Jun 6, 2016
Jambo La Msingi Unalotakiwa Kulijua, Ili Kutimiza Ndoto Na Malengo Yako.
Naomba
nianze makala hii kwa kukuuliza hivi je, umeshawahi kujiuliza ni sifa gani
walizonazo matajiri hadi kuwapelekea wao kuwa matajiri? Je, pia ulishawahi
kujiuliza ni mambo yepi ya ziada wanayowafanya watu mtajiri kuzidi kuwa
matajiri? Au je, pia na wewe binafsi ulishawahi kujiuliza ni aina gani ya
tabia, sifa, au imani unayotakiwa uwe nayo ili uwe tajiri?
Nimeanza
maswali hayo kukufikirisha kidogo kwa sababu naamini na wewe ni kati ya watu
ambao wapo kwenye safari ya kuelekea kwenye utajiri kama ilivyo kwangu. Na ni
vyema ukawa unajua majibu ya maswali haya ili wakati upo kwenye safari yako ya
kutafuta mafanikio makubwa ya utajiri yawe msaada kwako.
Naamini
sana hakuna mtu asiyependa mafanikio makubwa. Kila mtu anapenda mafanikio
makubwa ila tatizo la walio wengi hufikia mahali wanashindwa kujua waanzie wapi
ili kufika kwenye kilele cha mafanikio makubwa. Nasema hivyo nikiwa na maana,
ukisema hutaki utajiri basi utakuwa ni sawa na kuniletea hadithi ya sungura ‘sizitaki mbivu hizi’.
Sasa
kama nia na lengo ni kufikia mafanikio makubwa tena ya utajiri, huwezi kukwepa
kujua sifa, tabia na hata mambo wanayofanya matajiri ili kufikia pale walipo.
Bila kujua vitu hivyo ambavyo wanavifanya matajiri na hadi kufanikiwa itakuwa
ni kazi bure kwako kuweza kufanikiwa. Juhudi zako nyingi ambazo utakuwa
unaziweka zitakuwa hazina msaada sana.
Kwa chochote unachokifanya, kifanye kwa ujasiri. |
Watu
wenye mafanikio siku zote mambo yao na mipango yao wanaifanya kwa ujasiri na
kujiamini sana. Na mara nyingi huwa haijalishi wana uzoefu katika jambo hilo au
hawana, kikubwa wanachokizingatia ni kufanya kwa ujasiri hadi kufanikiwa, hata
kama hawana uhakika na matokeo. Ni ujasiri huohuo ambao kwa namna moja au
nyingine hupelekea wao kuwa washindi.
Ili
uweze kunielewa zaidi katika hili hebu twende kwa mifano. Mark Zuckerberg
mwazilishi wa mtandao maarufu wa facebook,
asingeweza kuanzisha mtandao huo ikiwa ndani yake asingekuwa na sifa ya kutenda
kwa ujasiri. Kilichokuwa kikimpa jeuri kwamba ni lazima atafanikiwa ni kule
kuamua kutenda kwa ujasiri. Na hiyo kweli ilimsaidia kufanikiwa.
Mwangalie
Evander Holyifield mpiganaji wa ngumi
enzi hizo pia naye asingeweza kumpiga Mike
Iron Tyson kama tu asingeamua kubeba sifa ya kutenda kwa ujasiri. Ilikuwa
sio rahisi kwa mtu yoyote kuamini eti Tyson
anaweza kupigwa na Evander hasa
kutokana na Tyson alivyokuwa na uwezo
mkubwa wa kupigana ikiwa pamoja na kushinda karibu kila shindano.
Ukitenda kwa ujasiri unaweza. |
Hiyo
haitoshi hebu tutazame maisha ya Nick Vujicic.
Kwa kumtazama ni rahisi sana kumuonea huruma kwa sababu ya ulemavu wa miguu
alionao. Lakini ukiona maisha ya mafanikio aliyonayo unaweza ukalia kwa
kujionea huruma wewe kwa kuwa kamili lakini huna kitu.
Nick Vujicic
pamoja na ulemavu wake huo amefanikiwa kuwa mhamasishaji wa mafanikio na
kutenda mambo mengi sana ikiwemo hata kucheza piano, kuandika kwenye kompyuta
lakini akiwa hana mikono wala miguu. Kitu kikubwa kilichomfikisha hapo ni kule
kuamua kutumia sifa ya kutenda bila kuogopa kitu chochote.
Ukiangalia
historia ya dunia utakuja kuona ina watu wengi ambao waliitwa hawawezi kutokana
na walivyochukuliwa lakini wao walijiaminisha na kuweza. Ipo nguvu kubwa sana
ya kufanikiwa kama utatumia sifa ya kutenda kwa ujasiri. Tunaposoma maandiko
matakatifu yanatuonesha, hata Goliathi alipigwa na Daudi hiyo yote kwa sababu
Daudi aliamini nguvu kubwa ya kuweza kutenda kwa ujasiri.
Kuna
wakati katika maisha unaweza kupambana na changamoto nyingi sana, kiasi kwamba
ukajiona huwezi kitu tena. Lakini inapotokea hivyo, simama tena na jiambie
unaweza kupambana na chochote na hakika utakuwa mshindi. Kwa chochote
unachofanya, hata kama unakiona ni kigumu sana kifanye kwa kumaanisha huku
ukitenda kwa ujasiri, utafanikiwa.
Watu
waliofanikiwa si kwamba wao wana akili sana au uwezo mkubwa wa tofauti.
Wanafanikiwa kwa sababu wanaamua kutenda kwa ujasiri. Kila wanapokutana na
changagamoto hukabiliana nazo hivyo hivyo kwa ujasiri mkubwa. Siku zote acha
kujiruhusu kushindwa kwa urahisi, utapotea sana na hutafanikiwa. Lilokubwa
kwako tenda kwa ujasiri hadi kufanikiwa.
Je,
jiulize tena katika maisha yako unatenda mambo yako kwa ujasiri? Kama uko
kinyume na hapo anza sasa kutenda mambo yako kwa ujasiri ili kufanikiwa.
Kama
makala hii imekuasidia kwa namna moja au nyingine mshirikishe na mtu mwingine
aweze kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Nakutakia
siku njema na mafanikio mema.
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.