Jul 19, 2016
Mambo Manne(4) Ya Kuzingatia Ili Uweze Kufikia Ndoto Yako.
Nashika yangu kalamu ili kuleta maada
kama ambavyo inajieleza hapo juu. Sababu ya kuleta maada hii ni baada ya
kusikiliza radio katika kipindi ambacho huuongozwa na Harris Kapiga pamoja
Lilian Mwasha Antony na kumsikia mbunge ambaye ana umri mdogo kuliko wote
katika Bunge la Jamhuri ya Tanzania (2016) ambaye ana umri wa miaka 25 tu, na
huyu si mwingine ni MH. Augustine Vuma.
Inawezekana ukawa unajiuliza ni
kwanini nimeamua mpaka kuandika makala haya huenda ukasema ni kwasababu ya
msukumo wa kisiasa la hasha wala mimi huko sipo. Ila nimeamua kuandika makala
haya kwa sababu mosi naamini katika kujifunza, pili hii ni kutokana na mambo
ambayo ameyazungumza mbunge huyo, mambo ambayo kila mtu mwenye ndoto za
kimafanikio ambaye anatamani kuona malengo yake yanataka kutimia lakini haelewi
na jinsi gani ndoto hizo zitakwenda kutimia?
Hivyo nakusihi kama unaamini katika
kujifunza kama mimi uweze kuambana nami mwanzo mpaka mwisho wa makala haya ili
niweze kukujuza kile ambacho nimekisikia kutoka kwa watangazaji hao na mbunge
huyo. Kimsingi ni mambo ambayo ni ya msingi sana ambayo unatakuwa
kuyafahamu ili uweze kutimiza ndoto yako.
Kimsingi Kuna wakati mwingine ambao
umekuwa unatamani kuwa sehemu fulani kwa maana ya kwamba unatamani ndoto yako
iwe imetimia lakini umekuwa hujua ni vitu gani ambavyo unatakiwa kuvizingatia
ili kuweza kuwa kile ambacho unataka, nakusihi ushushe pumzi kisha twende sawa
maana nipo kwa ajili yako.
Yafutayo ni mambo manne (4) ya
kuzingatia ili iweze kutimiza ndoto yako.
1. Kuwa na nguvu ya rohoni.
Nguvu ya rohoni katika safari yako ya
mafanikio imegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya nguvu ya rohoni
amini katika Mungu kwamba mungu yupo hivyo unatakiwa kumuomba kwa imani
uliyonayo ili Mungu aweze kukusaidia, pia maisha ya dini yatakufanya uweze
kuishi kwa kanuni na sheria zake, pia kama una amini hilo ni lazima ndoto yako
itakwenda kuwa kweli maana Mungu ni muweza wa yote, sehemu ya pili ya nguvu ya
rohoni ni kwamba ni lazima uweze kujiamini wewe mwenyewe juu ya ndoto yako
kwamba inakwenda kutimia.
Mfano unataka kuwa mfanyabiashara wa
nguo ukiwa na imani hiyo ni lazima ndoto hiyo iweze kuwa kweli. Imani ndiyo
ambayo itakusaidia juu ya jambo lako kwa kuwa utakuwa pia unamini katika nguvu
ya Mungu ili kutimiza hilo jambo lako. Pia ikumbukwe ya kwamba nguvu hii ya
rohoni itakusaidia kukupa matumaini ambayo yatakusaidia kupambana pia
itakusaidia kukipata kile ambacho unakitaka uweze kukipata.
2. Kuwa na malengo.
Kila mtu kwa namna moja ama nyingine
ana malengo ila malengo hayo mengi huwa hayatimii kwa sababu mhusika huyo hajui
ni namna gani! Unaweza kuyatimiza malengo hayo? Usichoke endelea kufuatana nami
mpaka mwisho nitakujuza namna ya kutimiza malengo hayo. Moja ya njia bora ya
kutaka kutimiza malengo yako ni lazima uweze kujitambua.
