Mar 31, 2017
Toka Kwenye Vifungo Hivi,..Utengeneze Zaidi Mafanikio.
Vipo vifungo vingi ambavyo vinaweza kukufunga na
kukupotezea mafanikio yako. Vifungo vingine unavijua na vingine unaweza ukawa
huvijui. Kwa mfano;-
Acha kujiweka kwenye vifungo vya kidini na kuamini
utajiri mkubwa ni dhambi. Kumbuka, mafanikio hayana uhusiano moja kwa moja na
kutenda mabaya.
Acha kuamini umaskini ndio ni kitu kizuri kwako.
Hivyo ukashindwa kuweka juhudi zako zote kwa kisingizio cha kwamba ukiwa
maskini ni sawa kwako.
Acha kuamini ukiwa na pesa nyingi ndio ushetani.
Utajikwamisha sana wewe mwenyewe kufikia mafanikio yako bila kujijua ukiwa upo
kwenye kifungo cha dini.
Acha kuamini kwamba Mungu atakusaidia kila kitu, hata kama umebweteka na wala hujitumi sana yaani huweki juhudi sana, ndio maana amekupa akili ufikirie na vingine.
Acha kutumia uvivu wako kutumia kama kisingizo
ukiamini hio ndiyo imani sahihi.. Kama kuna kazi unayotakiwa kufanya, fanya
kweli. acha kuendekeza uvivu unaomba kazi kwenye kampuni moja halafu unamlaumu
Mungu. Ukiona uko hivyo ujue kabisa upo kwenye kifungo..
Toka kwenye kila aina ya vifungo ambavyo unaona
vinakukwamisha kufanikiwa sana kwenye maisha yako, kuwa huru ili utengeneze
mafanikio yako.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio
makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Mshauri wa
mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog,
dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano;
+255 628 929 816, +255 713 048 035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Mar 30, 2017
Nufaika Na Kilimo Bora Cha Matango.
Habari
rafiki na karibu sana katika safu hii ya makala za kilimo. Katika somo
liliopita tuliangalia juu ya umuhimu wa kutumia mbegu bora na faida zake. Sasa
leo tutaangalia kilimo cha matango kwa kutumia mbegu bora inayoitwa Hybrid
Cucumber YETU F1 ambayo utaanza kuvuna baada ya siku 45-50 kutoka kupandwa
kwake.
YETU F1 ni mbegu chotara
ambayo ina umbo zuri na hupendwa sana na walaji. Kiasi cha mbegu 300g(Gramu
300) huweza kutosha ekari moja ambayo utainununua kwa shilingi laki
tatu(300,000/=) za kitanzania.
UANDAAJI
WA SHAMBA.
Chagua sehemu iliyo
nzuri,na ukipata sehumu ya tifutifu iliyo changanyikana na mchanga itakuwa
vizuri zaidi.
Pia ukipata sehemu yenye
udongo mzito lakini usiwe una tuamisha maji.
Lima shamba na hakikisha
umelisawazisha vizuri(yaani hallowing),baada yapo panga matuta yako.
KIASI
CHA MBEGU.
Gramu 300 zenye kiasi ya
YETU F1 kinatosha kupanda eneo la ekari moja(100m×40m).
Na hii aina ya mbegu 1g
ina mbegu 30-40.
KUPANDA.
Kabla ya kupanda hakikisha
una mbolea ya kupandia kama DAP ikichanganywa na Agrigrow starter yenye madini
mengi ya phosphorus.
Panda mbegu kwa nafasi
150cm×45cm mbegu mbili mbili kila shimo.
Na hii mbegu huota baada
ya siku tatu hadi tano,hivyo huchukua muda mfupi kuota.
Mara baada ya kuota tumia
mbolea ya majani Agrigrow starter ambayo itaimarisha mizizi hivyo kurahisisha
mmea kupata chakula kutoka kwenye udongo.
Huu mmea huchukua muda
mfupi kukua hivyo hivyo mara baada ya kuota baada ya siku chache tumia mbolea
ya yara mila winner kukuzia.
Pia yatakavyo anza
kutambaa tumia mbolea ya majani Agrigrow vegetative hii itafanya yawe na matawi
mengi hivyo kuongeza uzalishaji.
Maua yakianza kuonekana
tuu,tumia mbolea ya majani Agrigrow flowering and fruiting,hii itasaidia maua
kuto pukutika,pia itaboresha muonekano wa tunda,itafanya maua yawe mengi hivyo
na kupatikana kwa matunda mengi.
Epuka kumwagilia maji
jioni sana kwa kuwa unaweza ukasababisha magonjwa kama ya fangasi kwa mmea.
Pia epuka kupulizia dawa
pale wadudu wa muhimu wawapo shambani(kama nyuki)kwani kutafanya kupunguza kwa
mazao shambani.
DAWA
ZA WADUDU
Ukiwa ni mkulima unayelima
kitaalamu na unayetaka mafanikio kupitia kilimo yakufaa kuwa na dawa za wadudu
zifuatazo.
1. Prosper 720EC yenye mchanganyiko wa sumu
mbili(Profenofos 600g/L +Cypermethrin 120g/L),hii ni dawa ambayo ina ua wadudu
katika wigo mpana(yaani ni broad spectrum). Na mchanganyiko wake ni 2mls au 2cc
kwa maji lita 1.
2. Avirmec 1.8EC (Yenye sumu ya Abamectin) hii
itauwa utitili shambani wa aina yote,na mchanganyiko wake ni 7mls kwa lita 20
za maji.
3. Dawa ya ukungu Agrilax 72WP,hasa kwa
nyakati za baridi,hii ni dawa ambayo ina mchanganyiko ya wa sumu mbili yaani
Mancozeb na Metalaxyl,ambayo mancozeb kwa ajiri ya kukinga(Preventive) na metalaxyl kwa kutibu(Curative).
Hivyo Agrilax hukinga na
kutibu magonjwa yote yatokanayo na fangasi(yaani fungicide diseases).
MAVUNO.
Matango(YETU F1) huwa
tayari baada ya siku 45-50 kutoka siku ya kupandwa.
Je utakuwa na miche
mingapi kwa ekari moja? Kwa kawaida miche hufikia 11850.
