Jul 22, 2016
Mambo Ya Msingi Unayotakiwa Kujua Kuhusu Ujasiriamali, Kabla Hujaacha Kazi.
Inawezekana
umechoshwa sana na kazi unayoifanya na una hamasa kubwa ya kutaka kuwa
mjasiriamali kwa kujiajiri. Kama hayo ndiyo mawazo yako, kwanza hongera sana,
kwani unachagua njia sahihi itakayokufikisha kwenye ndoto zako za kweli.
Nasema
hivyo kwa sababu, watu wenye mafanikio makubwa duniani ni wajasiriamali na si vinginevyo.
Lakini pamoja na kwamba umekuwa umechagua njia sahihi ya kukufikisha kwenye
ndoto zako, ipo haja ya wewe kujua mambo ya msingi kwenye ujasiriamali kabla
hujaingia huko.
Kwa
kujua mambo hayo itakusaidia wewe kujiwekea misingi imara itakayokufanya
usitetereke. Naamini kwa kusoma makala haya, itakusaidia usiwe na maamuzi ya
kukurupuka ikiwa upo kazini na unataka kuachana na kazi yako na kuingia kwenye
ujasiriamali moja kwa moja.
Sasa
bila kupoteza muda, twende pamoja kujua mambo ya msingi unayotakiwa kujua kuhusu
ujasiriamali, kabla hujaacha kazi.
1. Ujasiriamali unataka kujituma sana.
Hakuna
ubishi katika hili kama umemua kuwa mjasiriamali wa kweli ni lazima kujituma
sana kila siku. Bila kufanya hivyo hutafika kilele cha mafanikio. Kuna wakati
unatakiwa kufanya kazi kuliko kawaida ili kuweza kufikia kilele cha mafanikio
yako.
Kama
upo kazini na unataka kuingia kwenye ujasiriamali huku ukiamini utakuja
kujiachia sana utakuwa unajipoteza. Hivyo, unachotakiwa kujua kama una mpango
wa kuacha kazi na kuingia kwenye ujasiriamali, elewa unaingia kwenye kambi
inayokutaka kujituma sana ili kuweza kufanikiwa.
Kujituma ni muhimu sana kwa mafanikio ya mjasiriamali yeyote. |
2.Ujasiriamali
hautakupa uhuru wote.
Kama
ilivyo kwa mwajiri wako kuna wakati anaweza kukubana, halikadhalika nao ujasiriamali
uko hivyohivyo. Hata kama unafanya kazi ya kwako kuna mambo ambayo huwezi kuwa
huru kwa asilimia zote, kwani ukifanya hivyo utapoteza mengi.
Kuna
kipindi ambacho utatakiwa kuamka asubuhi na mapema. Pia kuna wakati itatakiwa
kujinyima baadhi ya mambo ili kufikia mafanikio yako. Hiyo yote hutokea, kwani
bila kufanya hivyo, utakaa sana kwa muda mrefu eneo moja bila kufanikiwa, kwa
sababu utakuwa kama unazunguka tu.
3.
Ujasiriamali unataka juhudi ya kujifunza kila siku.
Ili
uweze kuwa mjasiriamali bora na mwenye mafanikio ni lazima ukubali kujifunza
kila siku. Kila wakati ubongo wako ni lazima upokee vitu vitakavyokusaidia
kukubadilisha wewe ili ukubaliane na hali yoyote ya shindani.
Mjasiriamali
wa kweli ni yule anayekubali kujifunza na kurekebisha udhaifu wake pale
unapohitajika. Kujifunza huko hakuishii kwenye maandishi peke yake ila mpaka
kwenye vitendo. Binafsi jiulize upo tayarii kujifunza kila siku? Kama ni ndiyo
endelea na safari yako ya ujasiriamali bila kuchoka.
4.
Hutakiwi kukata tamaa mapema.
Unapoamua
kuwa mjasirimali na kuchagua njia yako mwenyewe, kitu cha kimojawapo cha cha
kukijua, ni kwamba hutakiwi kukata tamaa mapema. Kuna wakati mambo na
mipango yako inakuwa inakwenda hovyo sana lakini unatakiwa kuvumilia bila
kuchoka.
Ukiingia
kwenye ujasiriamali halafu huku ukawa una roho ile ya kukata tamaa mapema hutafika
popote. Kwa hiyo ingia kwenye ujasiriamali ukiwa tayari kwa lolote. Ikitokea hasara
vumilia na kisha chukua jukumu la kuweza kusonga mbele bila kukata tamaa.
Hayo
ndiyo mambo ya msingi unayaotakiwa kujifunza kabla hujaingia kwenye
ujasiriamali. Chukua hatua sitahiki za kubadili maisha yako na endelea
kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.