Jun 2, 2016
Watu Hawa Badala Ya Kuzeeka Wanazidi Kuwa Wazuri.
Je,
imeshawahi kukutokea kwako ukatazama kwenye kioo na kubaini kwamba, umekuwa
mzuri zaidi ya ulivyokuwa jana? Kama hiyo imeshatokea, ujue kwamba, huko peke
yako. Kwa nini huko peke yako? ni kwa sababu, hata watafiti wamebaini kwamba, binadamu
hutokea akaoongezeka uzuri kwa kadri siku zinavyokwenda.
Haijafahamika
hata hivyo kwamba, ni hisia au mitazamo tu yenye kubadilika au ni kweli watu
huongezeka uzuri kwa kadri siku zinavyokwenda mbele. Hata hivyo kiwango cha
utafiti uliofanywa kinaonyesha kwamba, huenda kuna ukweli kwamba, kiwango cha
mtu kuvutia huongezeka kwa kadri siku zinavyoenda.
Hata
hivyo, wanawake wameonekana kuwa kwenye uwezekano wa kuhisi kuongezeka uzuri
kuliko wanaume, kwa kadri siku zinavyoenda. Imebainika kwamba, wasichana wanaomaliza
elimu ya sekondari na hata vyuo, wako kwenye umri ambao, ndiyo hasa mabadiliko
hayo yanaonekana au kujitokeza zaidi. Kuna wale ambao hubaini kwamba, katika
miezi kadhaa, wameongezeka uzuri na wengine kubaini kwamba, uzuri wao
umeongezeka tofauti na walivyolkuwa miaka mitano nyuma.
Imeelezwa
kwamba, wanawake huwa wanaona kwamba, siku zilizopita hawakuwa wazuri na wala
hawakuwa na miili mizuri kama waliyonayo hivi sasa na huamini pia kwamba,
watakuwa wazuri zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda.
Wanawake
wanaamini kwamba, kila siku kuna nafasi kwa upande wao kujibadili linapokuja
suala la uzuri, kwa hiyo wanakuwa na matumaini kwamba, watajiwezesha kuwa
wazuri kwa kadri siku zinavyosonga. Usishangae sana, shusha pumzi kasha utulie.
Kumbuka huu ni utafiti tu, ambao umefanywa na watafiti.
Tunakutakia
siku njema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.