Tuliangalia katika somo la
matikiti kanuni ya kutafuta idadi ya miche yaani Plant population(I.e PP)
Plant population(PP) =(Area/Spacing)
×no of seeds per hole.
Kwa mfano:-Area(A)=1acre=4000m square.
-Spacing (SP)=150cm×45cm
or 1.5m×0.45m.
-No of seeds to be sown
per hole=2seeds.
-Required: Plant
population (PP)
Then,from the formula;-
PP=((A/SP))×no of seeds per hole.
PP=((4000)÷(1.5×0.45))×2.
PP=(4000÷0.675)×2
PP=5925×2
PP=11,850Plants/acre
Therefore, there will be
11,850plants per acre.
Na haya matango kwa
matunzo mazuri, huwa na matunda mengi sana ambayo yataweza kufikisha viroba 150
kwa makadilio ya chini kabisa ambayo
utauza kwa sh 70,000/= kwa kiroba kimoja kwa bei ya chini kabisa.
Viroba 150@sh 70,000 ni sh
10,500,000/= kwa makadilio ya chini na hyo pesa ni kwa ekari moja tu.
Na hayo mapato ni kwa wale
ambao wamepanda bila kuwekea nguzo(Non trellised)
Kwa wale watakao wekea
nguzo(Trellised) wataweza kutumia eneo dogo na kupata mavuno mengi zaidi.
Na hivi ndivyo kilimo
biashara kinavyotakiwa kuendeshwa(lima eneo dogo vuna mazao mengi)
Hebu tuangalie kwa wale
watakao wekea nguzo(Trellised Cucumber)
Shamba la ekari moja(4000m
square), Spacing =80cm×40cm(0,8m×0.4m),number of seeds per hole =1seed,Plant
population (PP)=?
Therefore:-
PP=(Area/spacing) × no of
seeds per hole.
PP=((4000)÷(0.8×0.4))×1.
PP=4000÷0.32
PP=12,500Plants/acre
-Na kwa kuiwekekea
nguzo(Trellised cucumber) huweza kuzaa matunda mengi zaidi kuliko bila
kuyawekea nguzo.
-Kwa kuyawekea nguzo mche
mmoja huweza kuzaa matunda 15-30 kwa mche mmoja.
-Tuchukulie kwa makadilio
madogo kabisa mche mmoja umezaa matunda 15
Kwa hiyo basi;-
1plant=15fruits
12500plants=x?
By crossing:
x=12500×15
x=187,500fruits/plants
-Kwa hiyo utakuwa na jumla
ya matunda 187,500 kwa ekari moja
-Kwa kuuza kwa bei ndogo
kabisa ya sh 50 kwa tunda moja,utakuwa na jumla ya fedha =187,500×50= Tzs
9,375,000/=
-Kwa watakao uza kwa sh
100 kwa tunda moja,basi utakuwa na jumla ya pesa 187,500×100=18,750,000/=.
Kazi kwako kwa wewe
mkulima unaye taka mafanikio,tumia mbegu bora (Hybrid seeds) zikuletee
mafanikio.
Wako mtaalamu wa kilimo.
Boniface
L Pwele,
Kwa
mawasiliano zaidi piga simu namba 0762567628 au tuma ujumbe kwa barua pepe
blugahno95@gmail.com
Mar 29, 2017
Hawa Ndio Wanawake Waliofanikiwa Sana Kwenye Ujasiriamali.
Siku zote tunasema na tutaendelea kusema kwamba mafanikio hayana rangi, kabila, umri
wala jinsia, ukiamua kufanikiwa kwa vyovyote vile ulivyo hata uwe katika kona
gani ya dunia utafanikiwa tu, kwa sababu umeamua iwe hivyo kwako na itakuwa.
Nasema hivyo kwa sababu, mara nyingi watu wengi linapokuja suala
la mafanikio huwa kuna bagua bagua nyingi sana kwa upande wao. Kwa mfano, mtu
anakwambia kabisa huwezi kufanikiwa kwa sababu wewe umri wako ni mdogo au
huwezi kufanikiwa sana kwa sababu wewe ni mwanamke.
Ukiangalia ukweli wa mambo ulivyo kwenye mafanikio hauko hivyo,
kwa vyovyote vile ulivyo unaweza ukafanikiwa na kutengeneza mafanikio makubwa
bila kujali unaishi nchi gani au bila kujali wewe ni mtu wa jinsia gani yaani
mwanaume au mwanamke.
Kutilia mkazo katika hilo na ili unielewe vizuri ninachosema
hapa, leo kupitia makala haya tuangalie baadhi ya wanawake ambao wamepata
mafanikio makubwa sana duniani kupitia ujasiriamali, ingawa kuna wakati pengine
walibezwa na kukejeliwa sana kwamba hawawezi kufika popote.
1. Oprah Winfrey
Pamoja na kwamba Oprah kwa sasa ameshaacha mambo ya utangazaji
kwenye televisheni lakini ni moja ya wanawake ambao wamefanikiwa sana na kuwa
na pesa nyingi kutokana na kujituma na kuwekeza kadri alivyoweza hadi kufikia
mafanikio aliyonayo sasa.
Yeye kama yeye kupitia kituo chake cha ‘Oprah Winfrey leadership
academy’amefanikiwa kuwasaidia watoto wengi wa kike, pia ni jambo
ambalo limekuwa llikimuungizia pesa za kutosha. Ameidhirihishia dunia kwamba
mafanikio hayana jinsia ni kujituma tu.
2. Folorunsho Alakija
Alakija ni moja
pia ya wanawake wenye pesa na tajiri sana nchini Nigeria. Biashara zake zilizompa
utajiri ni biashara ya mapambo na mafuta. Kwa sasa Alikija anakadiriwa
kufikia utajiri wa dola za kimarekani billion 1. 6.
Mpaka hapo unaona
ni kwa jinsi gani ambavyo naye amejitahidi kuweka juhudi nyingi za kufikia
mafanikio yake aliyonayo katika kile anachokifanya. Hiyo yote inaonyesha juhudi
ikiwekwa popote hakuna kinachoshindikana.
3. Wang Laichun
Laichun pia inasemekana
ni moja ya mabillionea wa kichina ambapo utajiri wake alionao ambao kwa sasa unafikia
dola za kimarekai bilini 1.67, umetokana na juhudi zake binafsi na sio kurithi.
