Jul 25, 2016
Sheria Tatu (3) Za Mafanikio (3 Laws Of Success).
Uhali gani mpenzi wa makala haya, ni
matumaini yangu makubwa umzima wa afya kabisa, katika makala hii natakaka
tujikite zaidi katika kujua sheria ambazo zitatufanya tuweze kutimiza
ndoto zetu.
Mara kadhaa umekuwa ukizoea kuona ya
kwamba mahali palipo na sheria lazima pawe chombo au mtu wa kuzisimamia ili
sheria hizo ziweze kutekelezeka kirahisi.
Lakini katika sheria za ya mafaniko
huwa ni kinyume kwa sababu haina haja ya kuwepo chombo au mtu wa kukuongoza
isipo kuwa wewe mwenyewe ndiye nahodha wa Maisha yako.
Maana tunaambiwa ya kwamba hatima ya
maisha yetu tunayo wenyewe. Hiyo ina maanisha kwamba sheria za mafanikio zipo,
uwe unajua au hujui, ila unapovunja sheria hizo lazima uadhibiwe na ulimwengu.
Leo katika makala haya, Afisa mipango
nataka nikushirikishe na wewe sheria tatu tu za mafanikio. Ikiwa ikatokea
ukazitumia sheria hizo uwe na uhakika utafanikiwa.
Zifuatazo Ndizo Sheria Tatu Za Mafanikio.
1. Fikiri (think).
Kila mwanadamu ana uwezo binafsi
ambao amezaliwa nao kwa ajili ya kufiri, lakini fikra hizo hizo hutofautiana
baina ya mtu mmoja na mwingine, hata siku moja hakuna mtu ambaye atafanana
uwezo wa kufikiri na mtu mwingine.
Hata hivyo kila kitu chochote ambacho
unakiona leo hii yupo mwazilishi wa kitu hicho. Hapa ina maana ya kwanza
yupo yule mwanzilishi wa kitu na yupo yule ambaye ni mtaalamu kwa ajili ya
kufanya marekebisho ya kitu hicho andapo kitukuwa hakipo sawa.
Vilevile katika kufanya vitu ambavyo
tunaviona leo vinazidi kuwa katika ubora huohuo hutuna budi kutazama vitu hivyo
katika jicho la tofauti sana, inawezekana bado hujanielewa ila ukweli ni huu
upo utofauti mkubwa kati ya kufikiri na kuwaza.
Mara kadhaa endapo utamsikia mtu
anasema nilitaka kufanya hiki na kile lakini hakijaenda kama alivyokuwa amepaga
ujue fika mtu huyo ni alikuwa anawaza tu. Lakini ukweli ni kwamba ukitaka kufika
kilele cha mafanikio yako huna budi kuweza kufikiri mambo kwa hali juu sana na
sio kuishia kuwaza tu.
Unajua ipo hivi hapa ulimwenguni
hakuna kazi ngumu kama ya kufikiri vitu vipya, na kama nilivyosema hapo awali
ya kwamba kila binadamu ana uwezo wake binafsi ambao amezakiwa nao kwa ajili ya
kufikiri, hapo sasa inategemeana ya kwamba unafikiria nini ?
Je ni mawazo chanya au mawazo hasi?
Tafakari kidogo kisha ugundue juu ya jambo hili .Hata hivyo wapo baadhi ambao
wamefanikiwa kimtazamo hata kimaisha watu hawa wao walifikiri mambo ya msingi
katika mtazamo chanya, ndivyo hivyo ambavyo leo inatupasa mimi na wewe kuweza
kutazama katika mtazamo huo huo ili tuweze kufanikiwa zaidi.
Kwa kuongezea pasipo kumung'unya
mdomo wala kuharibu silabi za matamshi, kila kitu ambacho unakifijiria ambacho
kipo katika mtazamo chanya huna budi kukiandika katika sehemu ambayo mara
kadhaa utakuwa unakiona, kufanya hivi kutakufanya uweze kufikiri kwa kina zaidi
ni kwa jinsi gani ambavyo unaweza ukakitekeleza kitu hicho. Mara kadhaa ukitaka
kufanikiwa zaidi kumbuka kufikiri tofauti.
2. Panga (plan).
Jambo la pili ndugu msomaji wa mada
hii, ni kwamba baada ya kufanya tafakari juu ya jambo lako huna budi kukaa
chini na kutengeneza mpango kazi kwa ajili ya utekelezaji wa jambo hilo. Katika
kupanga mpango kazi wa kile ambacho umekifikiria kitakupa picha kamili juu ya
kile ambacho unatamani kukifanya, hii ikiwa na maana ya kwamba kitakuwa na
matokeo chanya au matokeo hasi.
Kwa mfano labda unataka kufanya
biashara, ni lazima uwe na mpango wa kibiashara (business plan) ambayo itakupa
picha kamali ya jinsi ya biashara yako itakavyokuwa, kufanya hivi ni chachu ya
kufika mahali ambapo unatamani kufika.
Pia yamkini unatamani kufanya jambo
fulani kwa hapo mbeleni hivyo tumia muda huu kupanga mambo ya msingi
yatayokwenda kukufanikishia jambo lako. Maana kuna usemi ambao unasema ukikosea
kupanga mambo ya msingi umekwisha kufeli mambo yako.
3. Fanya (do).
Baada ya kufanya tafakari ya kina,
pia baada ya kupanga namna ya kutekeza, jambo la tatu huna budi kuanza kutenda
jambo hilo, si kutenda tu! Bali kutenda kwa njia tofauti na ulivyozoea kutenda
au watendavyo watu wengine.
Pia kwa jambo lolote ambalo unataka
kulifanya, au umekwisha kuanza kulifanya ili uone ya kwamba jambo hilo lina matokeo
kiasi gani ni lazima ukipende jambo hilo haijalishi lina changamoto kiasi
gani.
Kwa mfano unafanya biashara
haina haja ya kutumia nguvu katika kutafuta wateja bali unachotakiwa ni
kuongeza thamani katika bidhaa au huduma, kufanya hivi wateja watakuja wao
wenyewe, kwa sababu moja ya tabia ya wateja wengi wana tabia ya kuambiana hasa
ni wapi ambapo hutolewa huduma nzuri. Narudia kusema tena penda kutoka ndani ya
dhamira yako kwa jambo lolote ambalo unalifanya, maana hapa ndipo mzizi wa mafanikio
yako ulipo.
Ni matumaini yangu makubwa ya bila
shaka tumeelewana vizuri, na nikuhakikishe tu kwamba endapo ulichokisoma hapo
juu utakwenda kukiweka katika matendo basi mafanikio yanakuja kwako kwa
asilimia zote.
"Naamini katika kujifunza"
kama na wewe unaamini hilo tukutane tena siku nyingine katika makala ijayo.
Ndimi; Afisa Mipango; Benson Chonya.
Email; bensonchonya23@gmail.com
Phone no; 0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Asanteh kwa makala nzuri
ReplyDeleteAsanteh kwa makala nzuri
ReplyDelete