Jul 27, 2016
Je! Wajua Ni Kwa Nini Mpaka Leo Malengo Yako Hayajatimia?
Moja
yachangamoto ambayo inawakabili watu wengi ni kwamba ni wazuri sana wa kusema
kuliko kuchua hatua, hapa nina maana ya kwamba kila mmoja anapenda kuona matarajio
yake yanatimia.
Hata
hivyo, kutokana na imani hiyo imepekelekea watu wengi sana kubaki na maisha
yale yale kila siku. Unajua ni kwanini? Basi nakusihi ufuatane nami kwani
nataka nikijuze siri ambayo watu wengi hawaijui juu ya upangaji wa malengo.
Ipo
hivi niliwahi kufanya uchunguzi mdogo katika kazi yangu ya uhamasishaji mahali
fulani, moja ya mada ambayo nilikuwa naizungumzia siku hiyo ilikuwa inahusiana
na jinsi gani unavyoweza kutimiza
malengo yako na kila mmoja ilionekana kufurahia somo hilo. Kila mmoja
wetu ambaye ulikuwepo siku hiyo ilionekana dhahiri anayo ndoto ambayo inasukuma
kufikia kilele cha mafanikio.
Ndipo
nikachukua jukumu la kutaka kujua kila mmoja aliyekuwepo siku hiyo ni nini
ambacho anadhamiria katika maisha yake? Kila mmoja alieleza kwa mapana kutoka
na dhamira inavyomsukuma kutoka nafsini kwake. Baada ya kumaliza zoezi hilo la
kujua kila mtu lengo lake, ndipo nikawataka watu hao hao waandike kuhusiana na
njia ya kutimiza ndoto hizo.
Moja
ya maajabu ambayo niliyaaona ni kwamaba watu wengi ni wazuri sana wa kusema
nataka kuwa mtu fulani lakini linapokuja suala la utekelezaji wa jambo hilo
hapo ndipo ukakasi hujitokeza unajua ni kwanini? Niligungundua ya kwamba watu
wengi wana ndoto lakini hawajui mbinu za kutekekeza, hata wale ambao wanajua ni
wepesi sana wa kukuta tama.
Ndipo
nikawambia ya kwamba kwa jambo lolote ambalo unalitamani liwe kweli ni lazima
ujue mbinu ya utekelezaji wa jambo hilo hususani kwa kujifunza na ikiwezekana
kulipa gharama, lipa gharama kwa kuwa hakuna maisha ya kimafanikio ambayo
hayana gharama.
Pia
ikumbukwe ya kwamba katika kujifunza hukohuko kuna changamoto zake, changamoto
hizo hizo ndizo ambazo huwafanya watu wachache waweze kuhimili mikiki ya jambo hilo, na hawa ni watu ambao
wamefanikiwa katika sayari hii. Hata hivyo kwa asilimia kubwa ambapo wengi wetu
ambao ndio tupo humo huwa hatupo tayari kuvumilia mikikimikiki ya changamato
ambazo mara nyingi hujitokeza katika mambo amabayo tunayafanya.
Wengi
wetu tupo tayari kuahairisha mambo na
kuleta visingizio visivyokuwa na maana yeyote ile, kwa mfano unakutana na mtu
anakwambia anataka kufanya biashara fulani lakini changamoto yake kubwa ni mataji. Kimsingi ukichunguza changamoto hiyo
utagundua ya kwamba ni sababu yatima, nikiwa na maana ya kwamba huna haja ya
kuacha kufanya jambo fulani eti kwa sababu ambazo hazina msingi wowote.
Tuende
mbele turudi nyuma na kuyatafakari maisha ambayo tunayaishi leo hii, ni kwanini
yapo vile vile? Ni wakati wako muafaka ewe msomaji ambaye unasoma makala haya
kuweza kutafakari kwa umakini jambo hili japo kwa dakika chache na kuendelea
kutafakari juu ya maisha yako.
Tafakari
ni kwanini mpaka leo hii hujatimiza malengo yako? Kama umepata jibu, zama tena
katika halmashauri yako ya kichwa tafakari tena je unahisi sababu ambazo
umezipata ni za msingi au sio za msingi?
Kama umekwisha pata majibu inua macho yako mbiguni, tazama mbigu inavyong`ara
kisha tafakari tena na uje na majibu ya kina je unachukua hatua gani kwa hayo
yote uliyowaza? Usinibe majibu.
Mmmh,
sawa labda nisiendelee kuongea sana, maana naweza nikakupoteza kabisa ila cha
msingi ni kwamba tafakari hayo machache kisha uchukue hatua mathubuti za
kiutendaji. Hata hivyo nikazie kwa kusema ya kwamba mara zote ukiwa na malengo
usiishie kusema tu, bali onyesha njia sahihi za utekezaji. Kufanya hivi kutukupa
mwelekeo tosha kwa upande wako kwa kuonesha ni nini! Ambacho unatakiwa kuwa
nacho? Na baada ya muda gani!
Huenda
bado ukawa haujanielewa nazungumzia masuala ya uwezo wa utekelezaji wa jambo
hilo. Maana tunafahamu ya kwamba ili yaitwe mafanikio kuna njia ya kufikia
mafanikio hayo kwa mfano kujifunza kutoka kwenye vitabu, video, semina na watu
wengine ambao kiujumla wamekwisha fanikiwa. Nikakumbushe kwa mala nyingine kuwa
ni lazima uwe na picha kamili ya kule ambapo unataka kuelekea.
Nikushuru
sana kwa kusoma makala haya, lakini shukrani zangu zangu zitakuwa zimekamilika
endapo utachukua hatua kwa hayo ambayo umekwisha yasoma kwenye makala haya.
Nikusihi ya kwamba ulichojifunza mshirikishe mwenzako kama ambavyo mimi nmefanya
kwako.
Endelea kujifunza kupitia dirayamfanikio.blogspot.com kila siku.
Ndimi;
Afisa mipango Benson Chonya
Blogu;
dirayamafanikio.blogspot.com
Simu; 0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.