Biashara
iliyompaisha hadi kufika huko aliko sasa ni biashara ya vifaa vya umeme ambavyo
anavisambaza na amekuwa mojawapo ya wanawake matajiri sana duniani.
4. Debbie Fields
Pia katika
wanawake wajasiriamali na wenye pesa huwezi kumsahau mwanadada huyu Debbie
fields katika ulimwengu wa mafanikio. Ni moja ya wanawake kweli waliofanikiwa
haswaa.
Utajiri wake hasa
ni wa nini? Huu ni mwandada anayejihusisha na kutengeneza vyakula vya aina tofauti
tofauti vyenye mfumo kama wa keki. Ambapo kwa sasa anasambaza vyakula vyake
zaidi ya nchi kumi duniani.
Mafanikio katika
maisha yako yanawezekana. Huna haja ya kuwa na sababu kwamba mimi sina hiki au
kile au mimi kwa sababu ni jinsia hii siwezi kufanikiwa, weka juhudi, matokeo
utayaona.
Endelea kujifunza
kupitia dirayamafanikio.blogspt.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
Mar 27, 2017
Namna Unavyoweza Kugeuza Makosa Yako Na Kuwa Mafanikio.
Makosa katika safari yoyote
ya mafanikio ni kitu ambacho
hakikwepeki. Bila shaka wewe na mimi tumeshawahi kukosea katika maeneo kadhaa
ya maisha yetu. Kukosea huko kulitufanya pengine tujute au kuumia kabisa na
kujiona kama vile hatufai.
Je, kitu cha kujiuliza hivi
ndivyo tulivyotakiwa kuyachukulia makosa haya na kujihukumu vya kutosha. Jibu
rahisi hapa ni hapana. Hatukuwa na sababu ya kujihukumu sana kutokana na makosa
yetu, zaidi ya kugeuza makosa hayo na kuwa ushindi.
Na ni kwa namna gani
tunaweza kugeuza makosa yetu kuwa ushindi?
1.
Jifunze kutokana na makosa hayo.
Ili
uweze kuwa mshindi na kugeuza makosa yako kuwa ushindi, ni lazima kujifunza
kutokana na makosa ambayo unayafanya. Kama hujifunzi, hakuna utachokuwa
unafanya, zaidi utaendelea kukosea na kubaki hapo. Wanaojifunza na kuchukua
hatua ndio wanaofanikiwa.
Kukosea
kwako hakuna shida sana, shida inakuja pale unaposhindwa kujifunza. Ni muhimu
kujifunza kutokana na makosa yako na kurekebisha pale ulipokosea. Kwa kadri
utakavozidi kujifunza utajikuta makosa yako yanageuka kuwa ngazi ya
kukufanikisha badala ya vizuizi.
USHINDI NI LAZIMA |
2. Chukua jukumu la kuwajibika.
Hautaweza
kwenda popote wala kupata mafanikio, ikiwa utakuwa ni mtu wa kulaumu wengine
kwamba ndio waliosababisha ukakosea. Mtu wa kwanza kuwajibika kwa makosa
uliyofanya ni wewe. Acha kulaumu wengine, utakuwa unapoteza wako bure. Wajibika
kwanza wewe.
Unapochukua
jukumu la kuwajibika elewa wewe ndiye kiongozi wa maisha yako, hivyo kama kuna
makosa yamefanyika kwa sehemu una mchngo wa kusababisha makosa hayo kujitokeza.
Badala ya kulaumu, tafuta nini kilichokufanya ukakosea, kirekebishe baada ya
hapo endelea na safari yko.
3. Jifunze kutokana na uzoefu.
Linaweza
likawa ni jambo linalokuuma sana, hasa pale unapokosea. Lakini nina uhakika
pamoja na maumivu hayo kuna kitu ambacho unaweza ukajifunza hapo. Kujifunza
huko, huo ndio uzoefu ninaotaka uuchukue hapo na kuugeuza kuwa ushindi pengine
yanapotokea makosa kama hayo kwa baadae.
Acha
kuishia kuumia na kulalamika na ukabaki hivyo, utakuwa hufanyi kitu. Utumie
uzoefu kukusaidia kufika kwenye kilele cha mafanikio. Mara nyingi kwenye
kipindi cha kukosea unaweza ukakiona ni cha mateso na maumivu. Lakini , kumbuka
siku zote uzoefu ni mwalimu mzuri w mafanikio yako.
4. Badili tabia zako.
Inawezekana
ukawa unashindwa na unaendelea kufanya makosa kwa sababu ya tabia ulizonazo.
Ili uweze kutoka hapo na kuepuka makosa huna namna nyingine zaidi ya wewe
kuweza kubadili tabia zako mara moja. Ukiweza kubadili tabia zako hizo zinazokurudisha
nyuma, basi yapo makosa ambayo unayarudia kuyafanya utayaepuka moja kwa moja na
kuwa mshindi.
Hivi ndivyo unavyoweza
kugeuza kushindwa kwako na kuwa ushindi wa mafanikio. Acha kuhuzunika na
kusononeka sana. Fanyia kazi mambo hayo yatakuwa msaada mkubwa kwako sana.
Endelea
kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO na kumbuka tupo pamoja.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako
wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Mar 25, 2017
Habari Njema Kwa Wafugaji Wote Wa Kuku.
Habari njema kwa wafugaji wote wa kuku. Dezhou Runde Metal Products, Ltd tuliopo Tanga,
Tanzania ni wauzaji wa mashine za
kuangulia vifaranga (Incubators) kwa bei
nafuu sawa na kiwandani.
Pia hio haitoshi tunauza na vifaa vingine ambavyo vinatumika
kwenye ufugaji wa kuku kama Drinker, Nipple drinker, Auto drinker, chick auto
drinker, cages na vinginevyo vingi kulingana na mahitaji yako.
Kama una hitaji mashine bora za kuangulia vifaranga kwa muda
mfupi na bei nafuu, tafadhari wasiliana nasi kwa kutupigia simu moja kwa moja
kwenda 0767 04 80 35.
Hata hivyo pia ukiona Tangazo hili, mwambie na mwingine, asiikose fursa hii.
WOTE MNAKARIBISHWA NA TUPO KWA AJILI
YAKO KWA KUKUPA HUDUMA BORA NA YA FAIDA.
