May 30, 2017
Fanyia Kazi Mambo Haya, Ili Kuendelea Kujenga Msingi Mkubwa Wa Mafanikio Yako.
1.
Zipo kelele nyingi sana katika dunia hii ya habari. Utasikia hiki mara utasikia
kile. Usipokuwa makini utajikuta kila kitu unataka kufatilia. Sasa njia ya
kuweza kujiokoa na kelele hizo na kuweza kufanikisha malengo yako ni kwa wewe
kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kile unachokifanya.
Angalia
kipi unakifanya, kisha kifatilie kitu hicho kila siku. Kelele za huku mara kule
acha kuzifatilia zitakupoteza. Kumbuka, mikwenzi mingi ilimpoteza mbwa
mawindoni, usiwe miongoni mwa watu watakao potea kwa sababu ya kelele. Simamia
na fatilia mipango yako kwa kuweka nguvu za uzingativu kwa kile ukifanyacho na
utafanikiwa.
2.
Maisha na mafanikio ya kweli yanakuja kwa wewe kuweka thamani na kutoa mchango
mkubwa kwa wengine. Mafanikio hayaji kwa bahati nasibu au chochote kile ambacho
kipo kwenye njia ya mkato. Mafanikio ya kweli yanatengenezwa sana na kwa wewe
kuendelea kuweka thamani na kutoa michango kwa wengine.
3.
Kila wakati tafuta mafanikio yako kwa kufanya kile unachokipenda. Unapofanya
kile unachokipenda utake usitake ni lazima utajituma tu bila hata kusukumwa.
Kupenda kile unachokifanya, kazi kwako itakuwa ni kama mchezo na kwa kifupi ni
rahisi tu kuwa mlevi wa kazi yaani ‘workaholic’
hasa kama unafanya kile unachokipenda.
Mara
nyingi unapoona watu wanasukumwa sana katika kazi zao, na ni watu ambao kama
hawajitumi ni rahisi kujua watu hao wanafanya kazi ambazo hawazipendi na wala
hazipo kwenye mioyo yao. Wanafanya ili mradi siku ziende. Timiza mipango
uliyojiwekea, kwa kuchagua kile unachokipenda kwenye maisha yako na kifanye.
4.
Wakati tukiwa vijana wadogo wengi wetu tulikuwa na ndoto nzuri sana kwamba
nikikua nitafanya hiki au kile na ilikuwa rahisi kuweza kuona kama vile kila
kitu kinawezekana na wala hakuna changamoto kubwa sana.
Lakini
kwa kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda zile ndoto zetu zilianza kupotea
hasa baada ya kukumbana na changamoto za kimaisha za hapa na pale. Kitu cha
kujiuliza kwako kwa mfano je, ile ndoto yako ya utotoni unayo au imepotea?
Kwa
vyovyote vile ilivyo ndoto yako ipo ila kikubwa ulichokifanya umeizika ndoto
yako bila kujua.Umeshindwa kufanya namna nzuri ya kuweza kuifufua ndoto yako na
kuiweka wazi hadi iweze kufanikiwa.
Sasa jiulize hivi kama huna mpango na ndoto yako
ambayo ulikuwa unapienda, kwa sasa unaishi maisha a aiana gani? Ni rahisi
kukwama katika maisha na kupata ugumu fulani kama hufuati ndoto yako na hufanyi
kile kitu unachokipenda maishani.
Kuanzia sasa jipe muda wa kufikiri tena na anza
kufatilia ndoto yako ile ambayo ulikuwa umeisahau. Kaa chini ujiulize una ndoto
ipi ambayo unatakiwa kuifailia? Kisha anza kuifatilia ndoto yako na itakuwa
kweli.
5.
Kuna wakati tunajiambia sana ‘mwaka huu nahitaji kuongeza mtaji, mwaka huu
nahitaji pia kufanya biashara ile, au mwaka huu nahitaji kufanya hiki au kile’.
Hizi ni sentensi ambazo naamini umezisikia sana zikisemwa na kuna kipindi hata
wewe umekuwa ukijisemea hivyo.
Katika
ulimwengu wa mafanikio ipo hivi kile kinachokufanikisha si kile unachokihitaji,
bali kile kinachokufanikisha ni kile unachokifanya au kukifanyia kazi, ndicho
hicho kinachokufanikisha na kukupa mafanikio.
Hakuna
atakayejali kwa kile unachohitaji au unakisema sana hata kiwe kizuri vipi,
dunia inajali kile unachokichukulia hatua na kukifanya. Hicho unachokifanya
kila siku, hicho ndicho kinachokusogeza kwenye mafanikio yako.
Unaweza
ukahitaji mambo mengi sana lakini kama huchukui hatua uwe na uhakika huwezi
kufanikisha kitu chochote katka maisha yako, zaidi yako utaishia kusema nahitaji
hiki au kile na miaka inaenda na bado ukajikuta hupati kitu.
Kuna
watu ambao ukiwachunguza karibu maisha yao yote ni watu wa kusema nitafanya
hiki mwaka huu au kile na hawafanyi. Maisha ya mafanikio hayataki ‘blaa blaa’
yanataka ufanye kitu yaani uchukue hatua za kimafanikio.
Kumbuka
unachokihitaji hakiwezi kukupa mafanikio unayoyataka kwa asilimia zote, acha
kulinga na kujidai kwa kile tu unachokihitaji, badala yake uelewe kabisa kile
unachokifanya hicho ndicho kitakachokupa maisha na mafanikio unayotaka.
6.
Kipimo cha mafanikio yako kipo kwako
wewe mwenyewe na wala hakipo kwa mtu mwingine. Njia pekee itakayokufanya uweze
kupima mafanikio yako ni kwa kwewe kuangalia hatua unazozipiga kulekea kwenye
mafanikio hayo.
Mafanikio
yako hayapimwi kwa kuangalia mafanikio ya mtu mwingine. Bali mafanikio yako
yanakuja kwa sababu ya zile hatua zako mwenyewe unazotakiwa uzipige kila siku
kuelekea kwenye mafanikio.
Unawezaje
sasa kujua kama umefanikiwa ikiwa hujilinganisha sana na wengine? Hilo ni
rahisi tu, ni kwa wewe kuangalia ni hatua gani umepiga ukijilinganisha na mwaka
jana au wakati uliopita.
Kumbuka
kila siku hili, chukua hatua kila siku za kuelekea kwenye kile unachokifanya.
Usijali wala usiangalie ikiwa unachukua hatua kidogo, kitu cha msingi chukua
hatua kwani hicho ni kipimo cha mafanikio yako.
7.
Kuna wakati tunakutana na ugumu sana katika kufanya vile tunavyotaka kuvifanya.
Kutokana na ugumu huo na kuna wakati huweza kujikuta hata tukitaka kuahirisha
kufanya mambo yetu. Kwa hali yoyote unayokutana nayo hata kama ni ngumu vipi,
hebu hicho unachotaka kukifanya kifanye.
Usiahirishe
mambo yako kwa sababu ya ugumu, fanya hivyo hivyo, ‘just do it,’. Weka
visingizio pembeni, usiwe kama mtoto mdogo ambaye kila kitu anasingizia.
Tengeneza ukomavu wa kiakili kwa kuamua kufanya hata kama ipo shida na ugumu
vipi wewe fanya kwa kusukuma na utaona mafanikio yakijitokeza kwako.
Nakutakia
siku njema na kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea
DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza kila
siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713
04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.