Jul 20, 2016
Mambo Ya Msingi Kuzingatia Katika Kilimo Cha Alizeti.
Alizeti hulimwa kwa wingi katika
mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya,
Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA
UZALISHAJI
Kuchagua aina bora ya mbegu. Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa,
wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta. Vilevile chagua
aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji.
KUWEKA MBOLEA
Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea
za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora.
KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA
Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavuno. Hivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na bora. Pia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidi. Njia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema.
Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavuno. Hivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na bora. Pia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidi. Njia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema.
MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA;
UKAGUZI
Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaa. Alizeti hukomaa kati ya miezi minne hadi sita tangu kupanda. Wakati huo punje huwa na unyevu wa asilimia 25. Ni muhimu kuvuna alizeti mapema ili kuepuka mashambulizi ya panya, mchwa na ndege waharibifu.
UKAGUZI
Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaa. Alizeti hukomaa kati ya miezi minne hadi sita tangu kupanda. Wakati huo punje huwa na unyevu wa asilimia 25. Ni muhimu kuvuna alizeti mapema ili kuepuka mashambulizi ya panya, mchwa na ndege waharibifu.
DALILI ZA ALIZETI ILIYOKOMAA
Suke hubadilika rangi kutoka manjano na kuelekea kuwa nyeusi. Viuwa vya pembeni mwa suke hunyauka na hubadilika kutoka rangi ya manjano na kuwa ya kahawia.
UVUNAJI, UKAUSHAJI NA UBEBAJI
Suke hubadilika rangi kutoka manjano na kuelekea kuwa nyeusi. Viuwa vya pembeni mwa suke hunyauka na hubadilika kutoka rangi ya manjano na kuwa ya kahawia.
UVUNAJI, UKAUSHAJI NA UBEBAJI
Vifaa vya kuvunia na kubebea kutoka
shambani
Kisu, Vikapu, Magunia, Matenga Vifaa vya kukaushia, Maturubai, Mikeka, Kichanja bora, Vyombo vya usafiri kutoka shambani, Matoroli, Matela ya matrekta, Mikokoteni ya kukokotwa na wanyama, Magari KUVUNA Alizeti huvunwa kwa kutumia mikono ambapo suke hukatwa kwa kutumia kisu.
Kisu, Vikapu, Magunia, Matenga Vifaa vya kukaushia, Maturubai, Mikeka, Kichanja bora, Vyombo vya usafiri kutoka shambani, Matoroli, Matela ya matrekta, Mikokoteni ya kukokotwa na wanyama, Magari KUVUNA Alizeti huvunwa kwa kutumia mikono ambapo suke hukatwa kwa kutumia kisu.
Pia mashine (combine harvester)
hutumika kuvunia alizeti katika nchi zinazolima alizeti kwa wingi. Masuke ya alizeti
huwekwa kwenye vikapu ambavyo hutumika kusomba alizeti ndani ya shamba. Kisha
alizeti hufungashwa kwenye magunia na kusafirishwa hadi nyumbani tayari kwa
kukausha.
KUKAUSHA
Kuna hatua mbili za kukausha alizeti;
kukausha masuke na kukausha mbegu za alizeti. Kukausha masuke . Masuke
hutandazwa kwenye kichanja bora katika kina kisichozidi sentimita 30 ili yaweze
kukauka vizuri. Vilevile huweza kutandazwa kwenye maturubai, mikeka au
sakafu safi. Lengo la hatua hii ni kukausha masuke ya alizeti ili kurahisisha
upuraji.
KUPURA Upuraji hufanyika baada ya
kuhakikisha kuwa masuke ya alizeti yamekauka vizuri. Masuke ya alizeti hupurwa
kwa kutumia mikono ambapo mbegu hutenganishwa kwa kupiga masuke taratibu
kutumia mti. Ni muhimu kupiga masuke taratibu ili kuepuka kupasua mbegu. Pura
kwenye kichanja bora, maturubai au mikeka.
KUKAUSHA MBEGU
Mbegu za alizeti hukaushwa juani kwa
kutandazwa kwenye vichanja bora, maturubai, mikeka au sakafu safi. Tandaza
mbegu katika kina kisichozidi sentimita 4 ili ziweze kukauka vizuri.
Lengo la hatua hii ni kukausha mbegu baada ya
kupura ili kufikia kiwango cha unyevu kinachotakiwa kwa hifadhi salama ambacho
ni asilimia 8.