Mar 24, 2017
Kinachokupotezea Mafanikio Yako Sana Ni Hiki Hapa.
Acha
kujidanganya kwamba unatafuta mafanikio wakati hata unashindwa kubadili tabia
ndogo ndogo za kukupeleka kwenye mafanikio yako, huo utakuwa ni uongo mkubwa.
Acha
kuendelea kujidanganya kwamba kesho yako itakuwa bora wakati hata leo hii
hufanyi kitu cha uhakika cha kubadilisha maisha yako. Maisha yako kiukweli hayataweza
kubadilika.
Acha
kuendelea kulaumu watu wengine kwa maisha yako kuendelea kuwa mabaya. Mtu wa
kwanza unayetakiwa kumlaumu ni wewe mwenyewe hasa kutokana na mienendo na tabia
zako.
Sio
kwa sababu maisha ni magumu kwa sasa, basi unachanganyikiwa na kuona kila kitu
hakifai kwako na kwa wengine. Maisha yanahitaji sana utulivu wa hali ya juu ili
ufanikiwe, unatakiwa ujue hili.
Kama
unaona maisha yako yamekweda hovyo, jichunguze, panga mipango yako upya kwa umakini
na utulivu na hata wala usikurupuke katika hilo. Utulivu ni kitu cha msingi
sana ambacho kinaweza kukupa mafanikio.
Tabia
mbaya na mienendo mibovu ulionayo hiyo ndiyo inaokufanya au naweza kusema
inaharibu maisha yako moja kwa moja. Angalia hilo halafu utaujua ukweli ambao
ninakwambia.
Kila
wakati jiulize, unaendelea kukua kimafanikio, au unarudi nyuma? Kama unarudi
nyuma, kama nilivyosema kuwa makini sana na tabia na mienendo yako, hiyo ndiyo
inayokukwamisha.
Kama
umefika wakati kwako wa kusema uko 'serious' na mafanikio yako, basi hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kubadilisha tabia zako na kujenga tabia
zitakazokuwezesha kufanikiwa.
Kumbuka
pia kinachokupotezea mafanikio yako, ni tabia ambazo unazo na unazibeba kila
wakati, hicho ndicho kitu kikubwa kinachokupotezea mafanikio yako ya leo na
kesho.
Nikutakie
siku njema na kila kheri,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
Mar 23, 2017
Hatua Nne Za Kufikia Malengo Yako Kwa Uhakika Mkubwa.
Kila
mtu katika maisha yake ana malengo maalumu ambayo anakuwa amejiwekea na anakuwa
ana waza kwamba kwa namna yoyote ni lazima baada ya muda fulani malengo yake
yatatimia.
Pia
sina shaka na wewe, naamini umejifunza kwa sehemu namna au mbinu ambazo mtu
anaweza akazitumia kuweza kufikia malengo yake. Lakini leo hii, si vibaya kama
nitakung’ata sikio kukumbushia tena jinsi unavyoweza kufikia malengo yako kwa
uhakika mkubwa.
Najua
kila mtu ana njia zake na mbinu ambazo anazitumia kuweza kufikia malengo yoyote
katika maisha. Leo hii, naomba nikuonyeshe mbinu ambazo zinatumiwa karibu na
watu wote wenye mafanikio makubwa kufikia malengo yao kila wakati.
Andika malengo yako chini.
Yaweke
malengo yako kwenye karatasii ili yawe rahisi kuyaona. Yawe ni malengo mahsusi
ambayo utekelezaji wake unafikika na uwe tayari umejiwekea tarehe maalumu ya kuyafikia.
Hio ndiyo sifa ya malengo unayotakiwa kuwa nayo.
Anza kuweka mipango.
Umesha
andika malengo yako tayari. Hatua inayofuata ni kwa wewe sasa, kuweka mipango
ya kufanya. Kumbuka unapofanya jambo unapata nguvu zaidi ya kuweza
kulifanikisha kuliko ukitulia. Hivyo ni lazima mipango yako iwe hai na ya kiutekelezaji.
Lipa gharama.
Kubali
kulipia kila gharama inayohitajika ili kufikia malengo yako. Gharama hizo
zinaweza zikawa ni muda au nidhamu binafsi. Lakini gharama yoyote fanya kila
ufanyalo hakikisha unailipa. Kama utakwepa kulipa gharama yoyote ile naomba
nikwambie sahau mafanikio.
Yapitie malengo yako kila siku.
Hakuna
namna ya nyingine ya kuwa mshindi zaidi ya wewe kukomaa kupitia malengo yako
kila siku. Unapopitia malengo yako kila siku yanakupa nguvu na hamasa kubwa ya
kuona ni jinsi gani yanawezekana na unaweza kuyafikia.
Hivyo
ndivyo, unaweza kutimiza malengo kwa kufuata hizo hatua rahisi kabisa.
Nikutakie
siku njema na kila kheri,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
Mar 22, 2017
Haya Ndiyo Mahusiano Yaliyopo Kati Ya Mafanikio Na Afya Yako.
Je kuna mtu ambaye hapendi mafanikio katika maisha yake? Kila mtu ukimuuliza atakwambia ana taka mafanikio, maendeleo na maisha bora.
Lakini ulisha wahi kujiuliza afya yako ina husiana vipi na
mafanikio unayoyahitaji? Je una weza kufanikiwa bila kuwa na afya bora na
imara? Haya ni baadhi ya maswali ya msingi unayopaswa kuji uliza kabla huja
endelea kusoma makala hii.
Tabia zetu zimekua zikiathiri moja kwa moja afya yetu hivyo
kupelekea kushindwa kutimiza malengo tunayo jiwekea katika maisha yetu. Tabia
hizo ni vitu ambavyo tunaviendekeza na kuvichukulia kama sehemu ya maisha yetu
bila kujua madhara yake baadae.
Tofauti kati ya bustani na msitu ni matunzo, bustani hutunzwa
hivyo hustawi na kupendeza na kuifanya izae matunda mazuri yapendezayo. Hivyo
mwili nao unahitaji matunzo ili uweze kukupa matunda unayo tamani.
