Oct 25, 2016
Sheria Ya Mafanikio; Nguvu Ya Umakini.
Katika mojawapo ya hatua za mwanadamu kujitambua,
kufahamu sheria hii ni mojawapo kati ya hatua za muhimu sana kwenye kufahamu
maajabu ya ulimwengu. Uelewa wa sheria hii ni faida kubwa sana hasa kwa
wanadamu wanaopenda kujifunza mengi na kuboresha maisha yao katika njia sahihi.
UMAKINI: Ni nguvu kani. Ni kama vile energy. Umakini unapelekea kukusanya ufahamu wako katika
sehemu moja na kupelekea nguvu zako kukusanyika na kuweka nguvu kubwa kwa
pamoja.
Mwalimu
mmoja wa ki-Asia aliwahi kusema kuwa “Umakini ni kama mwanga wa jua, unauona ni wa kawaida lakini
ukiweka lensi mbinuko unaukusanya mwanga ule na kuwasha moto.”
Ni sawa na umakini. Unaweza ukawa umeshawahi kuona
tamaduni za Ki-Asia mtu akiwa anajifunza wanasisitiza mtu kujifunza kwanza
kuuongoza umakini. Mfano Kung-Fu mtu ili aweze kutumia nguvu ya Chi anatakiwa
aweke umakini wake katika nguvu hiyo na attention yake yote iwe hapo ndipo
nguvu hiyo huamka.
Kile unachokizingatia sana, ndicho Unachokipata. |
Umakini una nguvu kubwa sana katika ulimwengu, ukijifunza
chochote kwa umakini unaweza kuwa na uwezo mkubwa sana. Mfano mzuri ni pale
unapoamua kujifunza kitu kama Piano na Guitar, ukiweka akili yako hapo kwenye
Piano utajikuta unaweza kupiga mzunguko ambao hata hukutegemea kama ungeweza
kutengeneza.
Hapo bado hatujaingia katika sheria hii kwa undani. Hapo nilikuwa najaribu kukuelekeza umakini ulivyo.
Sheria hii kiini chake kipo hivi. POPOTE UNAPOELEKEZA UMAKINI WAKO AU FOCUS YAKO PANAKUA. Unapoelekeza
ufahamu wako katika hali fulani, mawazo fulani, ufahamu fulani, utaona ufahamu huo
unakua.
Buddha aliwahi kusema hivi,”Chochote unachokiwekea umakini ni lazima kikue”
Mfano ukiwa unanyanyua vyuma misuli itatumika sana,
halafu baada ya kutumika kunyanyua vyuma hukua na kujaa. Chochote unachokitumia
sana kinakua au kinaboreka ili ukitumia vizuri.
Hii sio sheria ya ufahamu tu bali hii ni sheria ya
ulimwengu, ni sheria ambayo Uasili au ‘Nature’
imekua ikitumia kufanya kazi yake. Mnyama akitumia kiungo fulani sana kiungo
kile kinakua na kuboreka kumsaidia akitumie vyema na kwa zaidi. Kisichowekewa
mtazamo au matumizi kunapotea. Hii nisheria ya asili, na hata akili ni asili hivyo
ipo mpaka kwenye fikra, mawazo au misimamo.
Mfano unaweza kukuta mtu anaamini kitu fulani, ameweka
ufahamu wake wote hapo na anaamini hivyo na huwezi kumbadili hivyo. Naye anaona
anachoamini ni uhalisia kabisa. Kumbe ‘reality’
yake imetokana na kujizoesha kuamini hivyo na kuelekeza ufahamu wake huko
mwishowe anajikuta anaamini hivyo na yeye mwenyewe hajui hilo kwani hafahamu
kuwa kuna sheria kama hii duniani.
Kufahamu ufahamu huu itakusaidia kuuliza unachokiamini.
Je ni kweli ‘reality’ yako imetokana
na umejizoesha kuamini hivyo au kufahamu hivyo na kupelekea wewe leo hii kuona
hivyo au ni reality?
Wewe ni ufahamu wako, wewe unajitambua kupitia ufahamu
wako, Hakuna kitu kingekwepo bila ufahamu. Ufahamu ni kinachouona ulimwengu.
Kwa sasa ufahamu wako unategemea milango yako ya ufahamu (macho, pua, ulimi,
ngozi, masikio) kuutazama ulimwengu.
Ulimwengu huu ni ulimwengu wa milango ya ufahamu. Shida
unazoziona, raha unazoziona zote unazihukumu kwa kusema hiki ni shida na hiki
ni raha kwa kutumia milango yako ya ufahamu na sio ufahamu wenyewe.
Ungezaliwa katika ulimwengu unaoamini maumivu ni raha
ungeona ni raha kwani ufahamu wako hauna uhusiano na kitu au hali yenyewe.
Ufahamu unaweza kubadilika na kupelekea hali kuonekana tofauti kwani ni ufahamu
unaohukumu hali na sio hali yenyewe.
Kuelewa sheria hii utajifunza kuwa kuna umuhimu wa kuwa
makini na unachokiamini, kuwa makini na kinachoendelea katika akili yako, kuwa
makini na matumizi ya hisia zako, kuwa makini na kutazama mawazo yako, kuwa
makini kwa kutazama imani na maamuzi yako halafu linganisha na maisha yako ya
nje. Kuelewa sheria hii ni kuelewa kuwa ulimwengu wa ndani yetu unaumba
ulimwengu wa nje.
Watu walioweza kujitambua na kufahamu sheria hii waliweza
kujitahidi kuongoza fikra zao kwa kuumba uhalisia wao. Mtu makini ni mwenye
ufahamu kuwa yeye na mchango mkubwa katika kubadili maisha yake na sio kingine.
Haijalishi unaishi katika hali gani, ni kubadili mtazamo wako na KUUTAZAMA MTAZAMO WAKO.
Una maumivu kwenye bega. Unaweza ukaamua kuweka fikra
yako katika kuwaza jinsi ulivyo na maumivu katika bega na kukosa raha au
unaweza kuweka umakini wako kwa sehemu nyingine za mwili ambazo ni nzima na
kushukuru kwa kila jambo. Lakini kuna ambao wataelekeza akili yao kwenye
maumivu na wengine wanakata taamaa kabisa na kuona hatapona.
Unaweza ukahisi unaumwa ugonjwa fulani na kuona unaanza
kuumwa ugonjwa huo. Upo ushahidi wa kisayansi kuwa kuna magonjwa yanachangiwa
na akili. Kuna dalili nyingine zimetokana na mtu kuwaza ugonjwa sana na anaanza
kuona dalili.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA APOLINARY
MACHA WA JITAMBUE SASA.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.