May 17, 2017
Jinsi Unavyoweza Kutengeneza Bahati Yako Ya Mafanikio.
Sina
shaka umeshawahi kukutana na watu ambao wewe kwa haraka haraka ulikiri watu hao
wana bahati sana katika maisha yao. Labda nikuulize tena je, umeshawahi
kukutana na watu wenye bahati na hadi na wewe kutamani kuwa kama wao?
Hapa
sitaki unipe jibu, baki nalo kimya kimya ila ninachotaka kukwambia ni kwamba hata
wewe unaweza ukawa na bahati na ukawa na mafanikio. Naona unaanza kushangaa,
sikiliza, yapo mambo mawili tu ya kukufanya ili uwe na bahati.
Kama
utaweza kuyatumia mambo haya vizuri na kwa ufasaha basi jiandae na wewe kuitwa mtu
wa bahati, ingawa bahati kama bahati kiuhalisia haipo kwenye maisha. Unashangaa?
Ndiyo haipo, ila inatengenezwa, kivipi?
Bahati inatengenezwa. |
Kwanza, tafuta fursa ambapo pale wengine
hawaoni.
Fursa
yoyote unayoitafuta katika maisha yako haiji hivi hivi tu inakuja kwa wewe kuwa
na jicho la kuona vitu vya ziada ambavyo wengine hawawezi kuviona. Kama una
uwezo huo wa kuona yale ambayo wengin hawaoni, hapo ndipo wengine wataanza kuona
una bahati.
Utakua
pale ambapo watu wengine labda wanalalamika maisha ni magumu lakini wewe pale
ndipo unapoona kitu cha kufanya. Ili kufanikiwa na kuwa na jicho la namna hii
ni lazima ujue kufikiri kwa utofati.
Anza
kufikiri watu hawa wanapata chnagamoto gani kubwa, kipi kinachowasumbua? Ukishaligundua
hilo wape watu hao kitu hicho na kila kitu kitaweza kufanikiwa na kuwa cha mafanikio
makubwa na wengine watakuona ni kama vile una bahati.
Tatizo
la watu wengi hawataki kufikirisha bongo zao. Wanataka kuwa ni watu wa kulala
na kuamka bila kuwaza ni kipi cha kufanya au ni kipi ambacho jamii inakihitaji
na wakitumie kama fursa ya kutoka kimaisha.
Karibu
siku zote watu wenye jicho la tatu, watu ambao wanaona mapema fursa kuliko
wengine hao ndio hujikuta wakiitwa ni watu wa bahati. Je, leo na wewe unataka
kuwa mtu wa bahati, tafuta fursa ambapo pale wengine hawaoni.
Pili, jiandae kwa fursa.
Wale
watu wanaoitwa watu wa bahati ni watu wa kujiandaa na fursa, ni watu wa kukaa
na kuachia masikio yao huko na kule na kuangalia fursa sahihi kwao ambayo
inaweza kuwafanikisha na kufika kwenye kilele cha mafanikio.
Kujiandaa
kwa fursa hakuji hivihivi tu unatakiwa ujenge nidhamu. Na nidhamu inajengwa
sana kwa wewe kuamua kuweka juhudi zaidi karibu kila siku ili uweze kufanikiwa
kwa unachokihitaji maishani mwako.
Kwa hiyo
mpaka hapo unaona unatakiwa ujenge nidhamu ya kujifunza, unatakiwa ujenge
nidhamu ya kukusafanya mtaji na pia unatakiwa ujenge nidhamu ya kuwa na matumizi mazuri ya pesa
yatakayoweza kukupelekea ukawa mwekezaji mzuri.
Kwa kujua
mambo hayo mawili yaani kutafuta fursa ambapo kuna wale wengine hawaoni na
kujiandaa na fursa ni mambo ambayo yana uwezo wa kukufanya na wewe ukaonekana
na wewe una bahati katika maisha yako.
Nikutakie
siku njema na kila la kheri katika kufikia ndoto zako zikawa za kweli.
Ni wako
rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713
04 80 35,
dirayamanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.