TABIA ZINAZO ATHIRI AFYA ZETU
1. Ulaji Mbaya Wa Chakula.
Hapa ndipo watu wengi wana angukia, kuna makundi mawili ya
ulaji mbaya
Ratiba mbaya ya kula
Watu wengi hawana ratiba nzuri ya kula na wengi huchelewa kula
kwa madai kazi zina watinga. Lakini ukweli ni kuwa ukichelewa kula una ua mwili
wako taratibu, magonjwa kama vidonda vya tumbo yamekua yaki wasumbua watu wengi
kutokana na kushindwa kula kwa wakati.
Kula usiku sana hupelekea mwili kutunza mafuta na kuongezeka
uzito. Kupoteza uwezo wa kufikiri,na kusinyaa kwa ubongo kutokana na kukosa cha
nguvu kwa muda mrefu.
Kula vyakula hatarishi
Ulaji wa vyakula vya sukari kwa wingi,chumvi na kahawa hupelekea
magonjwa kama shinikizo la damu na kusukari pia kuongezeka uzito kupunguza
uwezo wa moyo kufanya kazi na kuathiri uwezo wa kufikiri.
CHAKULA BORA NI MAFUTA YA UBONGO.
CHAKULA BORA NI MAFUTA YA UBONGO.
Kula chakula bora kwa afya yako. |
2. Msongo wa mawazo.
Ndio msongo wa mawazo, kuwaza ni kitu cha kawaida kwa mwanadamu.
Lakini kuwaza kupitiliza husababisha matatizo makubwa bila kujijua.
Vitu kama kufanya kazi kupitiliza, majibizano,kukosa muda wa kutosha kupumzika, kukataliwa huweza kusabisha msongo wa mawazo.nakuleta madhara kama kupoteza mwelekeo, kushindwa kufanya maamuzi,kupoteza umakini,kushindwa kuhusiana na watu vizuri.
Vitu kama kufanya kazi kupitiliza, majibizano,kukosa muda wa kutosha kupumzika, kukataliwa huweza kusabisha msongo wa mawazo.nakuleta madhara kama kupoteza mwelekeo, kushindwa kufanya maamuzi,kupoteza umakini,kushindwa kuhusiana na watu vizuri.
3. Kukosa Muda mzuri wa Kulala.
Uta shangaa kulala? lakini ukweli unabaki pale pale,
kulala kwa wakati. Una lala saa kumi na kuamka saa kumi na moja hii ni moja
kati ya tabia hatarishi sana kwa afya zetu. Wanasayansi wana shauri kulala kwa
afya ni masaa 6-7.
Magonjwa ya figo,moyo,uzito ulio pitiliza,kisukari na
shinikizo la damu yana weza kusababishwa na kukosa muda wa kutosha kulala.
4. Tabia binafsi.
Hizi ni zile tabia ambazo mtu huzi anzisha na baadae
kushidwa kuzi himili na huanza kumuendesha, tabia kama ulevi,kuvuta
sigara,madawa ya kulevya,ngono zembe,huanza taratibu na baadae hugharimu afya
yako.
Watu wotewalio fanikiwa hujali afya zao kuliko mali walizo
nazo, lakini maskini hutumia kidogo alicho nacho kuharibu afya yake bila kujua,
na huku aki hitaji kufanikiwa.
HUWEZI KUPATA MAENDELEO KAMA HUTA ITUNZA AFYA YAKO.
ITUNZE AFYA YAKO KWA MAENDELEO YAKO.
ITUNZE AFYA YAKO KWA MAENDELEO YAKO.
Makala imeandikwa na Dr.Julius Kimaro,
0745524031.
Mar 21, 2017
Utajiri Na Umaskini Unatokana Na Nini?
Kila mmoja ninaamini anao
uwezo wa kuwa tajiri, isipokuwa binadamu huwa na fikra tofauti juu ya mambo
yale yale. Kitu kilichoko akilini mwako ndicho kinacho leta tofauti ya hali ya
maisha unayoishi kwa sasa .
Maana yake ni kwamba, jinsi
ulivyo wewe ni zao la yale yote unayofikiri kila siku. Watu waliofanikiwa kuwa
matajiri, wana mambo kama 5 ambayo wameyafanya kuwa kama kanuni zao za kudumu
na kwakuwa ni kanuni, wao huzitekeleza na kuziishi kila siku.
Kanuni zenyewe ni....
Namba moja: Matajiri
wana fikra vichwani mwao kwamba kila kitu duniani kipo kwa wingi. Lakini
maskini wao hufikiri kwamba kila kitu duniani hakitoshi. Kwa maneno mengine ni
kwamba, masikini kila wakati anafikiria uhaba, jambo ambalo umletea wasiwasi na
kumnyima uwezo na moyo wa kusubiri mambo makubwa yatokee kwake.
Watu wote tuko duniani hapa hapa, lakini tunatofautiana sana utajiri tulionao.
Kitu kimojawapo kinachosababisha utofauti huu mkubwa ni jinsi tunavyofikiri na
mtazamo tulionao juu ya ukweli wa rasilimali zilizopo hapa duniani.
Matajiri wao uamini katika ukweli kwamba fikra za binadamu ndizo uzaa vitendo
na vitendo uzaa matokeo, ambayo ni pamoja na pesa. Kwa vyovyote vile ukifikiria
kupata pesa kiasi fulani lazima ufikirie kitu cha kufanya ambacho ukikifanya
kitakuletea pesa zaidi ya ile uliyokuwa unahitaji.
Uzuri wa matajiri ni kwamba,
wao hufikiria na kuiona pesa kwenye akili yao tayari kabla ya kuishika au
kuipata. Maskini wao hufikiria na kuona uhaba ndani ya akili yao kabla ya
kupata pesa.
Kwakuwa maskini wao hufikiria uhaba kwanza kabla ya kitu kingine, ndiyo maana uishia kufanya kazi ndogo ndogo na vitu vidogo vidogo, ambavyo mwisho wake umpatia pesa kidogo (haba) zinazolingana na uhaba alioufikiria mwanzoni kwenye akili yake. Kwa maana nyingine watu maskini pesa kidogo wapatayo, huifikiria mapema kabla hata ya kuanza kazi ya kuitafuta.
Namba mbili: Matajiri wao huona fursa mbele yao, wakati maskini wao uona matatizo tu mbele yao.
