May 2, 2017
Tumia Mbinu Hii Ili Kupata Majibu Ya Changamoto Inayokukabili.
Je wewe ni
miongoni mwa watu ambao hukata tamaa katika maisha? Kama jibu ni ndiyo makala
hii inakuhusu sana, cha msingi nakusihi usome makala haya mwanzo hadi mwisho.
Maisha ya
mwanadamu yamejawa na changamoto na shida mbalimbali. Changamoto hizo hizo,
wapo baadhi ya watu huzivumilia katika kutenda jambo fulani, lakini pia wapo
baadhi ya watu hukata tamaa kabisa. Na hao ambao hukata tamaa ndio ile idadi
kubwa ya watu ambao hufa ni ndoto zao mapema.
Lakini ukweli
ni kwamba changamoto na shinda mbalimbali za maisha ni kipimo cha akili, kwani
wapo baadhi ya waimbaji wa nyimbo huimba katika nyimbo zao na kusema changamoto
ni majaribu, na majribu ni mtaji. Hivyo katika maisha haya ni jambo la ajabu
sana kama utaendelea kukataa tamaa katika maisha yako kwani hakuna dhambi kubwa
kama kukata tamaa.
Na ukweli ni
kwamba ili uweze kufanikiwa wanasema changamoto hazikwepeki, na changamoto ndio
njia ambayo itakufikisha kule ambapo unataka kufika, endapo tu utaamua
kupambana na changamoto hizo.
Swali
linakuja nawezaje kupambana na changamoto hizo?
Jambo la
msingi unalotakiwa kufanya ni kuhakikisha unapambana na changamoto za maisha
ni;
Orodhesha
changamoto zote ambazo zinakukubali. Hata kama zipo zaidi ya changamoto tano
ziandike zote.
Baada ya
kuorodhesha changamoto hizo tano, jambo ambalo unatakiwa kufanya baada ya hapo
unatakiwa kuchugua jambo ambalo lina umuhimu sana katika kulitekeleza.
Baada ya
kulipata jambo hilo, usiishie kulichagua tu. Tafuta mbinu ya jinsi ya
kuondokana na changamoto hiyo. Na mbinu hizo ziandikwe mahali ambapo
panaonekana na uanze utekelezaji mara moja.
Mbinu hii ya
kupambana na changamoto itakusaidia sana katika kupiga hatua mbele zaidi
kivitendo kuliko kukata tamaa.
Nimekupa mbinu hii, kwa sababu wengi wengi huwa tunajitenga na changamoto za kimasha hasa pae zinapojitokeza.
Nimekupa mbinu hii, kwa sababu wengi wengi huwa tunajitenga na changamoto za kimasha hasa pae zinapojitokeza.
Lakini kama nilivyoeleza
hapo awali ni kwamba changamoto za kimaisha ni kigezo tosha cha kuweza kutimiza
ndoto yako, jambo la msingi tafuta majibu ya jinsi ya kuondokana na changamoto
hiyo.
Kama
hutatafuta majibu ya changamoto zinazokukabli itakuwa ni sawa na bure, kwani
utazidi kuwa maskini maisha yako yote.
Ndimi; Afisa
mipango Benson Chonya,
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.