May 15, 2017
Faida Ya Kufikiri Kama Tajiri Hata Kama Huna Kitu Mfukoni.
Kuna
wakati unakuwa unashangaa kwa nini watu wengine ni matajiri sana na wakati
wengine ni maskini. Najua umekuwa na mawazo mengi juu ya hili na kufikiri
pengine hawa ni watu wenye bahati sana, wamezaliwa kwenye familia tajiri au
pengine watu hawa wana kazi nzuri na wamezaliwa kwenye nchi zenye mafanikio.
Ni ukweli,
yote haya yanaweza kuwa majibu kwa namna fulani, lakini hata hivyo kipo kitu
kimoja muhimu sana ambacho kinafanya watu wengine kuwa matajiri na wengine
kuendelea kubaki kwenye umaskini. Kitu hiki ambacho kinaleta tofauti zote hizo
si kingine bali ni mawazo yako.
Badala
ya kuendelea kulalamika kwa nini upo kwenye hali ngumu, kwa nini maisha yako
yako magumu, kwa nini hufanikishi malengo yako fulani ambayo unayatamani sana
karibu kila siku, kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kukiangalia, angalia sana
mawazo yako hasa linapokuja suala la pesa.
Fikiri kwa mafanikio. |
Mawazo
yetu mara nyingi sana yana nguvu ya kutupa kitu chocho ambacho tunakihitaji
katika maisha yetu. Mawazo yetu yamepewa uwezo wa kuumba fursa na kila hali
ambayo tunaitaka ijitokeze kwetu. Kinachotakiwa kufanyika ni kuamua kutumia mawazo haya kwa ufasaha hadi kuweza kutufanikisha.
Kwa hiyo
mpaka hapo unaelewa kabisa faida kubwa ya kufikiri kama tajiri hata kama huna
kitu mfukoni inakusaidaia wewe kuweza kupata kile unachokihitaji kwa hatua. Ni
suala la kuujaza ubongo na akili yako taarifa za kitajiri, taarifa za mafanikio
na hapo utatengeneza mazingira mazuri ya kufanikiwa.
Epuka
sana kuwa na mawazo mgando, mawazo ambayo kila wakati yanalenga kukukwamisha. Ukiwa na mawazo hayo
utateseka sana kwenye dimbwi la umaskini na hautaweza kutoka hapo. Kikubwa endelea
kuwa chanya mpaka kuhakikisha ndoto zako zinatumia na kuwa kweli.
Ansante
sana kwa kuendelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Nikutakie
siku njema na kila la kheri katika kuyafikia mafanikio yako makubwa.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.