Mfano mwalimu mmoja alifundisha wanafunzi darasani, lakini mwisho wake wanafunzi wengi wakashindwa vibaya sana wakalazimika kukaririri darasa. Mwalimu huyu alianza kulalamika na kusononeka. Mara akafikiria kuwa darasa hilo yawezekana lina wanafunzi ambao hawana uelewa wowote ni wabovu wa kufikiri. Mwalimu mwingine aliposikia na kujionea hali halisi ya kushindwa kwa wanafunzi hawa, akaona fursa.
Baada ya kuona fursa hiyo, akatunga kitabu cha mwongozo wa “jinsi ya kufauru mtihani na akatoa fursa kwa wanafunzi kuweza kulipia na kupata masomo ya ziada. Kitabu pamoja na masomo ya ziada kwa wanafunzi ni vitu vilivyompatia pesa nyingi wakati mwalimu huyo mwingine aliendelea kulalamika huku akiandamwa na umaskini wake kama kawaida. Walimu hawa wawili wanawakilisha makundi mawili ya watu—maskini na tajiri ambao tofauti zao ni fikra tofauti kwa kitu kile kile.
Namba tatu: Matajiri wao hununua vitegauchumi ambavyo baadae uwatengenezea faida na faida hii wao huiwekeza tena na tena. Kitendo hiki cha kurudisha faida kwenye vitegauchumi kila mara, uwapa fursa ya kuifanya faida waliyoipata kuzaa pesa nyingine zaidi.
Namba nne: Matajiri wao hujali sana kuwa na mtandao wa watu waliofanikiwa. Maskini wao upenda kukaa peke yao, kufanya kazi peke yao Matajiri huona umuhimu sana wa kuwa na watu waliofanikiwa.
Kwakuwa maskini wao hufikiria uhaba kwanza kabla ya kitu kingine, ndiyo maana uishia kufanya kazi ndogo ndogo na vitu vidogo vidogo, ambavyo mwisho wake umpatia pesa kidogo (haba) zinazolingana na uhaba alioufikiria mwanzoni kwenye akili yake. Kwa maana nyingine watu maskini pesa kidogo wapatayo, huifikiria mapema kabla hata ya kuanza kazi ya kuitafuta.
Namba mbili: Matajiri wao huona fursa mbele yao, wakati maskini wao uona matatizo tu mbele yao.
Mfano mwalimu mmoja alifundisha wanafunzi darasani, lakini mwisho wake wanafunzi wengi wakashindwa vibaya sana wakalazimika kukaririri darasa. Mwalimu huyu alianza kulalamika na kusononeka. Mara akafikiria kuwa darasa hilo yawezekana lina wanafunzi ambao hawana uelewa wowote ni wabovu wa kufikiri. Mwalimu mwingine aliposikia na kujionea hali halisi ya kushindwa kwa wanafunzi hawa, akaona fursa.
Baada ya kuona fursa hiyo, akatunga kitabu cha mwongozo wa “jinsi ya kufauru mtihani na akatoa fursa kwa wanafunzi kuweza kulipia na kupata masomo ya ziada. Kitabu pamoja na masomo ya ziada kwa wanafunzi ni vitu vilivyompatia pesa nyingi wakati mwalimu huyo mwingine aliendelea kulalamika huku akiandamwa na umaskini wake kama kawaida. Walimu hawa wawili wanawakilisha makundi mawili ya watu—maskini na tajiri ambao tofauti zao ni fikra tofauti kwa kitu kile kile.
Namba tatu: Matajiri wao hununua vitegauchumi ambavyo baadae uwatengenezea faida na faida hii wao huiwekeza tena na tena. Kitendo hiki cha kurudisha faida kwenye vitegauchumi kila mara, uwapa fursa ya kuifanya faida waliyoipata kuzaa pesa nyingine zaidi.
Namba nne: Matajiri wao hujali sana kuwa na mtandao wa watu waliofanikiwa. Maskini wao upenda kukaa peke yao, kufanya kazi peke yao Matajiri huona umuhimu sana wa kuwa na watu waliofanikiwa.
Unapokuwa na mtandao wa watu
waliofanikiwa unapata nafasi ya kusikiliza simulizi zao za mafanikio, na wakati
mwingine wanapata kukwambia njia sahihi walizotumia kufanikiwa. Mambo yote
mazuri unayojifunza kutoka kwao, ukufanya na wewe upende na kuanza kufanya kama
wao.
Namba tano: Matajiri wao pesa huwafanyia kazi wakati watu maskini hufanyia kazi pesa. Maana yake ni kwamba, maskini wanafanya kazi kwa niaba ya pesa na kwa upande wa pili pesa inafanya kazi kwa niaba ya tajiri. Kinacholeta tofauti hapa ni kwamba kwakuwa tajiri pesa inamfanyia kazi, anakuwa na muda wa kufanya vitu vingine vingi ndani ya masaa 24.
Maskini yeye anafanya kila kitu mwenyewe, kwasababu anaogopa kutumia pesa isije ikaisha—muda wote anajihami pesa isiishe, ingawaje mara zote imekuwa ikiisha bila kujali ubahili wake.
Namba tano: Matajiri wao pesa huwafanyia kazi wakati watu maskini hufanyia kazi pesa. Maana yake ni kwamba, maskini wanafanya kazi kwa niaba ya pesa na kwa upande wa pili pesa inafanya kazi kwa niaba ya tajiri. Kinacholeta tofauti hapa ni kwamba kwakuwa tajiri pesa inamfanyia kazi, anakuwa na muda wa kufanya vitu vingine vingi ndani ya masaa 24.
Maskini yeye anafanya kila kitu mwenyewe, kwasababu anaogopa kutumia pesa isije ikaisha—muda wote anajihami pesa isiishe, ingawaje mara zote imekuwa ikiisha bila kujali ubahili wake.
Tatizo la kufanya kazi
mwenyewe, ni kwamba unatakiwa kufanya kazi muda wote wa Maisha yako, kwani siku
ukiacha pesa nayo inakatika. Ndiyo, maana inakuwa vigumu kusafiri au kufanya
kitu chochote kile nje ya hiyo kazi.
Maisha ya namna hii si
mazuri hata kidogo. Tunahitaji kufanya kazi ambazo mwisho wake zinatupatia
mazingira ya kuwa na uhuru wa kuchagua mambo mbalimbali tunayoyapenda.
