Jul 8, 2016
Pesa Haihitaji Mtaji Kuipata Ni Kweli?
Kila ninapojaribu kushirikisha Rafiki zangu Juu ya dhamira yangu
ya kufanya mambo makubwa maishani kama vile kuwa kati ya mabilionea wakubwa 10
nchini Tanzania, huwa ninapata Jibu la "Huwezi", kwamba
Hayo ninayotaka kuyafanya yanataka mtaji mkubwa sana.
Hata hivyo, nimeapa
kutokata tamaa, kwasababu wanasema "mtu akikwambia Huwezi kufanya
Hili" Maana yake.
anakwambia yeye hawezi. Ukiuliza ni Kwanini wanasema "Haiwezekani" kufanya mambo makubwa, Jibu lao huwa ni moja tu nalo ni "mambo mazuri yanataka mtaji" .
anakwambia yeye hawezi. Ukiuliza ni Kwanini wanasema "Haiwezekani" kufanya mambo makubwa, Jibu lao huwa ni moja tu nalo ni "mambo mazuri yanataka mtaji" .
Suala la kukosa
mtaji limetolewa na watu wengi kama sababu moja Kubwa ya wao kushindwa kujikomboa
kutoka kwenye janga kubwa la umaskini na hasa umaskini wa kipato. Kutokana na
hali hii, watu wengine wemefikia hapo hata ya kuacha kufikiria Kitu Chochote
kinachohusu mafanikio.
Wanasema kila
wakiwaza kufanya Kitu chochote cha maendeleo au uwekezaji wanagundua Kuwa hawana
hata senti moja ya pesa. Kwahiyo, mtaji kwao umekuwa ni kizuizi cha wao
kufikia maisha mazuri. Hali hii ya kujiona hatuna mtaji ni jambo la hisia
zaidi kuliko uhalisia (Ukweli) wenyewe.
Tangu tukiwa wadogo
tumeaminishwa uongo Kuwa "Huwezi kufanya Kitu cha maendeleo Mpaka
upate pesa Kwanza" . Lakini, Baadae imekuja kugundulika Kuwa
suala la kuhitajika pesa na upate pesa ni uongo mtupu.
Tumia akili yako vizuri, itakupa pesa. |
Najua utajiuliza
maswali mengi bila kupata jibu kamili juu ya usemi huu, na hii ni kutokana na
kwamba ukweli, kwa miaka mingi umeweza kusikia na kuambiwa na watu wako wa
Karibu Kuwa "unahitaji Kuwa na pesa ili kupata pesa".
Kwa vyovyote vile
kama umekuwa ukiambiwa maneno haya mara kwa mara, ni wazi kwamba umekuwa
muumini mzuri wa maneno haya. Ni vyema leo ukaanza kuhoji juu yako ya imani
hii ambayo umekuwa nayo kwa miaka mingi na inawezekana imechangia hata kukukwamisha
kufikia mafanikio makubwa ambayo ni haki Yako ya msingi.
Jaribu leo kuipa
akili yako changamoto ya kufikiri nje ya ya mazoea siku zote. Na
ukiendelea kuipa akili yako changamoto ya kufikiri upya, ninapenda
nikushirikishe walau sababu chache za kwanini ni hatari endapo utaendelea
kuamini uongo huu wa kwamba unahitaji kuwa na pesa ili kupata pesa.
Imani ya kwamba ni
lazima kuwa na pesa kwanza ili kupata pesa ina athari lukuki na ni mojawapo ya
kikwazo kikubwa cha sisi kushindwa kufanikiwa, kwanini ni kwa sababu Inaiba
matumaini yako yote.
Kwanini matumaini
ni muhimu? Kwa sababu kama huna pesa na ukachagua kuamini uongo huu kuliko
kuamini kwamba una nguvu. Unajihisi kunaswa kwenye mbio za sakafuni ambazo
uishia ukingoni. Matokeo yake unajihisi na kujisikia Kuwa unahitaji pesa,
ili kujinasua kwenye mtego wa umaskini.
Kwahiyo, unapoona huna
pesa Kwanza unaamua kuendelea na umaskini wako bila kuchukua hatua yoyote kwasababu
wewe unaamini umaskini wako utaondoka tu Siku ukipata pesa - kibaya zaidi ni
kwamba siku Hiyo haijulikani itafika! lini inakufanya kuwa mchungu.
Kama unaamini kuwa
inahitajika pesa kwanza ili kutengeneza pesa, na huna pesa, basi inawezeka
kabisa ukajisikia na kujiona mnyonge mbele ya watu wengine na hatimaye kujiona
mwenye mkosi au bahati Mbaya kuliko watu wengine.
Kwahiyo badala ya
kuwa na hamasa unapoona mafanikio ya wenzako, wewe unaanza kuwachukia walichonacho. Nadhani
mtakubaliana na mimi kuwa hapa Tanzania hali hii ya kuwachukia matajiri bila Sababu
inazidi kuota mizizi kadiri siku zinavyozidi Kwenda mbele.
Na badala ya
kuongeza kujiamini hadi kufikia mafanikio, unaanza kuona mafanikio ya wengine
kama tishio la wewe kupata uhuru wa kipato (fedha). Inakupa kisingizio:
Mojawapo ya jambo
la hatari Kubwa kuliko zote ni kutumia uongo huu kama kisingizio au sababu ya
wewe kushindwa kuboresha na kuongeza elimu yako juu ya uwekezaji, ujasiriamali
na fedha. Badala ya kusonga Mbele na kuchukua kila fursa au mwanya wa kujifunza
Juu ya fursa mbalimbali zilizopo, unaamua kuacha kuendelea.
Saa utakayokubali kwamba "haiitajiki pesa kupata pesa" , ndipo mara moja utaanza kujipa Nguvu, matumaini na la muhimu Zaidi, utaacha kutoa visingizio kama sababu ya wewe kushindwa kuchukua fursa fulani fulani zinazojitokeza kila Siku.
Saa utakayokubali kwamba "haiitajiki pesa kupata pesa" , ndipo mara moja utaanza kujipa Nguvu, matumaini na la muhimu Zaidi, utaacha kutoa visingizio kama sababu ya wewe kushindwa kuchukua fursa fulani fulani zinazojitokeza kila Siku.
Hii ddiyo tofauti
ya watu ambao wamefanikiwa na wale ambao hawajafanikiwa. Ewe mtanzania
mwenzangu, malalamiko juu ya kukosa mtaji hayatakaa yaishe, kwani hakuna watu
maalumu ambao wapo kwaajili ya kukugawia mtaji.
Kupata mafanikio
makubwa kunahitaji ndoto ya maisha mazuri, muda, mipango au mikakati. Kikubwa zaidi,
tunatakiwa kuchambua na kujua tunahitaji nini ili kuishi maisha ya ndoto yetu.
Ukishafahamu nini
hasa mahitaji yako, rahisi kujipanga na kutenda kidogo, huku ukichukua hapo
hatua moja baada ya nyingine. Endapo utaweza kuwa na ndoto na baadae ukatenda
sawa na ukubwa wa ndoto hiyo, basi ujue kuwa siku moja utaweza kufika kwenye
mafanikio makubwa uliyokuwa ukitamani kuyapata.
Mwisho niseme
kwamba endelea kusoma makala mbalimbali hasa zinazopatikana hapa DIRA YAMAFANIKIO kila siku.
Makala hii imeandikwa Cypridion Mushongi wa MAARIFA SHOP BLOG.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.