Jun 8, 2016
Sifa Muhimu Unazotakiwa Kuwa Nazo Ili Kutimiza Malengo Yako.
Ili kuweza kufikia mafanikio makubwa, kati ya
kitu ambacho hutakiwi kukwepa ni kujiwekea malengo na kuyatimiza. Malengo ni
muhimu sana katika kufikia mafanikio yoyote yale. Hakuna mafanikio ambayo
unaweza kuyapata bila kujiwekea malengo. Haijalishi malengo uliyonayo ni
makubwa au madogo kiasi gani, lakini ni lazima kujiwekea ili kutimiza ndoto
zako.
Bila shaka utakubaliana nami, karibu kila mtu ana malengo yake. Kila mtu ukimuuliza juu ya malengo yake, atakwambia mwaka huu nataka kufanya hiki au kile. Lakini kitu cha kushangaza, pamoja na kwamba kila mtu ana malengo kwenye maisha ni watu wachache sana ambao huwa wanayatimiza malengo hayo. Wengi hujikuta wakiishia kupanga tu, lakini inakuwa ngumu kutimiza malengo yao.
Kitu cha kujiuliza watu hawa huwa wanakosea wapi hasa hadi kushindwa kutimiza malengo yao? Kiuhalisia, wengi huwa hawajui wanakosea wapi, na matokeo yake hujikuta wakizidi Kurudia makosa yale yale yanayowafanya wasitimize malengo yao huku wakiendelea kulaumu wengine au kujiona Kama wana mikosi. Kwa sababu ya lawama hizo kwa wengine au kujiona kama wana laana hivi, hupelekea wao kushindwa kupata jibu la nini kinachowakwamisha hasa hadi kushindwa kufikia malengo.
Soma; Aina Nne(4) Za Hofu Zinazokukwamisha Kufikia Malengo Yako.
Hata hivyo, kitu wasichokijua watu hawa, ili uweze kutimiza malengo yoyote ni lazima uwe na sifa za kukuwezesha kutimiza malengo hayo. Bila kuwa na sifa hizo, utasumbuka sana kufikia malengo yako. Naona unashangaa, ndio sijakosea ni lazima uwe na sifa kwanza za kutimiza malengo yako. Pengine unajiuliza Imani unaongea kitu gani? Sikiliza, twende pamoja sasa bega kwa bega, nikionyeshe sifa unazotakiwa kuwa nazo ili kutimiza malengo yako:-
Mosi, kuwa chanya. Siku zote naamini sana ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe chanya wakati wote. Hakuna mafanikio ambayo unaweza ukayapata kama upo hasi. Unapokuwa na mawazo hasi kama vile mimi siwezi katika hili, nimezaliwa familia maskini kwa hiyo siwezi kuwa tajiri au unaamini sana katika mikosi na laana, kamwe elewa kufanikiwa kwako itakuwa ngumu sana.
Mawazo hasi mara nyingi yanabomoa sana maisha
yako kuliko unavyofikiri. Ili uweze kufanikiwa hakuna namna nyingine ya kufanya
zaidi ya wewe kuwa na sifa ya kubeba mawazo chanya. Hakuna ambaye amefanikiwa
na huku akang'ang'ania kubebelea mawazo hasi. Watu wenye mafanikio mawazo yao
ni kuyawaza chanya kila wakati. Hii ni sifa muhimu sana unayotakiwa kuijua ili
kutimiza ndoto zako.
Hata hivyo, kitu wasichokijua watu hawa, ili uweze kutimiza malengo yoyote ni lazima uwe na sifa za kukuwezesha kutimiza malengo hayo. Bila kuwa na sifa hizo, utasumbuka sana kufikia malengo yako. Naona unashangaa, ndio sijakosea ni lazima uwe na sifa kwanza za kutimiza malengo yako. Pengine unajiuliza Imani unaongea kitu gani? Sikiliza, twende pamoja sasa bega kwa bega, nikionyeshe sifa unazotakiwa kuwa nazo ili kutimiza malengo yako:-
Mosi, kuwa chanya. Siku zote naamini sana ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe chanya wakati wote. Hakuna mafanikio ambayo unaweza ukayapata kama upo hasi. Unapokuwa na mawazo hasi kama vile mimi siwezi katika hili, nimezaliwa familia maskini kwa hiyo siwezi kuwa tajiri au unaamini sana katika mikosi na laana, kamwe elewa kufanikiwa kwako itakuwa ngumu sana.
