Jul 4, 2016
Mambo Manne (4) Yanayofanya Maisha Yako Kuwa Bora Wakati Wote.
Wengi
wetu katika maisha, tunapenda sana kuwa na maisha bora. Hakuna hata mmoja
ambaye anapenda maisha yake yawe hovyo. Kila mmoja wetu hujitahidi kwa kadri
anavyoweza ili kufanya maisha yawe bora na thamani kubwa.
Lakini
hata hivyo wengi bado huwa hawajui mambo ambayo wanatakiwa kuyafanya ili
kufanya maisha yao kuwa bora. Kwa sababu hiyo wengi hujikuta wakifanya hata mambo
yasiyowasaidia kufanya maisha yawe bora, zaidi ya kuwarudisha nyuma.
Ni
kusudio la makala haya likusaidie kutambua mambo unayotakiwa kuyazingatia ili kufanya
maisha yako kuwa bora kila siku. Kwa kujifunza mambo hayo itakusaidia
kubadilika wewe na hata wale wanaokuzunguka siku hadi siku.
Yafuatayo Ni Mambo Manne
(4) Yanayofanya Maisha Yako Kuwa Bora Wakati Wote.
1.
Thamani.
Unaweza
kuwa ni ukweli unaouma lakini huo ndio uhalisia kwamba, huwezi kufanikiwa
katika maisha yako kama hutoi thamani inayostahili. Ni lazima utoe thamani ili
kupata hicho unachokihitaji. Unaposhindwa kufanya hivyo lazima maisha yako
yatakwama tu.
Mara
nyingi tumekuwa tukiambiwa tunavuna tulichopanda. Ndiyo, huo ndio ukweli. Huwezi
kuvuna mafanikio makubwa kama thamani unayotoa ni kidogo au haiendani na
mafanikio hayo unayoyataka. Kama hutoi thamani inayostahili tambua kabisa
mafanikio yako yatakuwa kidogo sana.
Hivyo,
ni jukumu lako wewe kuongeza thamani katika maisha yako katika kila eneo ambalo
unaona haupo vizuri. Kwa mfano kama unaona huna maarifa ya kutosha katika jambo
fulani, ongeza maarifa hayo na kujiboresha kila siku kwa kujisomea vitabu. Hapo
utafanikiwa na kujenga maisha bora unayoyataka.
2.
Marafiki wazuri.
Kujijengea
marafiki wazuri ambao wanakupa nguvu na hamasa katika safari ya mafanikio, ni
jambo ambalo lipo wazi lazima lifanye maisha yako kuwa bora na thamani.
Marafiki ni chachu kubwa sana ya mafanikio ikiwa utawatumia vizuri.
Ogopa
sana kuwa na marafiki hasi, wakatisha tamaa na ambao watakufanya kila wakati
ujisikie vibaya. Jifunze kutafuta ‘timu’
nzuri ya marafiki itakayokufikisha juu kwenye kilele cha mafanikio. Marafiki
hao watakusaidia kushirikiana katika mipango mizuri na kufanya maisha yako kuwa
bora.
3.
Familia bora.
Maisha
bora lazima yahusishe familia bora. Familia hii bora unatakiwa kujijenga wewe.
Huwezi kujidai ukasema eti maisha yako ni bora wakati familia yako iinateseka.
Ni lazima uhakikishe familia yako iko salama na inapata mahitaji yote muhimu
kwanza.
Ukiwa
kama baba wa familia ni muhimu kulijua hili na kulifanyia kazi. Migogoro ya
hapa na pale ni lazima kuachana nayo ili kujenga familia bora. Furahia maisha
na watoto wako, furahia maisha na mke wako hapo utakuwa unajijengea maisha bora
ambayo kila mtu atayatamani.
4.
Maisha ya kiroho.
Ni
muhimu sana kuishi maisha ya kiroho ili kufanikiwa. Ni lazima utambue uwepo na
HOFU ya Mungu ili kufanikiwa. Huu utakuwa ni msingi bora na muhimu sana kwako
na kizazi chako kijacho katika kutengeneza maisha bora ya kila siku.
Kwa
kuzingatia thamani unayotoa, marafiki wazuri wanaokuzunguka, kujenga familia bora
na kuishi maisha ya kiroho ni lazima utaishi maisha bora na utaiona dunia ni
moja ya sehemu safi na salama sana kwako.
Nikutakie
siku njema na endelea kuwaalika wengine waweze kujifunza kupitia mtandao huu wa
DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki, Imani Ngwangwalu.
MUHIMU; Tunatambua umuhimu wako mpenzi msomaji wa makala
haya, hivyo tunaomba maoni/ushauri wako kwani tunahitaji kufanya marekebisho ya
mtandao wetu wa Dira ya Mafanikio ili uwe bora zaidi. Tuambie ni nini unataka
tuongeze au tupunguze.
Tuma maoni yako kwenda namba 0757909942/0713048035 au dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.