Jul 11, 2016
Huna Haja Ya Kukata Tamaa, Mafanikio Yako Yanaanza Na Kitu Hiki.
Kila
safari yoyote unayoijua wewe, siku zote huanza na hatua moja. Hatua hiyo
hutengeneza hatua ya pili na mwisho wa siku safari nzima hata iwe ya kilometa nyingi kiasi
gani huweza kukamilika.
Kila
mradi wowote unaouona upo duniani mwanzo wake ulianza tu na wazo wala si mradi
kama hivyo unavyouona. Lakini wazo hilo liliweza kuendelezwa kidogo kidogo na
mwisho mradi ule ukaanza.
Kila
jengo unaloliona limesimama popote pale, pia mwanzo wake lilianza kwa tofali
moja tu. Tofali hilo liliweza kuendelezwa na matofali mengine juu yake mpaka
likaja kutokea jengo kubwa kabisa, pengine kufikia ghorofa.
Pia
kila kitabu kiliachoandikwa hata kiwe na kurasa nyingi vipi siku zote kilianza
kwa neno moja na hatimaye maneno hayo yakaunda sura, mwisho wa siku sura hizo
zikaunda kitabu chote kikakamilika.
Kila
siku mpya mara nyingi inaanza na nuru ya jua. Hainzi siku tu na mara tukaona
mchana. Huwa unaanza mwanga mdogo ambao unaashiria siku mpya nyingine imeanza.
Hivyo
ndivyo kila kitu ambavyo huwa kinaanza duniani. Hakuna kitu ambacho kilitokea
tu na kuwa hivyo kama kilivyo. Ni lazima kilianzia mwanzo fulani, mwanzo huo na
siku zote huwa ni mdogo. Na hii ndiyo kanuni ambayo haiwezi kuvunjwa na kitu
chochote.
Inawezekana
unasoma makala hii upo kwenye maisha magumu na umekata tamaa kabisa na huoni
tumaini la mafanikio. Lakini ninachotaka kukwambia huna haja ya kukata tamaa,
kwani kila mafanikio unayoyatafuta huwa yanaanza hatua kwa hatua, tena wakati
mwingine hatua ndogo kabisa.
Kama
kuna kitu ulitaka kukifanya, kifanye na kukifanikisha acha kujidharau kuwa
hakiwezi kuleta mabadiliko kwako hiyo si kweli. Kama umeamua kufanya biashara fulani
fanya na siyo lazima uanze na mtaji mkubwa kama unavyofikiri, anza kidogo na
hicho ulichonacho, mwisho wa siku kitakuwa kikubwa na utafanikiwa.
Mabadiliko
yote unayoyataka huwa yanaanza hatua kwa hatua. Na ukumbuke kwamba huwezi
kufanikisha kitu katika maisha yako kama usipoanza hatua moja kwanza. Hiki ni kitu
cha msingi sana katika mafanikio yoyote na ni lazima ukipitie. Vinginevyo kama
utajidanganya ipo njia ya mkato hutofanikiwa.
Hilo
unaweza ukaliona vizuri kwenye hatua za ukuaji wa mtoto. Bila shaka kila mtoto
unajua ni lazima atambae ndipo atembee na mwisho kukimbia. Hakuna mtoto aliyezaliwa
na kuanza kutembea. Huwa zipo hatua za lazima ambazo kwake ni lazima azipitie
ili kukamilisha ukuaji wake.
Hivyo
ndivyo ilivyo kwenye mafanikio, siku zote hakuna mafanikio ya mkato wala ya
haraka. Mafanikio ni mchakato unaenda hatua kwa hatua. Ndiyo maana watu wengi
ambao huwa wakitafuta mafanikio ya mkato hujikuta mara nyingi wakiishia pabaya
sana kuliko walivyokuwa mwanzo.
Hiyo
yote inatuonyesha huwezi kuvunja kanuni za
mafanikio hata iweje. Ni lazima hatua zifuatwe. Kwa hiyo hata hali yako
iwe mbaya vipi kiuchumi uwezo wa kubadilisha maisha yako unao. Kikubwa jipe
muda wa kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua na kila kitu kitabadilika mpaka
utashangaa.
Kumbuka
hakuna lisilowezekana. Amua kuwa utachukua hatua hata kama ni ndogo vipi lakini
zinakupeleka kule kwenye lengo lako. Kama nilivyoanza makala hii kila kitu huwa
kinaanza kidogo kidogo, hata maisha yako yanakwenda kubadilika ikiwa utachukua
hatua hizo ndogo na kuacha kusubiri tena. Ni bora ukasonga mbele ukiwa
unatambaa kuliko ukawa umekaa unasubri.
Nakutakia
kila la kheri katika safari yako ya kuboresha maisha yako na endelea kutembelea
DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia
mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035
kwa ushauri na msaada wa haraka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.