Kuwa mvumilivu, hadi kukamilisha malengo yako. |
Pili, ili uweze kutimiza malengo yako sifa nyingine unayotakiwa kuwa nayo ni lazima uwe king'ang'anizi. Katika kipindi ambacho unakuwa unatekeleza ndoto zako, wapo watu ambao watakuja kukwambia hilo jambo unalolifanya haliwezi kufanikiwa. Ikiwa utawasikiliza watu hao, uwe na uhakika utaacha mipango yako mingi hewani.
Elewa unapokuwa kwenye kipindi cha kutekeleza ndoto zako, usikubali kuwa mwepesi wa kukata tamaa. Ukitazama historia ya watu wote duniani wenye mafanikio makubwa, huwa sio wepesi wa kukata tamaa mapema. Hawa ni ving'ang'anizi sana wanaohakikisha mpaka maisha yao yanabadilika.
Soma; Kitu Kinachokufanya Ushindwe Kutimiza Malengo Yako.
Tatu, sifa nyingine unayotakiwa kuwa nayo ili kutimiza malengo yako ni uvumilivu. Hakuna kitu ambacho unaweza ukakipata bila kuwa mvumilivu. Uvumilivu unahitajika sana ili kuweza kufanikiwa. Ukumbuke wakati tunatafuta mafanikio huwa tunakutana ya na mengi sana ikiwemo kukatishwa tamaa. Sasa kwa hali hii unaposhindwa kuwa mvumilivu huwezi kutimiza ndoto zako.
Hebu jaribu kuwaangalia watu wenye mafanikio makubwa. Kwa mfano kuna wakati hukutana na misuko suko mingi kama kupata hasara au kukosa masoko, lakini hayo yote huwa hawayatazami zaidi ya kuvumilia na kuangalia mbele. Hii ni sifa mojawapo muhimu unayotakiwa kuijua na kuifanyia kazi ili uweze kutimiza ndoto zako. Kinyume cha hapo usishangae ndoto zako nyingi zikabaki kama zilivyo bila kutimia.
Nne, ili uweze kutimiza malengo yako jifunze kukaa kimya. Kwa kawaida tunapokuwa tunatimiza mipango na malengo yetu, huwa zipo kelele nyingi sana. Wapo ambao watasema huwezi, wengine watakwambia hilo jambo kwa wengi huwa halina mafanikio. Inapotokea hivi kwako jifunze kukaa kimya. Ziba masikio kabisa.
Endapo itatokea ukaamua kusikiliza kila kitu, elewa itakupelekea kwako kuwa vigumu kufanikiwa. Umeumbwa kutekeleza mambo yako ukiwa wewe kama wewe na si kusikiliza sana wengine. Ikiwa kila ushauri utausikiliza hutaweza kufanikiwa. Najua unahitaji kutimiza malengo yako, kama hiyo iko hivyo, usisikilize kila kitu cha nje na kuwa na msimamo wako kwa kukaa kimya.
Mwisho, sifa nyingine unayotakiwa kuwa nayo ili kutimiza malengo yako ni lazima uwe tayari kukua. Kukua huku ninakozungumzia sio kukua kwa mwili, bali ni kukua kiakili. Ni lazima ifike mahali ukakubali kujifunza na kuelewa kwamba makosa katika safari ya mafanikio yapo na unaweza kujirekebisha.
Unaweza ukaamua kukua na kuwa mjasiriamali mkomavu kwa kuamua kujifunza kila siku. Kila siku jaribu kutenga muda angalau wa saa moja kujifunza mambo mbalimbali ya kimafanikio. Unaweza ukajifunza kupitia vitabu au mtandao kama huu kila siku. Hapo utakuwa umejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kifanikiwa.
Kwa kuhitimisha makala haya, naomba niseme hivi ukiona hujaweza kutimiza malengo yako kwa namna moja au nyingine, elewa kabisa kuna sifa muhimu ambazo unakosa hadi kupelekea kushindwa kutotimiza malengo hayo. Hakikisha unajua sifa hizo unazozikosa na kisha jirekebishe na songa mbele.
Ansante kwa kunifatilia na
pia washirikishe wengine waweze kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YAMAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA
MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.