JINSI YA KUTAMBUA MBEGU ZILIZOKAUKA
VIZURI
Kufikicha mbegu
Mbegu zilizokauka
maganda yake hutoka kwa urahisi zinapofikichwa. Kumimina kwenye chombo kama
debe, Mbegu zilizokauka hutoa mlio mkali zinapomiminwa kwenye vyombo
hivyo. Mbegu zilizokauka hung’ara Kutumia kipima unyevu. Mbegu zilizokauka
vizuri kipimo huonyesha asilimia 8.
KUPEPETA NA KUPEMBUA
Kupepeta na
kupembua hufanyika ili kuondoa takataka kama vile mawe, wadudu, mapepe, mbegu
zilizooza au kupasuka. Mbegu za alizeti hupepetwa kwa kutumia ungo au mashine
zinazoendeshwa kwa mkono, injini au umeme. Mashine hizi zina uwezo wa kupepeta
na kupembua kilo 60 hadi 350 kwa saa kutegemea aina ya mashine na ukubwa wa
mashine yenyewe
KUHIFADHI
Alizeti iliyopurwa huhifadhiwa katika
hali ya kichele kwenye maghala bora, yaani vihenge, sailo au bini. Alizeti ya
kuhifadhi kwenye maghala ya nyumba ifungashwe kwenye magunia na ipangwe kwenye
chaga kwa kupishanisha. Ili kurahisisha kazi ya kukagua ghala, acha nafasi ya
mita moja kutoka kwenye ukuta. Ziba sehemu zote za ghala ili kuzuia panya
kuingia.
Panya hupenda sana kula punje za
alizeti, na husababisha upungufu mkubwa wa punje ambao husababisha upotevu wa
asilimia 30 kwa kipindi cha miezi mitatu ya hifadhi. Asilimia ya upotevu
inaweza kuwa kubwa zaidi kutegemea idadi ya panya na upatikanaji wa vyakula
vingine kwa wakati huo. Matumizi ya Mbegu za Alizeti Mbegu za alizeti hasa
zenye mistari zinaweza kuliwa baada ya kukaangwa au kukaushwa. Pia zinatumika
katika utengenezaji wa mikate. Mbegu za alizeti husindikwa kupata bidhaa ya
mafuta.
KUSINDIKA MBEGU ZA ALIZETI KUPATA
MAFUTA
Vifaa
Mashine ya kukamua mafuta
Chujio safi
Ndoo
Vifungashio
Sufuria
Mizani Malighafi
Mbegu za alizeti
Maji
Chumvi
NJIA YA KUKAMUA MAFUTA
Chagua mbegu bora za alizeti
Zianike kwenye jua kwa muda wa saa 1
hadi 2
W eka kwenye mashine ya kukamulia ya
daraja au Ram
Kamua mafuta
Chuja mafuta kwa kitambaa au chujio
safi
Pima mafuta yaliyokamuliwa.
Ongeza maji na chumvi. Katika lita 10
za mafuta weka lita moja ya maji na gramu 200 za chumvi.
Weka mafuta kwenye chombo cha
kuchemshia (sufuria)
Chemsha hadi maji yote yaishe
Sauti ya kuchemka ikiisha ni dalili
kuwa maji yamekwisha.
Ipua, acha yapoe, kisha chuja kwa
kitambaa safi au chujio
Fungasha kwenye vyombo safi na vikavu
na vyenye mifuniko
W eka lakiri na lebo
Hifadhi kwenye sehemu safi, kavu na
yenye mwanga hafifu.
MATUMIZI
Mafuta hutumika katika mapishi
mbalimbali na yana virutubishi vifuatavyo: - Mafuta gramu 100 Nguvu kilokalori
900
WASTANI WA MAVUNO YA ALIZETI KWA EKARI MOJA.
Ukipata shamba zuri ekari moja ya alizeti huweza kukupatia
kati ya magunia5-10 kutegemeana na aina ya mbegu uliyotumia na pia namna shamba
lako ulivyolihudumia.
Kwa maswali na
majibu kuhusu kilimo bora cha kisasa kitakachokutoa kwenye umaskini pamoja na
ufungaji wa hema(Green House) na Drop irrigation, unaweza ukawasiliana na
mtaalamu wetu wa kilimo Ndugu John Mabalaga kwa mawasiliano 0754 282 448.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.