Jul 6, 2016
Sababu Zinazokufanya Ushindwe Kwa Kile Unachokifanya.
Kuna
wakati katika maisha yetu hali ya kushindwa, huwa inajitokeza kwa namna moja au
nyingine katika mambo tunayoyafanya. Kimsingi, kushindwa huko mara nyingi pia
huwa hakutokei kwa bahati mbaya.
Kiuhalisia,
huwa yapo mambo mengi yanayochangia kushindwa huko. Je, binafsi ulishawahi
kujiuliza kwa nini kushindwa kunakuwa kunajitokeza katika maisha yako kwa
wakati fulani?
Hebu
kwa pamoja tuangazie nukta kadhaa zitakazotusaidia kukumbusha kwa nini kushindwa
wakati mwingine kunajitokeza katika maisha yetu.
1.
Mitazamo tuliyonayo.
Mara
nyingi mitazamo tuliyonayo ina uwezo wa kukufanya ukafanikiwa au ukashindwa kwa
kile unachokifanya. Mitazamo tuliyonayo ina nguvu kubwa ya kubadili maisha
yetu. Na mitazamo hii kuna wakati ina waangusha wengi kwenye safari ya
mafanikio bila kujua.
Kwa
mfano utakuta mtu ana karibu kila kitu, lakini unashangaa ameshindwa kwenye
jambo fulani. Ukichunguza chanzo ni mitazamo aliyobeba. Unapokuwa unajibebesha
mitazamo hasi, mitazamo ya kuona huwezi kwa kile unachokifanya ni lazima
utashindwa.
Mitazamo uliyonayo inauwezo wa kukufanya ukashindwa. |
2. Kukosa uvumilivu.
Wengi
wanashindwa katika maisha na kwa yale mambo wanayofanya kwa sababu tu ya kukosa
uvumilivu. Watu hawa hawashindwi si kwa sababu hawana maarifa au uwezo bali ni
kwa sababu ya kukosa uvumulivu wa kuwasaidia kuendelea mbele.
Kwa
mfano watu hawa wanaoshindwa, wanapokutana na changamoto hata kama ni ndogo
inakuwa ni rahisi sana kwao kukata tamaa na kuona kila kitu kimekwisha. Hivyo,
unapokuwa unakosa uvumilivu kwa kile unachokifanya ni rahisi na lazima
utashindwa.
3.
Kutokuwa tayari kujifunza.
Tatizo
kubwa walilonalo watanzania walio wengi ni kule kutopenda kujifunza. Kutokana
na tatizo hilo hupelekea wengi sana kushindwa kwa yale mambo wanayoyafanya.
Inawezekana hata wewe unashindwa kufanikiwa kwa viwango vya juu kwa sababu
hauko tayari kujifunza.
Kama
unafikiri nakuonea hebu jiulize, mwaka huu umesoma vitabu vingapi? Utaona idadi
ya vitabu ulivyosoma ni vichache au hakuna kabisa. Kwa sababu hiyo, huwezi
kufanikiwa kama huko tayari kujifunza. Ni lazima uwe na maarifa ya kutosha
kukusaidia kufanikiwa.
4.
Kurudia makosa yale yale.
Kuna
wakati unaweza ukajikuta unashindwa kwenye malengo yako, kwa sababu tu ya
kurudia makosa yale yale unayofanya kila wakati. Inapotokea umefanya kosa,
halafu kosa hilo ukalirudia tena na tena ni wazi kushindwa kwako itakuwa ni
rahisi sana.
Kitu
cha kutambua moja ya kitu kikubwa cha kuepuka ili usiendeleze kushindwa, acha
kurudia makosa yako mara kwa mara. Ukichunguza wengi makosa wanayoyafanya na kuyarudia
tena yamewagharimu na kupelekea wao kushindwa.
5.
Kukosa nidhamu binafsi.
Nidhamu
binafsi ni nguzo kubwa ya mafanikio makubwa. Unapokosa nidhamu hii kwa kawaida
kushindwa kwa kile unachokifanya hautaweza kukwepa. Unajua ni kwa nini? Ni kwa
sababu utafanya mambo mengi hovyo hovyo na kukuharibia ndoto zako.
Unapokuwa
na nidhamu binafsi inakujengea uwezo wa kujituma na kujitoa kweli kweli. Lakini
unapoikosa ni rahisi kwako kutumia pesa hovyo, au kufanya mambo yasiyokusaidia
kufikia ndoto hizo ulizonazo. Kwa namna yoyote ile ukiona huna nidhamu binafsi,
elewa hutaweza kufanikiwa.
Nimalizie
makala haya kwa kusema, mitazamo uliyonayo, ukosefu wa nidhamu, kukosa
kujifunza mara kwa mara na kushindwa kuvumilia, ni moja ya mambo yanayoweza
kukufanya ukashindwa kufanikiwa kwa jambo unalolifanya.
Chukua
hatua za kujifunza zaidi, lakini usiishie hapo tu endelea kuwashirikisha
wengine waweze kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika kusaka mafanikio ya kweli,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.