Jun 20, 2016
Mambo 8 Ambayo Watu Wenye Mafanikio Hawapotezi Muda Kuyafanya.
Katika
harakati za kutafuta maisha si ajabu sana kukutana na watu walio kata tamaa au
watu wenye msongo wa mawazo inayotokana hasa na kuona ndoto na malengo yao
hayatimii. Ni jambo ambalo huwa linatokea sana miongonii mwetu na kufikia
mahali kuona maisha kama hayafai.
Lakini
kitu nilichokuja kugundua, kipo chanzo kikubwa kimoja tu ambacho hupelekea
kuona ndoto au malengo ya wengi kutokutumia na kusababisha msongo wa mawazo au
kukata tamaa. Chanzo hiki si kingine bali ni kupoteza muda kwa mambo madogo
madogo.
Ukiwa
kama mjasiriamali ni muhimu sana kujua thamani ya kila sekunde unayoitumia.
Sasa wengi hawalijui hili, wanapoteza muda hovyo na kujifanya wanatafuta
mafanikio. Wajasiriamali waliofanikiwa hawapotezi muda wao kwa mambo yasiyowasadia.
Ni
wakati umefika wa kujua kila thamani ya muda wako unaoutumia kuanzia dakika,
saa mpaka siku nzima. Usipoteze muda kufanya mambo yanayokurudisha nyuma. Anza
sasa kuishi kwa mafanikio, kwa kujifunza mambo ambayo wajasiriamali wenye
mafanikio hawapotezi muda kabisa kuyafanya:-
1.
Hawapotezi muda kwenye mitandao ya kijamii.
Kuingia
kwenye mitandao ya kijamii kama face book, twitter au instagram kuangalia
taarifa za hapa na pale ni moja ya sehemu ya maisha yetu ya sasa. Lakini ikiwa
utashindwa kutawala muda wako na kujikuta wewe ni mtu wa kuperuzi utapoteza
muda mwingi sana ambao ungekusaidia kwa mambo mengine.
Watu
wenye mafanikio wana nidhamu kubwa sana juu ya hili, na wakati wote huwa makini
na mitandao hii ili isiwapotezee muda. Kama wewe ni mlevi wa mitandao ya
kijamii, jiwekee muda wa kuingia huko na kuangalia mambo yako. Usiingie tu kwa
kuwa unao muda. Yapo mambo mengi ya kufanya na muda ikiwa pamoja na kujisomea.
2.
Hawapotezi muda kufikiria makosa yaliyopita.
Kila
mtu anafanya makosa kwenye maisha yake, halikadhalika hata watu wenye mafanikio
wanafanya makosa pia. Siri kubwa ya mafanikio ni pale unapokosea jifunze juu ya
makosa hayo na ya kusaidie kuweza songa mbele zaidi ya pale ulipokuwa.
Inapotokea
unafanya kosa, huhitaji kulia sana zaidi ya kujifunza na kuchukua hatua za
kukusaidia kufanikiwa. Hata watu wenye mafanikio katika maisha yao wanapokosea,
huwa hawapotezi muda kufikiria makosa yao na kikubwa wanachokifanya ni
kuhakikisha wanajifunza na kuendelea mbele.
3.
Hawapotezi muda kuanza siku yako bila kuipangilia.
Watu
wenye mfanikio wana mipango ya kuwaongoza kufanikiwa kila siku. Ni watu wa
kuandika mipango yao ya kesho siku moja kabla. Hivyo, wanapoianza siku wanakuwa
wanajua ni wapi wanapotakiwa kuanzia na wapi wanapotakiwa kuishia kwa siku
inayofuata.
Kimsingi,
hakuna kitu kizuri kama kuianza siku yako kwa kuipangilia kwanza kabla
hujaifikia. Ni utaratibu mzuri sana ambao haukupotezei muda na unakufanya uishi
kwa ushindi. Watu wenye mafanikio hawapotezi muda kuainza siku yao bila
kuipangilia, nawe pia unatakiwa kujifunza juu ya hilo.
4.
Hawapotezi muda kufikiria mambo yanayofanywa na wengine.
Watu
wenye mafanikio ni mara nyingi hawapotezi muda wao wa thamani kujilinganisha na
watu wengine. Kwa kifupi, ni watu ambao hawaangalii sana wengine wanafanya nini
ili nao wafanye. Ni watu ambao wana misimamo yao wenyewe na kuamini kile
wanachokifanya kwamba kitawasaidia kufanikiwa hata kama ni kidogo.
Hata
hivyo kumbuka si vibaya kuangalia au kushindana na yale ambayo wengine
wanayafanya. Mtu pekee ambaye unaweza kushindana naye kwa yale unayoyafanya ni
wewe mwenyewe. Kila siku unatakiwa kuwa bora zaidi ya jana ili kuyaweka maisha
yako katika nafasi nzuri ya kufanikiwa.
5.
Hawapotezi muda kuwa na watu hasi.
Kwa
mujibu wa wataalamu wa mambo ya mafanikio wanatuambia kwamba, tabia na mienendo
yako kwa ujumla inaathiriwa sana na watu wanaokuzunguka. Watu wanaokuzunguka
wana athari kubwa sana juu ya maisha yako, haijalishi athari hizo ni chanya au
hasi.
Kwa
kulijua hilo watu wenye mafanikio, huwa ni watu ambao hawapotezi muda wao
kabisa kuwa na watu hasi. Kwa sababu wanajua watu hao watawakatisha tamaa na
kuwafanya washindwe kufikia malengo yao waliyojiwekea. Hivyo hicho ni kitu
amabacho huwasaidia sana kufanikiwa.
6.
Hawapotezi muda kwa mambo wasiyoyaweza kuyatawala.
Katika
maisha ya binadamu huwa yapo mambo na matukio ambayo katika hali ya kawaida
huwa si rahisi kuyatawala. Matukio haya yanaweza yakawa kama ajali, ugonjwa,
kufikiwa au hali mabaya ya uchumi. Haya ni baadhi ya matukio ambayo binadamu
huweza kukutana nayo na sio rahisi kwake kuyatawala.
Kwa
watu wenye mafanikio, wanapokutana na matukio ya aina hii, kwao huwa si rahisi
sana kupoteza muda na kuendelea kuyafikiria. Kitu wanachokifanya yanapowakuta
matukio kama hayo ni kuyapokea kama yalivyo, kisha baada ya kuyatatua basi
huachana nayo na si kuendelea tena kuyafikiria kila wakati.
Kwa
kuhitimisha makala haya, naamini umejifunza kitu kuhusiana na mambo amabayo
watu wenye mafanikio ambayo hawapotezi muda wao kuyafikiria sana. Kitu cha
kufanya chukua hatua za kuelekea kubadilisha maisha yako.
Tunakutakia
kila la kheri katika safari ya maisha yako. Kitu kikubwa ambacho kama DIRA YAMAFANIKIO tunakuomba ni kwamba endelea kuwashirikisha wengine ili waweze
kujifunza kama wewe unavyofanya sasa.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.