Jul 14, 2016
Sababu Zinazofanya Wafanyabiashara Wadogo Kushindwa Kufanikiwa.
Kwa
siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamimiko mengi iwe kwenye vyombo vya
habari au mtaani hasa kwa wafanyabiashara wadogo. Malalamiko hayo yamekuwa
yakihusisha mambo mengi, lakini mojawapo likiwa la wafanyabiashara hawa wadogo
kushindwa kufanya vizuri au kufanikiwa sana kwenye biashara zao.
Hoja
zao mara nyingi wamekuwa wakizielekeza kwenye lawama kulaumu pengine Serikali
au kundi fulani la watu ambalo wao wanaona kama linawabana katika utendaji na
hadi wao kushindwa kufanikiwa. Hoja hizi kwa siku ya leo sitaki kuzijadili hapa
kama ni za kweli au la!
Badala
yake makala haya itakuonyesha mambo mengine kadhaa ya msingi yanayopelekea
wafanyabishara wadogo kushindwa kufanikiwa. Mambo haya kwa sehemu yamekuwa
kikwazo na sababu kubwa inayopelekea wafanyabishara wengi wadogo kushindwa
kupiga hatua na kujikuta wapo palepale.
Hebu
kwa pamoja tuangazie nukta kadhaa zitakazotusaidia kujua ni kwa nini
wafanyabishara wengi wadogo wanashindwa kufanikiwa kwa viwango vya juu.
1.
Ukosefu wa mitaji ya kutosha.
Wafanyabishara
walio wengi wadogo, wakati mwingine wanashindwa kufanikiwa sana kwa sababu ya
mitaji midogo waliyonayo. Mitaji hiyo midogo inakuwa kikwazo cha mafanikio
kutokana na sababu mbalimbali kama tutakavyokwenda kuziona.
Kwanza,
kwa sababu ya mitaji midogo biashara
inakua inashindwa kwenda kwa kasi kama inavyotakiwa iwe, ili kukabiliana na
ushindani mkubwa uliopo sokoni. Hivyo kwa sababu hiyo hupelekea mafanikio
kutokuonekana kwa wafanyabiashara hawa wadogo kwa haraka.
Tengeneza usimamizi mzuri kwenye biashara yako, utafanikiwa. |
Pili,
kwa sababu ya mitaji midogo biashara nyingi za wafanyabiashara wadogo zinakuwa
zinakabiliwa na changamoto mbali kama kodi ya pango, kodi ya mapato na hata
matumizi binafsi.
Kwa
changamoto kama hizi kwa wafanyabiashara wengi walio wadogo huwa si rahisi sana
kukabiliana nazo kwa uhakika, hivyo kupelekea wao kushindwa kufanikiwa kwa
viwango vya juu.
Naamini
katika suala zima la ukosefu wa mitaji umeshawahi kulisikia sana likilalamikiwa
na wafanyabiashara wadogo walio wengi.
Na hii ni moja ya sababu inayowazuia kufanikiwa kwa viwango vya juu.
Nini
kifanyanyike?
Yapo
mengi yanaweza kufanyika ili kukuza mitaji kwa wafanyabiasha wadogo. Mojawapo
ni kujiwekea akiba hata kwa muda mrefu ambayo baadae itatumika kama mtaji wa
kuanzia biashara kubwa.
Pia
wafanyabiashara hawa wanaweza kuungana na kuanzisha mfuko wa pamoja kama mfumo
wa SACCOS au VICOBA ambao utawasaidia kwa urahisi kuweza kukopa pesa
zitakazowasaidia katika suala zima la mitaji.
Hiyo
haitoshi kitu kingine kinachoweza kufanyika ni kwa wao wafanyabiashara kuwa
waangalifu na makini na kodi wanazolipa pamoja na suala zima la matumizi ili
kukuza biashara.
2.
Usimamizi mbovu.
Pia
biashara nyingi ndogo zinashindwa kufanya vizuri kwa sababu ya kuwa na usimamizi
mbovu. Mara nyingi wafanyabiashara wadogo huwa wanakuwa na usimamizi mbovu katika
maeneo mengi kama mauzo, manunuzi, uzalishaji wa bidhaa duni na hata jinsi ya
kuwajali wateja.
Kama
hujanielewa vizuri katika hili nitakupa mfano. Utakuta mtu ana biashara yake ya
aina fulani, lakini biashara hiyo kamuachia mtu mwingine anayeiendesha karibu muda wote na wala hakuna
ufatiliaji ule wa karibu. Kwa usimamizi kama huo inakuwa si rahisi sana kuweza
kufanikiwa.
Hali
kama hizi za usimamizi mbovu kwa maeneo niliyoyataja zipo sana kwenye biashara
nyingi mtaani. Jaribu kutembelea mtaani au sokoni chunguza kile wanachokifanya
baadhi ya wafanyabishara wadogo, kuna wakati unaweza usiamini kile
wanachokifanya lakini ndio ukweli.
Kutokufanikiwa
kwa biashara zao naweza sema ni kama kifo cha kujitakia. Mambo mengi yanafanywa
kimazoea sana hasa jambo kama kumuchukulia mteja mtu wa kawaida kabisa na
kushindwa kumjali.
Kama
unafikiri natania katika hili, tembelea baadhi ya maeneo hapa nchini na
chunguza juu ya hilo, utashangaa jinsi wateja wanavyochuliwa na baadhi ya
wafanyabiashara. Hii ni hali halisi iliyopo katika jamii yetu na ndio chanzo
kikubwa kimojawapo kinachopelekea baadhi ya wafanyabiashara wadogo kushindwa
kufanikiwa kwa viwango vya juu.
Nini
kifanyike?
Kitu
cha kufanya hapa, ni lazima kwa mfanyabiashara yoyote kuwa makini na eneo la
usimamizi wa biashara, hiyo itasaidia sana kukuza biashara yako wakati wote na
kujenga mafanikio makubwa. Bila kufanya hivyo itasumbua sana biashara yako
kukua.
Kwa
leo niishie hapa naomba tukutane tena wiki ijayo na siku kama ya leo katika
sehemu ya pili ya makala haya, kuangalia sababu zingine zinazopelekea
wafanyabiashara wadogo kushindwa kufanikiwa.
Nikutakie
siku njema na mafanikio mema, ila endelea kujifunza na kuwekeza maarifa kupitia
DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.