Jaribu kutafakari baada ya kusoma makala hii, vuta picha ya maisha yako binafsi na uone kati ya makundi hayo mawili—maskini na tajiri wewe uko wapi na unaelekea wapi hata kama ni miaka 10 ijayo usijali, ilimradi tu una malengo mahususi.
Jaribu kutafakari baada ya kusoma makala hii, vuta picha ya maisha yako binafsi na uone kati ya makundi hayo mawili—maskini na tajiri wewe uko wapi na unaelekea wapi hata kama ni miaka 10 ijayo usijali, ilimradi tu una malengo mahususi.
Ukisha pata picha amua
unataka kukaa katika kundi lipi. Maamuzi yoyote utakayokuwa umeamua yasimamie
na usilalamike hata siku moja. Ikitokea ukaona upande uliochagua kuishi
haukufuraishi tena, basi fahamu kwamba wewe unao uamuzi wa kuhamia upande ambao
unakidhi matarajio yako, kwani kikubwa katika maisha ni Amani na furaha.
Makala hii imeandikwa na Cpyridion
Mushongi wa MAARIFA SHOP.
Mar 20, 2017
Tumia Mbinu Hizi Kubuni Jina La Biashara Yako.
Roho kubwa katika biashara ni jina la biashara yako. Watu wengi wamekuwa wakikurupuka katika kuanza kufanya biashara ila wamekuwa wakisahau ya kwamba kitu ambacho kinaibeba biashara kwa asilimia kubwa ni jina la biashara.Wengi wao wamekuwa wakishirikiana jina la biashara kama ni sehemu ya kawaida sana. Lakini ninachotaka kukwambia haijalishi ni biashara ya aina gani ambayo unafanya hakikisha ya kwamba jina la biashara linachukua kipaumbele.
Hivyo ili kuonyesha ya kwamba unaipenda biashara yako hakikisha inaendana nami siku ya leo kwani nitakueleza kiundani kuhusu mbinu itakapotimia katika kubuni jina la biashara yako.
Bila kupoteza wakati zifuatazo ndizo mbinu za kupata jina la biashara yako.
1.Jina ni lazima liwe fupi.
Imeshauriwa ya kwamba katika kubuni jina la biashara ni lazima uhakikishe unapata jina ambalo ni fupi. Kwani kuwa na jina refu katika biashara yako huwafanya wateja wako waweze kulishau kwa urahisi.
Pia ni vyema jina hilo ambalo utalitumia liwe ni rahisi kutamkika. Na kwa kuongezea tu ni kwamba katika kubuni jina la biashara yako ni vyema ukahakikisha jina unalolitumia lisizidi maneno matano. Kwa mfano kuna mama mmoja yeye huwa anauza mkaa hivyo banda lake ameamua kuliita " mkaa plaza" hivyo hata wewe jaribu kuchagua jina ambalo ni fupi pia ni rahisi kutamkika.
2. Hakikisha ni jina linalo akisi kile unachokifanya.
Katika kitu ambacho unatakiwa kuweza kukifahamu kila wakati ni kuhakikisha unachagua jina ambalo linaendena na kile ambacho unakifanya. Kama unauza nguo basi hata jina liwe katika maahadhi ya biashara hiyo, hata pale mtu anapolisikia iwe rahisi kujua ni biashara gani ya biashara ambayo unaifanya.
Jina linalogusa hisia za watu
Moja kati ya njia bora ya kupata wateja katika biashara yako, ni kuipa biashara hiyo jina ambalo litagusa hisia za wateja wako. Kufanya hivyo kunamfanya mteja wako ajihisi ni sehemu ya biashara yako. Kwa mfano hivi hajawahi kuona mteja fulani akikosa kinywaji fulani ambacho amezoea kunywa hughairisha kabisa? Bila shaka umewahi kuona aina hii ya mteja. Hapa ndipo ninapozungumzia ya kwamba mfanye mteja kuwa sehemu ya biashara yako kwa kutoa huduma bora na kwa wakati sahihi ili kugusa hisia zake.
Jina la kipekee
Hupaswi kunakiri majina ya biashara nyingine.Chagua jina la kipekee ambalo litakutambulisha wewe na biashara yako.Kuipa biashara yako jina la biashara nyingine inaweza kuleta athari kwa biashara yako kwani unaweza kuwa unaitangaza biashara ya mtu mwingine bila kujifahamu hususani kama biashara ya mtu huyo imekuwa kubwa kuliko yako. Kwani hata huyu mwenye biashara yake Atasema wewe ni tawi lake. Hivyo epuka mfanano wa majina.
Lakini nimalize kwa Kusema ya kwamba biashara bora huenda sambamba upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati sahihi na uwepo jina lililo thabiti la kibiashara.
Ndimi afisa Mipango Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com
Mar 17, 2017
Tumia Mbegu Bora Ukuze Kipato Chako.
Leo
tunaendelea na umuhimu wa kutumia mbegu bora kwa mkulima yoyote anayetaka
mafanikio ni lazima atumie mbegu bora ili kuyaendea mafanikio. Mbegu bora ndio
msingi wa mafanikio kwa mkulima.
Naomba
bila kupoteza muda tuangalie utofauti uliopo kati ya mbegu ya kawaida (Open
pollinated varieties OPV) na mbegu chotora (Yaani Hybrids seeds) na ni nini
faida yake kwa mkulima akishajua tofauti hizo.
Kwanza
katika uotaji,mbegu ya kawaida ina husua sua katika uotaji yaani uotaji wake ni
shida lakini mbegu chotora zina uhakika mkubwa sana wa kuota na mkulimahupotezi
pesa yako ukinunua.
Ukichunguza
kwa kina utagundua ndiyo maana mbegu nyingi chotara ukiuziwa uliza kabisa kuna
mbegu ngapi humu ingawa zingine zimeandikwa idadi ya mbegu. Hiyo yote
inaonyesha uhakika wa mbegu hizo.
Ustahimilivu wa magonjwa,Mbegu chotara huwa zina vumilia magonjwa yaani hazishambuliwi ovyo na magonjwa ukitofautisha na mbegu za kawaida hushambuliwa kirahisi na magonjwa.
Ubora
wa bidhaa, mbegu chotara huwa na ubora zaidi baada ya kuvuna ukitofautisha na
mbegu ya kawaida. Ndio maana wakulima wengi wenye mafanikio, hutumia sana mbegu
hizi.
