Jul 15, 2016
Kwanini Hutakiwi Kuwa Na Watu Hasi Kwenye Maisha Yako?
Moja
ya msisitizo mkubwa ambao mara nyingi tumekuwa tukitoa kama DIRA YA MAFANIKIO
ni kwamba ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe chanya wakati wote. Hilo tumekuwa
tukiliongelea sana kupitia makala mbalimbali tunazozitoa hapa.
Tumekuwa
tukiongea hilo na kuendelea kusisitiza uchanya huo hautakiwi kuwa nao wewe tu
bali mpaka watu wanaokuzunguka. Watu hawa wanaokuzunguka ni pamoja na marafiki,
ndugu na hata jamaa zako wa karibu sana.
Kitu
pengine unachotaka kujiuliza, kwa nini ni muhimu sana kuwa na watu chanya katika maisha yako. Kama
hilo ndilo swali lako majibu yake unakwenda kuyapata kwa kusoma makala haya, na
utajua ukweli kwa nini hutakiwi kuwa na watu hasi kwenye maisha yako.
1.
Utakuwa kama wao.
Kiuhalisia,
wewe ni matokeo ya watu watano wanaokuzunguka. Kama unazungukwa na watu watano
ambao ni wadanganyifu upo uwezekano mkubwa ukawa mdanganyifu pia. Kama unazungukwa
na watu watano maskini ni rahisi pia na wewe kuendelea kuwa maskini.
Watu hasi ni sumu kubwa ya mafanikio yako. |
Kwa
kundi lolote unalozungukwa nalo upo uwezakano wa kuwa kama wao. Kama ni hivyo
ni hatari sana kuwa na watu hasi, haijalishi uhusiano wenu ni wa kindugu au
kirafiki. Kwa kitendo cha kuwa nao, elewa ni lazima na ni rahisi sana kufanana
na wao utake au usitake.
2.
Ujasiri wako unapungua.
Unapokuwa
na watu hasi ni wazi lazima ujasiri wako utapungua. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu
ni rahisi kusikia maneno kama hutaweza kuwa tajiri, huna bahati au una mikosi
sana huwezi kufanikiwa na maneno mengine mengi yanayofanana na haya ili mradi
kukukatisha tamaa.
Unapokuwa
unatumia muda wako mwingi na watu hawa, kama nilivyosema watapunguza ujasiri
wako. Na kwa bahati mbaya ukikosa ujasiri huwezi kufanikiwa tena. Hivyo, lazima
uwe makini na watu hasi, vinginevyo kutokufanikiwa kwako kutakuwa nje nje.
3.
Huwezi kujifunza kitu kwa watu hasi.
Ikiwa
watu wako wa karibu unaoshirikiana nao ni watu wa kulaumu, kukaa kuongelea watu
wengine na wala hawajitumi, je, unafikiri unaweza kujifunza kitu kwao cha
kuweza kukusaidia kufanikiwa? Hata kwa akili ya kawaida hapo huwezi kujifunza
kitu sana sana utakatishwa tamaa kila siku.
Ifahamike
kwamba watu wote ambao wanafikiri hasi, hawafikiri makubwa huwa wana nguvu
fulani ya kukushawishi uwaze kama wao kwa namna ya hasi hasi. Kwa namna yoyote ile unatakiwa kuwa makini nao
na ndio maana ni muhimu kukaa nao mbali, vinginevyo watakukwamisha.
4.
Watakupotezea ndoto zako.
Pia
sifa nyingine ya watu hasi ni rahisi sana kukupotezea ndoto na malengo yako.
Kwa jinsi utakavyozidi kukaa nao utagundua kwamba mara kwa mara ni watu wa kutokuongelea
malengo ya kimaisha zaidi ya porojo za hapa na pale.
Sasa
unapokuwa na watu hawa si rahisi kufanikiwa. Ikiwa unazipenda ndoto zako na
kuziona zikitimia, acha mara moja kuendelea kuwa na watu hasi. Watu hawa
watakupotezea mengi sana katika maisha yako wakati mwingine hata bila wewe
kujijua.
Kumbuka
ni muhimu sana kuwakwepa watu hasi katika maisha yako kwa sababu unapokuwa nao
ni rahisi kuwa kama wao, watakufanya ushindwe kujiamini, hutaweza kujifunza
kitu kutoka kwao na zaidi watakupotezea ndoto zako za maisha.
Chukua
hatua sitahiki za kubadili maisha yako na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.