Kujitambua huko ndiko ambako
kutakufanya uweze kujua wewe upo vizuri kwenye nini? Kwa mfano baada ya kufanya
uchambuzi huo ndipo utapojua kwamba wewe ni mkulima, mwanasisasa, mtangazaji,
mshereheshaji na mengine mengi. Baada ya kujua malengo hayo haijalishi ni
malengo ya muda mrefu au muda mfupi, ndipo utakapojua kwa undani zaidi kwamba
unaelekea wapi. Pia ikumbukwe ya kwamba uwe na malengo ya kitu ambacho
anakipenda kwani utakwenda kutenda kitu hicho kwa ufanisi zaidi bila kujali
changamoto ambazo zitajitokeza.
3. Kuwa na mikakati.
Baada ya kuwa na malengo ya jambo
ambalo unataka kuwa, jambo ambalo linafuata ni kuwa na mikakati, mikakati
ambayo itakufanya wewe uweze kufikia malengo yako, ila jambo la msingi la
kuzingatia kila mikakati yako ni lazima uiandike katika sehemu ya kumbukumbuka
zako ili isiwe rahisi kwako kuisahau. Inawezekana malengo yako yanahitaji
kujifunza kwa kusoma hivyo huna budi kusoma, kwa mfano unataka kuwa mwanasheria
na hayo ndio malengo yako ni lazima uweze kuwa tayari kujifunza kuhusu sheria.
Pia inawezekana unataka kuwa
mfanyabiashara fulani katika eneo fulani mara kadhaa umekuwa ukishauriwa ya
kwamba ni lazima ujifunze kwa watu ambao wanafanya vizuri biashara ni kweli
fanya hivo kwani hii itakupa matumaini ya kwamba na wewe unaweza. Sio kwa
biashara tu bali kwa jambo lolote ambalo unataka kufanikiwa ni lazima ujifunze
kwa watu waliofanikiwa. Pia tubakubushwa ya kwamba tusijifunze kwa watu
walioshindwa kwani hawawezi kutusaidia zaidi ya kutukatisha tamaa.
Kumbuka kama unataka kuwa mtu fulani
kwa hapo baadae ni lazima uanze kuishi ndoto hizo sasa. Mfano unataka kuwa
mbunge unatakiwa kuishi maisha hayo sasa japo hujafikia ubunge huo kwa
kuangalia wabaunge wanavyofanya sasa na wewe uanze kufanya vivyo hivyo kwa
sasa. Pia tunakubushwa ya kwamba kila fursa yeyote ni lazima iwe na maandalizi
bora ili kuweza kuwa kile unachotaka. Kuna mwandishi mmoja aliwahi kuandika na
kusema hivyo ulivyo leo unatoka na maabdalizi yako ya Jana. Hivyo kuwa na
maandalizi leo ya ndoto yako ya kesho.
4. Kuwa na bidii.
Kwa jambo lolote ambalo unalifanya
leo na unalitaka liwe matokeo chanya ni lazima ulifanye kwa juhudi na bidii
zote. Bidii ambayo itakufanya uweze kutimiza mikakati yako ambayo umejipangia
na mikakati hiyo itakusaidia kwa kiwango kikubwa kuweza kutimiza malengo yako.
Pia katika suala la kuwa na bidii
katika jambo lako ni lazima uwe chanya, kuwa chanya kunakufanya usiweze kukataa
tamaa mapema. Pia tuambiwa kukata tamaa ni dhambi kubwa sana, hasa katika
ulimwengu huu usikowa na mwisho hapa nina maana ulimwengu wa mafanikio.
Nafahamu fika ya kwamba inawezekana
mara kadhaa kuna watu wamekuwa wakikukatisha tamaa, nakusihii wasikilize watu
hao ila maneno yao ya kukukatisha tamaa yafanye kama chachu ya wewe kusonga
mbele zaidi.
Mwisho afisa nimalize kwa kusema
endapo utayazingatia hayo Ndoto yako inakwenda kuwa kweli ndani ya muda wake.
Nikutakie mafanikio mema kwa kila jambo lako.
Ndimi Mjenzi wa Taifa kupitia
Uandishi ( MTU) ; Afisa mipango Benson chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.