Mavuno
ya mbegu chotara huwa zina mavuno mengi ukitofautisha na za kawaida. Mavuno
haya mara nyingi huwa ni makubwa na kumfanya mkulima kunufaika na kipato
atakachokipata.
Pia
mbegu chotara hutoa mavuno mengi na yaliyo bora (High yield and quality) lakini
za kawaida mavuno kidogo na siyo bora kama ya chotara(Low yield and not
quality)
Kwa mfano mbegu ya nyanya FAIDA F1 3169 na FAIDA F1 3104 huweza kuvunwa zaidi ya miezi sita na huzaa matunda mengi sana.
Hivyo
hata katika soko huwezi pambana na mtu aliyelima mbegu za kawaida na aliye lima
mbegu chotara, kwa mfano mtu atakaye lima nyanya mfano tanya hawezi fanana na
mtu aliye lima FAIDA F1 NTH 3104 au FAIDA F1 NTH 3169.
Pia
hata Yule aliye lima FAIDA F1 atauza bei ya juu (mara mbili au mara tatu zaidi)
kuliko aliye lima nyanya ya kawaida, kwa kuwa zina ubora ulio tofauti. Kwa hilo
hiyo mkulima hawezi kupata hasara kirahisi.
Naomba
sana utambue hivi ili uweze kuingia katika kilimo na ukapata matokeo chanya,
hutakiwi kukurupuka. Kaa chini, utulie, fanya uchunguzi wale wanaofanikiwa
kwenye kilimo wanafanya nini cha ziada.
Kilimo
cha manufaa hakiendeshwi kwa mihemuko au kwa whats app. Unataka kulima na
umelenga kupata matokeo mazuri na hujui wapi pa kuanzia waone wataalamu wa
kilimo.
Kazi
kwako kwa wewe mkulima unaye taka mafanikio, tumia mbegu bora (Hybrid seeds)
zikuletee mafanikio. Tukutane wiki ijayo kwa makala nyingine nzuri ya kilimo.
Wako
mtaalamu wa kilimo,
Boniface L Pwele.
Kwa msaada zaidi wa kuendesha kilimo
chenye mafanikio, usisite kuwasiliana
nasi. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0762567628 au tuma ujumbe kwa barua
pepe blugahno95@gmail.com
Mar 16, 2017
Biashara Nzuri Ambayo Unaweza Ukaifanya Na Kupata Faida Kubwa Ni Hii Hapa.
Habari za leo, mpenzi msomaji wa safu hii ya
biashara? Nikukaribishe kwa moyo mkunjufu ili tuweze kujifunza na elimu
hii ya biashara. Andaa ubogo wako ili uweze kupokea mambo muhimu ya kukusaidi kufanikiwa.
Moja ya maswali ambayo nimekuwa
nikiulizwa sana na wasomaji wetu ni kwamba je, afisa mipango Ben, nifanye
biashara gani ambayo itakuwa ina faida kubwa kwangu?
Kama ambavyo nimekuwa nikiulizwa mara
kadha wa kadha na swali hilo tena limekuwa likijirudia. Hivyo kwa kutumia
dakika chache naomba niweze kujibu swali hilo.
Jambo la msingi sana ambalo unatakiwa kulizingatia ni
kwamba kila biashara ambayo unaiona machoni mwako ina faida na hasara
zake, Nimeanza kwa kusema hivyo kwani watu wengi wamekuwa wakiaangalia
upande mmoja tu wa kupata faida tu.
Lakini ukweli ambao unatakiwa kuujua
mapema ni kwamba kabla ya kuingia katika biashara tambua ya kwamba katika
biashara hiyo kuna faida na hasara, hivyo uwe tayari kubeba mambo hayo mawili
pindi yatakapojitokeza.
Biashara yenye faida huanza na wazo, wazo ambalo
limekuwa likitokana na mfanyabiashara kabla ya kuanza kufanya biashara husika.
Wazo hilo hujengwa na misingi ya kina ya kufanya uchunguzi yakinifu juu ya
biashara hiyo.
Usipofanya uchunguzi wa kutosha juu ya biashara unayotaka
kuifanya ipo siku utalalamika. Ila tunashauriwa ya kwamba katika kufanya
uchunguzi wa kutosha ni lazima ujikite katika kuangalia eneo ambalo utaiendesha
biashara hiyo.
Wakati unangalia eneo kwa ajili ya kufanyia biashara,
angalia eneo ambalo:-
Eneo linalofikika kwa urahisi.
Angalia eneo ambalo lina uwingi wa mkusanyiko mwingi wa
watu tofauti tofauti.
Tafuta eneo ambalo kuna upatikaji wa huduma za kijamii,
kama vile ukaribu wa benki, umeme, maji na mengineyo mengi yatakoyokusiadia
kukua kibiashara.
Angalia eneo ambalo lipo karibu na wafanyabiashara
wengine. Kwa mfano, kama unafanya biashara ya mashati basi chagua eneo
ambalo kuna mfanyabiashara anauza tai. Kufanya hivi kuna msaidia mteja kutopata
tabu ya kuhangaika kupata bidhaa fulani.
Lakini kubwa kuliko yote ni kwamba katika kufanya
uchunguzi wa eneo la kufanyia biashara ni vyema unafanya uchunguzi kwa
kuangalia hasa ni yapi mahitaji ya watu. Kisha wewe uweze kuyasogeza
mahitaji hayo karibu.
Mwisho naomba ujiulize hivi, ni wapi ambapo imepanga kufanya biashara
h? Na watu wana changamoto zipi nawe umekuja suluhisho lipi? Ukipata majibu hayo huo ndio utakuwa
mwanzo wa kujua biashara gani italipa eneo hilo na hatimaye kupata faida.
Hivyo niseme hivi, biashara inayolipa
na kutoa faida kubwa ni ile biashara ambayo umeshaifanyia uchunguzi wa kutosha
na kujua soko lake liko wapi na lina ukubwa gani. Hiyo ndiyo biashara
inayolipa.
Endelea kujifunza maisha, mafanikio
na biashara kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku, usikose kumshirikisha
na mwingine ili aweze kupata maarifa haya muhimu.
Afisa mipango Benson Chonya,
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)