyohiyo ya kumuona mtu mwingine tabia
yake ndiyo ambayo inatumika kujua kipaji chako.
Hebu waulize nyie
mnanionaje, mna picha gani? Mnahisi nina kipaji Gani? Baada ya kuwauliza hayo
wao ndio watakupa picha kamili juu ya kipaji chako na maisha yako kwa ujumla.
3. Matatizo.
Matatizo
ni njia nzuri ya bora sana ya kugundua kipaji chako. Ulimwegu wa leo ni ulimwengu
wenye changamoto nyingi sana, hata hivyo kutokana na suala hilo, pale matatizo
yanapotokea na kuyapatia ufumbuzi sahihi hapo ndipo utakapojua kipaji chako.
Kwa mfano watu wengi
leo hii wanapenda maisha ya kufanyiwa kila kitu. Tuchukulie leo hii unamtegemea
mtu fulani ili aweze kukutimizia lengo lako. Halafu siku ya siku mtu huyo
anakufukuza nyumbani kwake na kukuambia nenda kajitegemee.
Baada ya kuambiwa
hivyo ndipo unakuja kugundua ni kipi kipaji chako baadala ya kuendelea
kuwa tegemezi. Hebu tuone mfano mwingine unakuta mtu alikuwa ni mfanyakazi wa
ofisini ila baada ya kustafu unajikita katika ufugaji mwisho wa siku unagundua
wewe ulikuwa una kipaji cha ufugaji badala ya kufanya kazi za maofisini.
Hivyo wito wangu
kwako ni vyema ukagundua kipaji chako mapema usisubiri changamoto fulani
zitokee ndipo ugundue kipaji chako.
4. Mashindano.
Kuna
baadhi ya nchi huandaa mashindano mbalimbali kwa ajili ya kusaka vipaji, hili
jambo jema sana hata hapa kwetu nchini kuna baadhi ya mashindano hufanyika ambayo
husaidia kujua vipaji vya watu kama vile bongo star search, fiesta, DJ
compition, umiseta na mangineyo mengi.
Hivyo kama kweli
unataka kujua kipaji chako endapo yatatokea mashindano yoyote yale jitahidi
sana kwenda kushiriki kwani hii itakusaidia kwa kiwango kikubwa kuweza kujua ni
kipi kipaji chako.
Mpaka
kufikia hapo niweke nukta kwa kusema kama ukwisha kugundua hicho kipaji chako
ni vyema ukajua ni namna gani ya kugeuza hicho kipaji chako kuwa pesa, kwani
hapo ndipo palipo kuwa na changamoto kubwa.
Ndimi
Afisa mipango Benson Chonya.
Simu( 0757909943)
bensonchonya23@gmail.com
Simu( 0757909943)
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.