May 4, 2017
Mambo Matatu Yakuepuka Katika Safari Yako Ya Mafanikio.
Kuna wakati
umekuwa unajilaumu kwamba maisha yamekuwa ni magumu, wengine husema wamelogwa,
wengine husemwa hawana bahati na meneno mengine kama hayo. Hizo sababu
zinginezo ni woga binafsi ambao kimsingi kama utaendelea kuzibeba basi
kufanikiwa kwako itakuwa ni ngumu. Lakini ukweli ni kwamba adui namba
moja wa maisha yako ni wewe mwenyewe.
Na adui huyu
ni mbaya sana, kwani hatima ya maisha yako unayo mwenyewe, kwanini ubaki
kuwanyoshea vidole watu wengine? Na ili hali wewe ndio mmliki mkuu wa maaumuzi
yako? Nilichogundua ni kwamba watu wengi tunashindwa kufanikiwa kwa sababu ya
mambo haya;
1. Kusubiri mtu mwingine akufanyie maamuzi.
Kama
tulivyosema hapo awali ya kwamba maisha yako yapo mikononi mwako kwanini
uache mtu mwingine afanye maamuzi juu ya maisha yako? Na jaribu kuwaza kwa
sauti ila sipati majibu.Nasema hivyo kwa sababu maisha yetu yanakuwa ya kawaida
kwa sababu tunapenda kuwaruhusu watu wengine watoe maaumuzi katika kutenda
jambo fulani.
Lakini ukweli ni kwamba
ukitaka kufanikiwa jaribu kutafakari juu ya maisha yako na uamue kutoa maaumuzi
juu ya jambo hilo. Lakini pia baada ya kutafakari ni nini cha kufanya jambo la
msingi ni kuhakikisha unapata mtu sahihi wa kukushauri ni nini ufanye katika
jambo hilo ili uwe bora zaidi.
Fanya maamuzi yako sahihi. |
2. Kukata tamaa mapema.
Watu wengi
sana huwa tunaathiriwa na ugonjwa huu wa ukataji tama mapema, na hii ni
kwasababu wengi wengi wetu huwa tunapenda matokea ya papo kwa papo. Ila ukweli
ni kwamba mafanikio ya papo kwa papo hakuna labda uamue kucheza bahati nasibu.
Ila kama unataka matokeo
ya uhakika na yenye kuleta mafanikio ya kweli unachokihitaji ni kuwa mvumilivu
kwa kila hatua ambayo unapiga kila siku katika jambo ambalo unalolifanya.
Hivyo niweke
nukta katika maelezo haya kwa kusema ya kwamba kuwa mvumilivu kila wakati.
Kwani mvumilivu hala mbivu, ila kumbuka kuongeza hatua za kiutendeji
ambazo zitakufanya uweze kusonga mbele na si kukata tamaa. Kwani kukata tamaa
ni chukizo mbele za Mungu wetu.
Usikate tamaa mapema |
3. Kuridhika mapema.
Kuridhika
mapema ni adui mkubwa wa mafanikio yako, naomba hili libaki kichwani mwako.
Mafanikio hayana ukomo, kila siku na kila wakati ona kabisa bado hujafanikiwa
hata kama watu wanasema umefanikiwa. Usibweteke na hali uliyonayo. Daima
kumbuka ya kwamba "Mafanikio ni njaa isiyoisha" hivyo kuridhika ni
kurudi nyuma katika hali ya kiutendeji.
Nimalizie kwa
kusema tena mafanikio hayana ukomo, hivyo achana na tabia ya kuridhika mapema.
Ndimi afisa
mipango; Benson Chonya
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.