May 8, 2017
Rasilimali saba (7) zinaweza kukupa mafanikio.
Moja ya changamoto kubwa
itukumbayo watu wengi ni ile hali tunayoshindwa kutumia vizuri rasimali
tulizonazo. Wengi huwa tunazichukulia ya kwamba rasilimali tulizonazo si kitu
katika kutuletea mafanikio. Lakini ukweli ambao upo wazi ni kwamba rasilimali
ni zawadi pekee ambayo ni zawadi tosha kwetu sisi kuweza kufanikiwa.
Swali la msingi ni je
tunazitumiaje rasilimali hizo kuwa fursa? Hapo ndipo palipo na changamoto kwa
watu wengi. Na daima ukumbuke ule usemi mzuri usemao kuzaliwa Masikini si
Kosa ila Kosa ni wewe kufa Maskini. Na kufa kwako maskini inategemea sana kwa
kutokutumia vizuri rasilimali zifuatazo.
1.Uhai.
Katika zawaidi na
rasilimali kubwa ambazo mwenyezi Mungu amekutunuku ni pamoja na uhai. Uhai
ndiyo zawadi pekee ambayo ni vyema ukaitumia vyema katika maisha yako.
Rasilimali hii ndiyo ambayo kila mmoja wetu anabidi aitumie vyema katika
kubadili maisha yake. Kwanini ufe maskini na ili hali wewe u hai? Tafakari
kisha tafuta majibu ya maswali yako.
Uhai huu tulionao hatuna
budi tuutumie vyema, kwani mwenyezi Mungu ana makusudi ya dhati na sisi.
Mwenyezi Mungu katupa uhai huu pasipo kutumia hata shilingi moja. Kama ndivyo
hivyo naomba utafakari tena ni kwanini ufe maskini? . Uhai ulionao hakikisha
unafanya kitu ambacho kitaacha alama duniani kote kabla hujarudi mavumbini.
2. Muda.
Muda ni rasilimali
nyingine ambayo itakufanya wewe uweze kufikia ndoto yako endapo utaamua kutumia
vyema muda ulionao. Katika hili ni vyema ukatenga kwa kila siku walau saa moja
ambalo litakufanya uweze kufikiri ni jinsi gani utaweza kufikia vyema ndoto
uliyonayo. Muda ni rasilimali kubwa sana ambayo watu wenye mafanikio huweza
kuutumia kama silaha dhidi ya umaskini.
3. Akili.
Kila mwanadamu katika
ulimwengu huu ana akili. Na akili hizi ndizo ambazo humtofautisha mtu mmoja na
mwingine. Akili ndiyo msingi mkuu wa kumfanya mtu mmoja atofautie na mwingine. Akili ni njia ambayo itakufanya uweze kutimiza
kusudio lako la kuwepo duniani hapa. Akili ndiyo rasimali tosha inayomfanya mtu
afikiri nini afanye na nini asifanye. Hivyo nikusihi ifanye akili iweze
kufikiri kabla ya kutenda, kwani changamoto kubwa ambayo inawafanya watu waweze
kuwa maskini ni vile mtu anavyoamua "kutenda bila kufikiri" au
"kufikiri bila kutenda'.
4. Nguvu.
Nguvu uliyonayo itumie vyema katika kutenda kazi mbalimbali. Lakini kutenda
huku si kutenda tu, la hasha bali ni kutenda bidii. Kufanya kazi bila kuonyesha
juhudi za maksudi ni sawa na bure.
5. Kipaji/ talanta.
Rasimali nyingine
uliyonayo inayoweza kukufanya uweze kufanikiwa ni kipaji. Watu wengi
wenye mafanikio waliweza kutumia kipaji kwa asilimia kubwa, na leo tumeshuhudia
ya kwamba mafanikio yamekuwa upande wao. Hivyo tumia talanta kama sehemu ya
kukutoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Je kipaji ulichonacho
kinakusaidia? Kama jibu ni hapana basi endelea kusoma mahali hapa kwani siku
sijazo nitakueleza jinsi ambayo utaweza kugeuza kipaji hicho kuwa pesa.
6. Ardhi.
Ardhi pia ni sehemu ya
maisha yako, kila kitu unachokitaka kukifanya lazima kiwe na mahusiano ya
karibu na ardhi. Tafakari kwa umakini juu ya ardhi hii kisha uone fursa lukuki
ambazo zimejificha katika ardhi, fursa hizo lukuki zitakusaidia kuweza
kufanikiwa katika maisha yako.
7. Watu.
Rasilimali ya mwisho ambayo tutaijadili siku ya leo, ni kuhusu watu ambao
wanakuzunguka. Kila kitu huwezi kufanya bila kushirikisha watu. Kama ni
biashara inahitaji wateja, kama ni shule inahitaji wanafunzi, kama ni kanisa au
mskiti nalo linahitaji watu pia.
Hivyo ni vyema ukaweza
kuwatumia watu mbalimbali kuweza kufikia lengo lako. Kama unataka mfanyabishara
tunachotegemea kuona kwako ni kuona rafiki zako wakubwa ni wafanyabishara
wanzako.
"Kwani kuna usemi
unao sema tutajie rafiki zako tujue tabia zako"
Hivyo hakikisha unazungukwa na marafiki wenye tija kila wakati.
Hivyo hakikisha unazungukwa na marafiki wenye tija kila wakati.
Bila shaka umenielewa
vizuri, kama umeshindwa kutumia vyema rasimali hizi basi "subiri
kumshuhudia simba akila majani"
Ndimi afisa mipango
Benson Chonya
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.